salosalo
JF-Expert Member
- Jun 7, 2012
- 596
- 278
Habari wakuu naomba kuweka kwenu huu mjadala mtu anayetumia cc 2000 lakini four cylinder na anayetumia cc 2000 lakini six cylinder.
Hapo tofauti ni nin
Nahisi unataka kuelewa jambo fulani muhimu sana ila ambalo ni pana na linachanganya kwa kiasi fulani kwa sababu ufafanuzi wake unahusisha vitu vingi vya mfumo wa injini. mbaya zaidi nahisi swali lako hujaliweka vizuri kutosha kueleweka unachotaka kutofautishiwa.
hata hivyo mm ntajifanya ulikuwa unaulizia hivyo vitu kwenye gari.
4 cylinder ni tofauti na 6 cylinder kwa upande wa nguvu ya gari pia matumizi ya mafuta.
kwanza fahamu kuwa cylinder ni mtungi unaopokea mafuta na kuyachoma ili yaweze kutengeneza nguvu ya kusukuma gari. mtungi huu una kitu kiitwacho pistoni kilichozama ndani yake na kina uwezo wa kuingia ndani na kutoka mithili ya pampu ya baiskeli unapojaza upepo tairi. pistoni hupanda na kushuka ndani ya cylinder, wakati pistoni inapanda huruhusu mafuta kuingia ndani ya cyinder na wakati inashuka hukandamiza na kuunguza mafuta yaliyoingia ambayo hutengeneza nguvu ya kusukuma gari. zoezi hili hurudia rudia kwa haraka sana na ndipo gari hutembea.
kujibu swaki lako
Ukisikia 4cylinder maana yake kuna mitungi minne ya kuchoma mafuta kwa wakati mmoja.. na 6 cylinder maana yake mitungi sita ya kuchoma kwa wakati mmoja...
1. ikiwa kila cylinder ina ujazo sawa wa lita 0.5 kwenye injini ya cylinder 4 basi kwa mpigo mmoja kila cyinder ya injini itachoma mafuta hivyo cylinder 4 zitachoma o.5 * 4= 2litre (2000cc)
japo kuna vitu vingine lkn kiwango cha mafuta yanayochomwa kwa mpigo mmoja huchangia kuamua nguvu ya gari.
ikiwa hiyo gari ya 6cylinder pia kila cylinder ina ujazo wa lita 0.5 inamaana kwa mpigo mmoja mafuta yanayochomwa ni 0.5*6= 3Litre (3000cc).
kwa hesabu hizo maana yake gar ya 4cylinder itakula mafuta kidogo kuliko ya ile ya 6cylinder, pia ya 4cylinder itakuwa na nguvu kidogo kuliko ya 6cylinder
2. sasa ili gari zenye idadi tofauti ya cylinder zile kiwango sawa cha mafuta itakuwa namna hii
Ikiwa injini ya 4cylinder inkula cc 2000 maana yake kila cylinder inabugia 500cc yaani cylinder moja ina ujazo wa 500cc tu, na kwa kadri vyilinder inavyoweza kuchoma mafuta mengi kwa pamoja ndivyo gari inavyokuwa sio na nguvu tu bali pia kasi japo kuna vigezo vingine vya kuamua.
ikiwa injini ya 6cyilinder inakula cc 2000 pia maana yake kila cylinder inabugia 333.3cc yaani cylinder moja ina ujazo wa 333.3cc tu. hivyo kwenye mpigo mmoja kila cylinder inachoma mafuta kidogo kuliko inavyofanyika kwenye injini ya cylinder 4. hivyo gari hii itakuwa na nguvu ndogo kuliko hiyo ya cylinder 4 japo itakuwa na uwezo wa kukimbia zaidi kuliko hiyo ya cylinder 4.
Kumbuka: nahisi ni nadra sana kukuta gari yenye cylinder nyingi kuwa na cc sawa na gari yenye cylinder chache. Mara nyingi kama sio zote gari ya cylinder nyingi huwa ina cc kubwa pia.