Four cylinder Vs six cylinder

Four cylinder Vs six cylinder

Habari wakuu naomba kuweka kwenu huu mjadala mtu anayetumia cc 2000 lakini four cylinder na anayetumia cc 2000 lakini six cylinder.
Hapo tofauti ni nin
Kama engine zote ni sawa kitechnologia mwenye 6 cylinder atafaidi yafuatayo
Higher engine eficiency
Lower fuel consumption
Less vibration at low engine revolution
Smoothness springy like feeling during driving at higher speed.
Engine iwe 1500cc afu iwe single cylinder ...mafuta itakunywa kama rocket..lakini wakaongeza idadi ya cylinder zisaidiane...umoja ni nguvu.
 
Nahisi unataka kuelewa jambo fulani muhimu sana ila ambalo ni pana na linachanganya kwa kiasi fulani kwa sababu ufafanuzi wake unahusisha vitu vingi vya mfumo wa injini. mbaya zaidi nahisi swali lako hujaliweka vizuri kutosha kueleweka unachotaka kutofautishiwa.

hata hivyo mm ntajifanya ulikuwa unaulizia hivyo vitu kwenye gari.
4 cylinder ni tofauti na 6 cylinder kwa upande wa nguvu ya gari pia matumizi ya mafuta.

kwanza fahamu kuwa cylinder ni mtungi unaopokea mafuta na kuyachoma ili yaweze kutengeneza nguvu ya kusukuma gari. mtungi huu una kitu kiitwacho pistoni kilichozama ndani yake na kina uwezo wa kuingia ndani na kutoka mithili ya pampu ya baiskeli unapojaza upepo tairi. pistoni hupanda na kushuka ndani ya cylinder, wakati pistoni inapanda huruhusu mafuta kuingia ndani ya cyinder na wakati inashuka hukandamiza na kuunguza mafuta yaliyoingia ambayo hutengeneza nguvu ya kusukuma gari. zoezi hili hurudia rudia kwa haraka sana na ndipo gari hutembea.

kujibu swaki lako
Ukisikia 4cylinder maana yake kuna mitungi minne ya kuchoma mafuta kwa wakati mmoja.. na 6 cylinder maana yake mitungi sita ya kuchoma kwa wakati mmoja...

1. ikiwa kila cylinder ina ujazo sawa wa lita 0.5 kwenye injini ya cylinder 4 basi kwa mpigo mmoja kila cyinder ya injini itachoma mafuta hivyo cylinder 4 zitachoma o.5 * 4= 2litre (2000cc)
japo kuna vitu vingine lkn kiwango cha mafuta yanayochomwa kwa mpigo mmoja huchangia kuamua nguvu ya gari.

ikiwa hiyo gari ya 6cylinder pia kila cylinder ina ujazo wa lita 0.5 inamaana kwa mpigo mmoja mafuta yanayochomwa ni 0.5*6= 3Litre (3000cc).

kwa hesabu hizo maana yake gar ya 4cylinder itakula mafuta kidogo kuliko ya ile ya 6cylinder, pia ya 4cylinder itakuwa na nguvu kidogo kuliko ya 6cylinder

2. sasa ili gari zenye idadi tofauti ya cylinder zile kiwango sawa cha mafuta itakuwa namna hii
Ikiwa injini ya 4cylinder inkula cc 2000 maana yake kila cylinder inabugia 500cc yaani cylinder moja ina ujazo wa 500cc tu, na kwa kadri vyilinder inavyoweza kuchoma mafuta mengi kwa pamoja ndivyo gari inavyokuwa sio na nguvu tu bali pia kasi japo kuna vigezo vingine vya kuamua.

ikiwa injini ya 6cyilinder inakula cc 2000 pia maana yake kila cylinder inabugia 333.3cc yaani cylinder moja ina ujazo wa 333.3cc tu. hivyo kwenye mpigo mmoja kila cylinder inachoma mafuta kidogo kuliko inavyofanyika kwenye injini ya cylinder 4. hivyo gari hii itakuwa na nguvu ndogo kuliko hiyo ya cylinder 4 japo itakuwa na uwezo wa kukimbia zaidi kuliko hiyo ya cylinder 4.

Kumbuka: nahisi ni nadra sana kukuta gari yenye cylinder nyingi kuwa na cc sawa na gari yenye cylinder chache. Mara nyingi kama sio zote gari ya cylinder nyingi huwa ina cc kubwa pia.
Inawezekana hajakuelewa watu wa Lumumba vchwa vizto mno ila mada umeimaliza
 
Logic ni kuwa kama gari ina cyljnder 4 na cc 2000 ni sawa na gari ya cylinder 6 ya cc 2000 ambapo ulaji wa mafuta ya 6 itakuwa na nafuu kidogo.
Zote ulaji wa mafuta zinafanana,tofauti yake ni kwamba hiyo 6 cylinder itakuwa inaakimbia sana kuliko 4 cylinder
 
6 au 4 ni idadi ya piston zinazo compress mchanganyiko wa oxygen na mafuta kusababisha combustion inayotoa nishati ya kuzungusha shaft. 6 itahitaji milipuko 6 kukamilisha mzunguko mzima wa shaft wakati 4 itahitaji milipuko 4 tu. Hivyo kama zote zina cc zinazolingana basi ile ya 4 cylinder itakuwa na inachoma mafuta mengi kwa kila piston moja ukilinganisha na piston ya 6 cylinder.
Hiyo ina matokeo gani katika utumiaji wa mafuta wa GARI!
 
Six cylinder ina nguvu sana na inakimbia kukiko 4 cylinder! Na six cylinder inakunywa mafuta madogo kiasi ukilinganisha na 4 cylinder.
Nguvu ya gari inatoka kwenye mafuta!! Haiwezekani GARI litumie mafuta kidogo halafu liwe na nguvu sana kuliko linalotumia mafuta mengi!!!
Ukweli ni kuwa mtengenezaji wa GARI kama anataka GARI liwe na nguvu kubwa ni lazima liwe na cylinder nyingi na matumizi yake ya mafuta yatakuwa ni makubwa!!! Usitarajie hata siku moja V8 itumie mafuta kidogo kuliko V6, na V6 itumie mafuta kidogo kuliko V4. Hii ni kweli kama magari yote tunayoongelea yako vizuri!! Ukiona V4 inatumia mafuta zaidi ya V6, ujue hiyo V4 ni mbovu!!!
 
Nahisi unataka kuelewa jambo fulani muhimu sana ila ambalo ni pana na linachanganya kwa kiasi fulani kwa sababu ufafanuzi wake unahusisha vitu vingi vya mfumo wa injini. mbaya zaidi nahisi swali lako hujaliweka vizuri kutosha kueleweka unachotaka kutofautishiwa.

hata hivyo mm ntajifanya ulikuwa unaulizia hivyo vitu kwenye gari.
4 cylinder ni tofauti na 6 cylinder kwa upande wa nguvu ya gari pia matumizi ya mafuta.

kwanza fahamu kuwa cylinder ni mtungi unaopokea mafuta na kuyachoma ili yaweze kutengeneza nguvu ya kusukuma gari. mtungi huu una kitu kiitwacho pistoni kilichozama ndani yake na kina uwezo wa kuingia ndani na kutoka mithili ya pampu ya baiskeli unapojaza upepo tairi. pistoni hupanda na kushuka ndani ya cylinder, wakati pistoni inapanda huruhusu mafuta kuingia ndani ya cyinder na wakati inashuka hukandamiza na kuunguza mafuta yaliyoingia ambayo hutengeneza nguvu ya kusukuma gari. zoezi hili hurudia rudia kwa haraka sana na ndipo gari hutembea.

kujibu swaki lako
Ukisikia 4cylinder maana yake kuna mitungi minne ya kuchoma mafuta kwa wakati mmoja.. na 6 cylinder maana yake mitungi sita ya kuchoma kwa wakati mmoja...

1. ikiwa kila cylinder ina ujazo sawa wa lita 0.5 kwenye injini ya cylinder 4 basi kwa mpigo mmoja kila cyinder ya injini itachoma mafuta hivyo cylinder 4 zitachoma o.5 * 4= 2litre (2000cc)
japo kuna vitu vingine lkn kiwango cha mafuta yanayochomwa kwa mpigo mmoja huchangia kuamua nguvu ya gari.

ikiwa hiyo gari ya 6cylinder pia kila cylinder ina ujazo wa lita 0.5 inamaana kwa mpigo mmoja mafuta yanayochomwa ni 0.5*6= 3Litre (3000cc).

kwa hesabu hizo maana yake gar ya 4cylinder itakula mafuta kidogo kuliko ya ile ya 6cylinder, pia ya 4cylinder itakuwa na nguvu kidogo kuliko ya 6cylinder

2. sasa ili gari zenye idadi tofauti ya cylinder zile kiwango sawa cha mafuta itakuwa namna hii
Ikiwa injini ya 4cylinder inkula cc 2000 maana yake kila cylinder inabugia 500cc yaani cylinder moja ina ujazo wa 500cc tu, na kwa kadri vyilinder inavyoweza kuchoma mafuta mengi kwa pamoja ndivyo gari inavyokuwa sio na nguvu tu bali pia kasi japo kuna vigezo vingine vya kuamua.

ikiwa injini ya 6cyilinder inakula cc 2000 pia maana yake kila cylinder inabugia 333.3cc yaani cylinder moja ina ujazo wa 333.3cc tu. hivyo kwenye mpigo mmoja kila cylinder inachoma mafuta kidogo kuliko inavyofanyika kwenye injini ya cylinder 4. hivyo gari hii itakuwa na nguvu ndogo kuliko hiyo ya cylinder 4 japo itakuwa na uwezo wa kukimbia zaidi kuliko hiyo ya cylinder 4.

Kumbuka: nahisi ni nadra sana kukuta gari yenye cylinder nyingi kuwa na cc sawa na gari yenye cylinder chache. Mara nyingi kama sio zote gari ya cylinder nyingi huwa ina cc kubwa pia.
Siyo nadra, hilo halipo!!! Huwezi kukuta gari mbili zenye idadi tofauti ya cylinder lakini CC ni sawa!! Hivi vipimo viko standard!!
 
Nguvu ya gari inatoka kwenye mafuta!! Haiwezekani GARI litumie mafuta kidogo halafu liwe na nguvu sana kuliko linalotumia mafuta mengi!!!
Ukweli ni kuwa mtengenezaji wa GARI kama anataka GARI liwe na nguvu kubwa ni lazima liwe na cylinder nyingi na matumizi yake ya mafuta yatakuwa ni makubwa!!! Usitarajie hata siku moja V8 itumie mafuta kidogo kuliko V6, na V6 itumie mafuta kidogo kuliko V4. Hii ni kweli kama magari yote tunayoongelea yako vizuri!! Ukiona V4 inatumia mafuta zaidi ya V6, ujue hiyo V4 ni mbovu!!!

Kweli kabisa, na ndio maana huwa wanaandika , mfano 6.8 litres v8 engine
 
Una maelezo mazuri sana. Nikuulize swali nje kidogo ya mada. Nissan X-Trail (2002) ni 4 cylinders, 2000cc. Gari hii inatembea 6km/Ltr hapa Dar es Salaam. Unaweza kusemaje, ni ulaji wa mafuta wa kawaida kutokana na aina au muundo wa gari au kuna part inahitaji kubadilishwa. Gari ni used from Japan.
Nissan xtrail zina mapiston makubwa aidha sensor zimeharibika
 
Kweli kabisa, na ndio maana huwa wanaandika , mfano 6.8 litres v8 engine
Hio ngoma sio mchezo, sahivi v8 kubwa ya Toyota ni 3UR-FE iko kwenye vx v8 zile new model inagonga 5.7litres! Sema mwendo upo yani hasa ukipata la petrol unainjoy sana overtaking! Kisahani 260km/hr
 
6 cylinder inakua na horse power kubwa hivyo na mwendo wake unakua mkubwa.....hiyo inatokana na 6 cylinder inakua na valve 6 badala ya nne....
Ulimaanisha 6 cylinder inakuwa na valve 6 au Piston 6? Mara nyingi gari zinakuwa na valve 4/piston. Kwamba za input ni mbili na output ni mbili.
 
Haya mambo ya CC na clyinders hua ni changamoto.Niliwahi kununua Mazda rx 8 ya 2005 ina cc 1300 na 4 clyinders ila ulaji wa mafuta ilikua 1litre inaenda km 6.5 highway ila inakimbia sana kuliko altezza na hizi gari nyingine sa saizi yake.Tatizo cc ndogo lkn mafuta inakula v8 vile
Rotary engine hiyo mkuu. Hataro sana halafi pia ni engine za ajabu sana; hazina piston kama hizi traditional engine zetu! Shida ya hizo engine ni maintanance yake tu. Ikifa hiyo engine ni kununua mpya tu, hainaga overhaul
 
ni sawa, kumbuka namba nilizoziweka hapo juu sio halisia ila zimetumika kuelezea uhusiano wa cylinder na cc.

pia kuna upungufu wa maneno ya kiswahili ya kuelezea mambo haya tofauti na kingereza labda ni kwa sababu mm siyajui au hayapo kabisa. mfano power, energy, force, torque zote nazijua kama nguvu kwa kiswahili japo kwa kingeleza ni nguvu zenye ujumbe tofauti.

pia mm sio mtu mwenye taaluma ya magari na injini ila nina uelewa fulani fulani.. nimejitosa baada ya kuona uzi hajapata wa kuusemea vizuri.. hata hivyo ni mwanzo mzuri kwa wenye uelewa zaidi kuweka ufafanuzi mzuri zaidi
Umeelezea vizuri, umeeleweka
 
good pia six mara zote huwa haitoi muungurumo mkubwa km four na hii inachangiwa na kuwa na cyrinder nyingi zaidi ya gari zenye four. chukulia mfano pikipiki yenye piston moja au mashine ya disel yenye piston zilivyo na kelele
kama tunaangalia kelele ndege nayo itakuwa na piston ngapi s
 
kama tunaangalia kelele ndege nayo itakuwa na piston ngapi s
Mkuu comment yako, na profile picture vinaendana.
Huyo kuzungumzia gari wewe umeruka kwenye ndege, wakati wowote utarukia kwenye meli.
Jaribu kuangalia kwa kina hiki kitu. Resonance in relation to number of piston with a consideration of fuel consumption .
Kabla ya kukua kwa technology tulikuwa na kitu kinaitwa governor ambayo ilikuwa mechanical. Ilikuwa inatumia proposional principal, ie unapofungua mafuta na ndivyo yatakavyolika.
Baada ya kukua kwa technology tukapata, proposional +derivatives governor, ie hata ufungulie mafuta hadi mwisho, mafuta yatatumika kulingana na mzigo, na hata ukibania mafuta unajisubmbua kwani engine itakosa nguvu
Baadae technology ikazidi kupanuka, tukapata proposional +derivatives +intergral governor. Hii imefuata kanuni ifuatayo, ukubwa wa pua si wingi wa makamasi. Ie unaweza kuta engine ina v12, lkn ulaji wake ukawa sawa na 6cylinder. How? Ni rahisi.
Sio kwa kuwa umetengeneza choo basi kila wakati ukajisaidie, no. Utaenda chooni pale utakapobanwa.
V12 on normal loads sio piston zote 12 will be supplied with fuel, may be 6 of them.
How do they achieve comfotability? Minimization of resonance, na ndio maana zipo kimya.
Kanuni ya hapo juu in applying only ktk magari.

Mkumbuke consumption inavyo hesabiwa.
Consumption kwenye barabara = power of engine xload x conditions of load x time ÷ distance covered.
Ile consumption ilioandikwa kwenye gari ni bench tested results. Ni engine imewekwa juu ya bench ikawashwa.
Wakora
 
cc maana yake ni cubic capacity,ukubwa wa hizo cylinder ambako piston zinawekwa. cylinder chache ziwe na cubic capacity sawa na cylinder nyingi sijaelewa au naweza sema haiwezekani
kila mtu anatafsiri anavojua !! sio ulivoandika ni cubic centimeter
 
Back
Top Bottom