Fredrick Lowassa, mbona kimya Bungeni?

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Mar 1, 2016
5,474
2,000
Monduli hakuna matatizo aongee nini?jamii yake ni watu wa kuhama hama, mifugo na wanyama pori.
 

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
24,680
2,000
Mkuu ukiiangalia tu ' Body Language ' ya Fredy Lowassa huhitaji ' IQ ' kubwa kugundua kuwa huo Ubunge alionao sasa Yeye hakuutaka ila 'alishinikizwa' na 'kulazimishwa' na Hayati Mwendazake ili tu 'Kumfurahisha' na hata 'Kumpoza' Baba yake na 'Maumivu' pamoja na 'Mateso' ambayo CCM na Serikali yake walimpatia Mzee wa Watu ili tu 'Kumkomoa' na arejee rasmi Chamani ( CCM ) na akarudi kweli.
Siasa za mwendazake zilikuwa za ki-analogy sana!!
 

The Khoisan

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
13,379
2,000
Ni takriban miezi saba sasa tangu uwepo wa bunge hili, Mbunge wa Monduli Mh. Fredrick Lowassa hatujamsikia akichangia chochote kama alivyokuwa mtangulizi wake, Mh. Julius Kallanga aliyekuwa na makeke sana?

Au naye kajiunga kwenye kundi la Mh. Abood yule wa Morogoro asiyechangia bungeni?
Like father like Son ...................!!
 

Valuhwanoswela

JF-Expert Member
Jun 27, 2019
1,223
2,000
Ni takriban miezi saba sasa tangu uwepo wa bunge hili, Mbunge wa Monduli Mh. Fredrick Lowassa hatujamsikia akichangia chochote kama alivyokuwa mtangulizi wake, Mh. Julius Kallanga aliyekuwa na makeke sana?

Au naye kajiunga kwenye kundi la Mh. Abood yule wa Morogoro asiyechangia bungeni?
Alifuata maslahi kama Wabunge wengine wote wa CCM na anapata, kelele za nini?
 

Mikono yenye Sugu

Senior Member
Jul 1, 2020
133
250
Hebu watafute wabunge wanaochonga sanaaaaa mfano Kibajaj, Msukuma n.k...

Halafu rudi kutazama maendeleo katika majimbo yao na uyalinganishe na majimbo ya wabunge watulivu bungeni...

Baada ya hapo tutaweza discuss hili la mwana wa Lowassa kuwa 'bubu bungeni'
Huyo Fred bungeni haongei na unaambiwa jimboni hakuna cha maana kinachoendelea. Akitoka zake Dodoma ni Dar...! Masaini aende kufanya nini huko? Na hata akiendea kampani yake ni ya wachapa kinywaji na hana muda wa kuonana na watu wa kawaida.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom