Freddy Mayaula Mayoni AFARIKI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Freddy Mayaula Mayoni AFARIKI

Discussion in 'Sports' started by Challenger, May 31, 2010.

 1. Challenger

  Challenger Member

  #1
  May 31, 2010
  Joined: Sep 5, 2007
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  JF members,

  Ni jambo lakusikitisha kuwa Afrika imempoteza mwanamuziki nguli, Freddy Mayaula Mayoni, tarehe 26 Mei 2010, ni siku ambayo Mayaula amemaliza maisha yake hapa duniani.

  Mwandishi mzuri wa mashairi ya muziki na pia mpiga gita la kati (rythim), pamoja na mwanasoka aliyewahi kuchezea klabu ya Yanga, amefariki Brussels – Ubeligiji akiwa baada ya kuugua kwa muda mrefu kutokana na ugonjwa wa kiharusi (stroke); ambayo ilimpata akiwa hapa Tanzania (Dar-es-salaam) miaka ya 2006.

  Wengi, uhusuani wale wapenzi wa Franco akiwa na bendi yake ya TP OK Jazz, watamkumbuka Mayaula kutokana na album zake hasa ile ya Mizele iliyotolewa miaka ya 1990 na L'Amour Au Kilo iliyotolewa miaka ya 1993 ikiwa na wimbo uliopendwa “Mbongo”. Nyimbo nyingine alizowahi kutunga akiwa na TOP OK Jazz ni kama Nabari Misere (ambao uliimbwa kwa ufundi mkubwa na mwanamuziki mwingine ambaye pia ni marehemu, Djo Mpoy Kaninda), na pia wimbo Cherie Bondowe.

  Mwanamuziki Freddy Mayaula Mayoni amefariki akiwa na umri wa miaka 64, akiungana na wanamuziki wengine aliowahi kupiga nao akiwa na bendi ya TP OK Jazz kama Madilu System, Franco, Djo Mpoy Kaninda, Aime Kiwanaka, Dalienst Ya Ntesa, Lola Checain, Decca Mpudi, Gerry Dialungana, Mongo, Ntoya Pajos, Empopo Loway, Issack Musekiwa, Rondot Kasongo nikiwataja kwa uchache.
  Mungu aiweke Roho Ya Marehemu Freddy Mayaula Mayoni mahali pema Peponi – AMENI

  Kisondella

  [​IMG]
   
 2. Mkosoaji

  Mkosoaji JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kifo chake ni ishara ya kumalizika kwa 'music era' ya 70s na 80s huko Congo. RIP Mayaula.
   
 3. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #3
  May 31, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  RIP Mayaula
   
 4. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #4
  Jun 3, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Ana nyimbo yake hiyo inaitwa Othman Bakayoko kaiimba kama slow flani hivi ni Balaa.
  Na nyingine iliitwa L'amour dah ni nyoko kwa kweli...

  Tangulia Mjomba, sie huku hatujui lini tamati.
   
Loading...