Francis Ndulane anahitaji sana ushauri asijidhuru

Francis Ndulane anahitaji sana ushauri asijidhuru

Watu wa kusini ni balaa, wakammezesha ndizi mbivu mzee wa watu ikamniga sauti ikagoma kutoka - jamani.
 
asaidiwe tu
 

Attachments

  • kuapa.PNG
    kuapa.PNG
    21.6 KB · Views: 6
Watu wanacheka sana na kushangilia kwa kilichotokea kwa mbunge wa Kilwa aliyeshindwa kuapa mbele ya Rais.

Hili sio tukio la kawaida kwa mbunge aliyeteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Madini.

Kwa mujibu wa Rais ni msomi mzuri tu wa kiwango cha uzamili katika fani ya fedha.

Imekuwa ni jambo la kushtua sana kwa mtu mwenye uzoefu kama wake kushindwa kuapa kwa kusoma maandishi ya kiapo.

Kama ikivyo kwa Watanzania wengi tunashangilia sana hasa baada ya rais kutoa msimamo wake kuwa atateua mbunge mwingine kushika nafasi hiyo.

Ndulane atakuwa na mfadhaiko wa hali ya juu sana pamoja na mke wake na watoto wake pia kama anao.

Hapo ndipo washauri nasaha wanahitajika sana kwa Ndulane kuliko kumcheka na pengine aweza chukua hatua mbaya sana.

Ni wakati wa umma kuwa karibu yake na kumpa moyo kwa fedheha ile kwa Ndulane
Kila mmoja atajiangalia mwenyewe na wale waliomsaidia katika wizi wa uchaguzi mpaka akafikia hapo kwani wale waliowaiibia uchaguzi wana machungu makubwa kuliko yake yeye kwani si bado atabakia na huo ubunge wa dhulma na kama atachaganyikiwa sisi tuliodhulumiwa ndivyo tunavyoomba mungu atulipie tukiwa tunaona na hata bado mpaka hilo kubwa Lao laana za mungu zitamfikia tu kwa duwa za waliouwawa na kdhulumiwa.
 
Back
Top Bottom