TANZIA Mwanamuziki mkongwe wa DRC, Josky Kiambukuta Londi afariki Dunia

luambo makiadi

JF-Expert Member
Nov 28, 2017
10,295
8,258
Habarini za usiku wakuu, kwa masikitiko mwanamuziki Josky Kiambukuta amefariki dunia mapema Leo huko Kinshasa.

Marehemu Josky Kiambukuta alikuwa mwanamuziki hodari aliyeimba katika bendi ya Tp okk jazz ya marehemu Franco, alijiunga na band hiyo mwaka 1973.

Nyimbo maarufu za marehemu Josky Kiambukuta Londi Ni Chandra, sincerite, ayez pitie n.k

Alizaliwa 14 February 1949

Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pepa peponi

Sehemu ya kazi yake:



Cc
Lucas Mobutu
Masiya
 
Kuna watu wakifariki inabidi ku-celebrate maisha yao kwa urithi wanao acha nyuma. Commandant Josky ni mmoja wao. 1969 alikuwa na Dr. Nico halafu akaingia Continental Orchestra na 1973 rasmi akakaribishwa TP OK JAZZ ya Luambo na Lutumba. Huyu ndio sauti ya OK Jazz kwani ameshiriki kuimba nyimbo nyingi kuliko muimbaji yeyote wa TP OK JAZZ.

Anaimba kwa madaha sana na hupanda na kushuka. Lakini pia ni mtungaji nyimbo wa kiwango cha juu kabisa akiwafuatia Franco na Simaro kwa ubora na wingi wa tungo zake. Ameacha ngoma kama Chacun poir soi, Nostalgie (papa yoyo) na Bimasha ngoma ambazo zilikuwa zinamvuruga mzee mzima Franco akiwa kwa stage. Alikuwa karibu sana na Lutumba Simaro ambaye ndie alimleta TP OK JAZZ. Adios vieux Josky.
 
Back
Top Bottom