Uchaguzi 2020 Frank Mwakajoka arejesha fomu ya kuomba uteuzi wa kugombea Ubunge jimbo la Tunduma

10 Julai 2020
Dodoma, Tanzania

Nyufa ndani ya CCM SONGWE, Makundi yaibuka

Tayari wana CCM ya Zamani wakiwakilishwa na MNEC toka Momba Songwe amefikisha ujumbe juu ya kutoridhika na CCM Mpya kuwasahau waliokipigania chama 2010 - 2015



Hayo yalibainika wakati wa mkutano mkuu wa CCM uliofanyika mjini Dodoma. Mwenyekiti wa CCM Mpya Mh. John Pombe Joseph Magufuli amewataka wanaCCM kutobweteka.

Mwenyekiti huyo wa Taifa wa CCM amewataka wanaCCM wote kuonesha umahiri wao kisiasa na kiuongozi na kuacha kulalamika.

Mwenyekiti wa CCM akaongeza inawezekana wahamiaji wa kisiasa wapya wanaonesha viwango vya juu vya umahiri ktk kuwakilisha hoja na kutetea wananchi na ndiyo maana wanapata nyadhifa za kuteuliwa kwa haraka kuliko wale wafia-chama wa siku nyingi waliopo ndani ya CCM.

Maana wafia-chama wa CCM baadhi yao wanaishia kugonga meza kuunga mkono hoja bungeni na ktk vikao vya chama bila kutoa michango ya hoja zenye ushawishi, wala kubainisha majibu ya tatuzi za changamoto ziwe vipi ili kusaidia serikali ya CCM Mpya isilale.
 
Back
Top Bottom