Sanamu ya Franco Luambo Makiadi yazinduliwa jijini Kinshasa

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
5,721
10,220
SANAMU YA LWAMBO YAZINDULIWA JIJINI KINSHASA

1698114053259.jpg

Miaka 26 baada ya kifo chake mwanamuzi nguli wa Kongo Franco Luambo Makiadi, sanamu yake imezinduliwa usiku wa kuamkia leo jijini Kinshasa kwa heshima ya gwiji huyo wa muziki.

Franco, ambaye anachukuliwa kuwa mwanamuziki bora zaidi Afrika kuwahi kutokea, aliaga dunia mwaka 1989 akiwa na umri wa miaka 51 akiwa kafanya kazi ya muziki iliyotukuka kwa zaidi ya miaka 30.

Sanamu hiyo, iliyozinduliwa na Waziri Mkuu wa Kongo Augustin Matata Ponyo, ni ya shaba na ina urefu wa mita 2.97 na uzito wa kilo 400. Imesimama katikati mwa wilaya ya Matongee katika wilaya ya Kalamu huko Kinshasa. Wilaya ya Matongee inajulikana kama mapigo ya moyo wa muziki wa Kongo.

Baadhi ya wanamuziki mashuhuri wa Kongo waliohudhuria hafla hiyo walipongeza kazi hiyo, na wanataka magwiji wengine wa muziki wa Kongo waheshimiwe kwa njia hiyo hiyo.

“Tunamshukuru Mkuu wa Nchi kwa ishara hii kubwa kwa ajili yetu. Tunatumai kuwa tukio la aina hii litaenea pia kwa wasanii wengine kama Kalle Jeff ambaye alikuwa mmoja wa wanamuziki wa Fiesta, "alisema rais wa Chama cha wanamuziki wa Kongo Kiamwangana Mateta Verkys ambaye wakati fulani katika miaka ya 1970 alikuwa mwanachama maarufu wa Franco. bendi ya TPOK Jazz.

Wakati wa hafla hiyo, Kundi la Ok Jazz ambalo Luambo alilianzisha na kuliongoza kwa muda mrefu, lilicheza lilitymbuiza.

Bendi hiyo imefufuliwa upya hivi karibuni na mtoto wa Franco na inacheza katika klabu ya usiku ya Une Deux Trois ambayo Franco alicheza wakati wa enzi zake.
 
Safi sana kwa kuniletea taarifa muhimu kama hii, welldone mkuu, ila nimepotea hapo kwenye jina la Rais wa chama cha wanamziki Kongo, Verkys...angali hai legend huyu?,BASATA kwangu ni wapumbavu,,wapo kufungia musicians wanaopingana na wapangaji wa lumumba na magogoni
 
BASATA ni chama cha wapumbavu, wanataka tuimbe nyimbo za ngono ma ulevi tu. Nyimbo za kuibua fikra mpya hazitakiwi nchi hii
 
Nimekumbuka nyimbo zake.
Mamou
Mario kwelii ni mwamba bado anaishi na ataendelea kuishi.
 
Back
Top Bottom