Former Cabinet Minister and Attorney General Charles Njonjo is dead

fimboyaasali

JF-Expert Member
Jan 14, 2011
8,382
7,909
njonjo.jpg

Former Cabinet Minister and Attorney General Charles Njonjo​

In a message of condolence, President Uhuru Kenyatta said Njonjo passed away peacefully at 5am on Sunday. He was aged 101.

"It is with a heavy heart that I have this morning, Sunday 2nd January 2022, received the sad and heartbreaking news of the passing away of Hon. Charles Mugane Njonjo," said Kenyatta.

Njonjo was the only surviving member of Kenya's independence Cabinet.

"The passing away of Hon. Njonjo is a big blow not only to his immediate family, friends and relatives but to all Kenyans and indeed, the entire African continent because of his leading role in the founding of the Kenyan nation at independence," added the Head of State.

President Kenyatta said Kenya owes a debt of gratitude to Njonjo and his generation of independence era leaders "for their selfless contribution to the laying of the solid foundation upon which our country continues to thrive."

Njonjo served as the country's first post-independence Attorney General between 1963 and 1979, and as Constitutional Affairs Minister between 1980 and 1983.

Source: Citizen Tv
 
Charles Njonjo aliyewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Kenya amefariki alfajiri ya leo 02.01.2022 saa 05:00Hrs aged 101. Aliacha wosia akifariki "asicheleweshwe" hivyo asubuhi majira ya 08:00hrs tayari amechomwa moto sawa sawa na wosia wake. Umeelewa?
 
Ni nani huyo mtu? Kwanini anakula jehanam angali duniani?
... aliwahi kuwa mwabnasheria mkuu (AG) wa Kenya enzi hizo ambapo alistaafu u-AG mwaka 1979. Mwaka 1980 alitwaa ubunge na Moi kumteua kuwa waziri wa sheria. Amefariki alfajiri ya leo majira ya 05:00Hrs na by saa 08:00Hrs alishachomwa moto sawa sawa na wosia wake.

At the age of 101 alikuwa ndiye mkenya pekee aliyekuwa hai katika wale wa baraza la mawaziri la kwanza la Kenya huru. Charles Njonjo ni jina kubwa sana Kenya kati ya wale waze waliokuwa na mali za kutosha na jeuri; in short kwa lugha ya vijana wa mtaani alikuwa "anatisha".
 
Alikuwa ni moja ya watu walipamnia Uhuru wa Kenya.. mwanasheria pia kafa akiwa na umri wa miaka 101 Leo saa 11:00 alfajiri.

Sent from my M2006C3MG using JamiiForums mobile app
Tunatoa pole kwa balozi wetu wa Kenya hapa Tz!

إِنَّا لِلَّٰهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ
 
Huyu ni mwanasheria nguli wa Kenya aliyekuwa amebaki hai katika baraza la kwanza la marehemu mzee Jomo kenyatta ni miongoni wa Waafrika waliokuwa hamwamini mwafrika mwenzake alioa mzungu akiwa na umri wa miaka 56 hakutaka kupanda ndege iliyokuwa inaendeshwa na Rubanj Mweusi hakuamini kabisa mtu mweusi anaweza alishangilia Sana Kuvunjika kwa iliyokuwa JUMUIYA YA AFRICA MASHARIKI alifungua CHAMPENI ndani ya bunge kwa furaha amefariki Leo alfajiri na mwili wake kuchomwa moto mchana huu wa tarehe 02/01/2022
 
Naona nothing zaid ya kumpondea marehemu. Which haisaidii lolote. Dead people dont talk
 
Huo umri ni mkubwa, Mungu alimtunza sana.

Anyways huwa nawaza sana kumbe .. maisha ni nini..
 
Ulivyo muelezea mzee wa watu ni kama mwanamke aliyepachikwa mimba na kuachwa, sasa anatoa povu kwa bwana wake.
Kula maembe mabichi mkuu umuelezee kwa undani siyo kama ulivyofanya hapa.
 
Huyu ni mwanasheria nguli wa Kenya aliyekuwa amebaki hai katika baraza la kwanza la marehemu mzee Jomo kenyatta ni miongoni wa Waafrika waliokuwa hamwamini mwafrika mwenzake alioa mzungu akiwa na umri wa miaka 56 hakutaka kupanda ndege iliyokuwa inaendeshwa na Rubanj Mweusi hakuamini kabisa mtu mweusi anaweza alishangilia Sana Kuvunjika kwa iliyokuwa JUMUIYA YA AFRICA MASHARIKI alifungua CHAMPENI ndani ya bunge kwa furaha amefariki Leo alfajiri na mwili wake kuchomwa moto mchana huu wa tarehe 02/01/2022
Aaaaaaa 😆😆😆huyu bwana alimpa hard time sana mzee Moi kipindi akiwa Rais, na alikuwa na dharau mingi sana na alikuwa ni mtu wa msimamo sana.

Na alikuwa na mategemeo kuwa akifa Jomo Kenyata basi yeye ndo angekuwa mrithi wake badala ya Moi kwasababu Njonjo alikuwa ni Mkikuyu msomi lakini lakini mzee Kenyata akawa karibu na kumuamini sana mzee Moi, siku zote watawala hupenda watu wasiokuwa na uwezo na profile ya kutisha kuwa manaibu wao.

Kwa msimamo wake Charles Njojo kuna kipindi aliwagomea wazungu kusoma kitu ambacho a
 
....aliwagomea wazungu kusomea kitu ambacho alikuwa hakitaki matokeo yake akafukuzwa chuo na sponsorship yake ikawa withdrawn na yeye akasema potelea mbali akatafuta wafadhili wengine waliomsomesha Law.

Huyu Njojo ndie aliefanikisha operation Entebe kule Uganda wakati wa-israel walipoenda kuwakomboa Ndugu zao waliokuwa wameshikiliwa kwenye uwanja wa ndege wa Entebe. Yeye ndie aliemshauli Rais kuwa Kenya iwe stop centre ya ndege za Israel wakati wa hiyo Operation Entebe, na kuwa Njojo awe centre of communication Kati ya Israel na Kenya secretly na kupelekea hiyo Operation kufanikiwa.
 
Anyways huwa nawaza sana kumbe .. maisha ni nini..
"Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu. Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya" - Mhubiri 12:13-14

Maisha ni kama Mfalme mmoja ambaye aliamua kuwapa watu watu sehemu ya milki yao ili wawe na mamlaka kiasi fulani ya kujiamulia. Baada ya kuwapa mamlaka hayo akawa anawatembelea kila mara ili kufurahia kwa pamoja maana aliwapenda sana. Yule Mfalme alikuwa na moja ya watumwa wake ambaye alimchukia sana. Akijua hana cha kumfanya kwa sababu ya mamlaka yake, akanuia kuwaharibu watu wa milki yake ambao Mfalme aliwapenda na kuwajali sana.

Siku moja, mtumwa mwovu alimtembelea mke wa gavana wa lile jimbo liliopewa mamlaka lijiendeshe chini ya milki ya Mfalme. Akamshawishi kwa habari ya kumwasi Mfalme ili wao wawe wafalme. "Kuwa gavana haitoshi, kama unaweza kuwa mfalme". Kuna shida gani ukitangaza uhuru wako? Mke wa gavana aliyachukua yale maneno akamshawishi gavana kuwa watakuwa huru zaidi wakiwa nje ya Ufalme na kuwa ufalme huru. Gavana alikubaliana na mkewe wakatangaza mapinduzi na kujitangaza wafalme. Wakaungana na mtumishi mwovu kuupinga Ufalme. Pamoja na kuwapenda sana watu wa jimbo lile, kwa sababu ya uadilifu wake Mfalme akatangaza siku ya kwenda kulikomboa jimbo na adhabu ya kifo kwa waasi wote.

Mfalme akatangaza sheria mpya kuwa kwa muda aliompangia kila raia wa jimbo lile, atapaswa kurudishwa katika makao makuu ya Ufalme apate kuhukumiwa kulingana na matendo ya uasi wake. Gereza likaandaliwa lenye kila aina ya mateso, kwa ajili ya mtumishi mwovu na watu wa jimbo lile. Ikawa kila siku watu zaidi ya mia moja wa jimbo lile waliitwa kurudi kwa Mfalme, na kuhukumia kifo katika gereza lile. Walitamani sana na walijaribu sana wasiitike. Walitengeneza kila aina ya dawa, kuziba masikio yao wasisikie sauti ya Mfalme, maana akikuita hakuna namna utaacha kuitika. Lakini haya hayakufua dafu, watu walimiminika kila siku na walihukumiwa kila siku.

Mfalme alikuwa ametoa amri. Ya kuwa yeyote ambaye ataamua kuweka silaha chini, kuukana uasi wa jimbo lile na kupokea msamaha huo, ujapofika muda wake wa kuitwa, hataadhibiwa. Mfalme alikwishalipa adhabu kwa wote walio tayari kuweka chini silaha na kuukana uasi wao. Wengi wa watu wa jimbo hili walijisikia fahari kwamba wako huru. Hawakutaka kabisa kuingiliwa katika uasi wao. Walimchukia Mfalme na wengine waliamua mioyoni mwao kuwa hayupo. Wengine walimtukana na wengine waliendelea katika uais wao bila kelele.

Watu walioamua kupokea msamaha wa Mfalme walionekana vichaa, wasio na akili na wasaliti. Walichukiwa na baadhi ya maeneo ya jimbo lile waliuawa. Kuna wananchi wengine waliwaona ni wasaliti na wakapigwa marufuku kuishi au hata kuonekana maeneo yale. Wengine hawakujali, ilimradi wao wanaendelea katika uasi wao. Lakini kila siku mamia waliitwa na mamia walihukumiwa.

Siku hata siku, nyakati za Mfalme kurudi jimbo lile kulikomboa ulikaribia. Mtumishi mwovu alijua hilo naye akachochea uasi uwe mbaya siku hata siku. Hata hivyo wengi walikubali kuweka silaha chini na kuupokea msamaha. Wengi zaidi na zaidi waliukataa, wakaudhihaki na kutema mate.......

Summary ya maisha ni nini, ni hii hapo. Mwenye kusoma na afahamu Mamndenyi
 
Huyu ni mwanasheria nguli wa Kenya aliyekuwa amebaki hai katika baraza la kwanza la marehemu mzee Jomo kenyatta ni miongoni wa Waafrika waliokuwa hamwamini mwafrika mwenzake alioa mzungu akiwa na umri wa miaka 56 hakutaka kupanda ndege iliyokuwa inaendeshwa na Rubanj Mweusi hakuamini kabisa mtu mweusi anaweza alishangilia Sana Kuvunjika kwa iliyokuwa JUMUIYA YA AFRICA MASHARIKI alifungua CHAMPENI ndani ya bunge kwa furaha amefariki Leo alfajiri na mwili wake kuchomwa moto mchana huu wa tarehe 02/01/2022
Kwa kukosa imani na weusi, nguo zake zilikuwa zinakuwa dry-cleaned London, kama mzee wa vijisenti.
 
Back
Top Bottom