Francis Ndulane anahitaji sana ushauri asijidhuru

Francis Ndulane anahitaji sana ushauri asijidhuru

MKEHA

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
716
Reaction score
1,144
Watu wanacheka sana na kushangilia kwa kilichotokea kwa mbunge wa Kilwa aliyeshindwa kuapa mbele ya Rais.

Hili sio tukio la kawaida kwa mbunge aliyeteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Madini.

Kwa mujibu wa Rais ni msomi mzuri tu wa kiwango cha uzamili katika fani ya fedha.

Imekuwa ni jambo la kushtua sana kwa mtu mwenye uzoefu kama wake kushindwa kuapa kwa kusoma maandishi ya kiapo.

Kama ikivyo kwa Watanzania wengi tunashangilia sana hasa baada ya rais kutoa msimamo wake kuwa atateua mbunge mwingine kushika nafasi hiyo.

Ndulane atakuwa na mfadhaiko wa hali ya juu sana pamoja na mke wake na watoto wake pia kama anao.

Hapo ndipo washauri nasaha wanahitajika sana kwa Ndulane kuliko kumcheka na pengine aweza chukua hatua mbaya sana.

Ni wakati wa umma kuwa karibu yake na kumpa moyo kwa fedheha ile kwa Ndulane
 
Kama kwa elimu yake hiyo anashindwa kujiamini basi kwenye seminar alikuwa hafanyi presentation mbele ya wenzake. Chuo tunajifunza vingi ikiwemo kuwa na confidence mbele ya watu wengi na wakubwa
 
Back
Top Bottom