Form 4 na wengine, angalieni hapa!

Form 4 na wengine, angalieni hapa!

Haya matokeo ndiyo hayo yametoka!! Kila kitu hadharani, sasa ukiwa hapa JF ndo mpango nzima!! Manake watu washaanza kuhoji, mi nina hiki au kile nitafanyaje, haya ngoja nitajaribu kuweka mwongozo na alternatively nyingine due to spme perfomances kwa wote, manake naona huku kitaa watu wanadanganyana sana!!

Hii ni kwa kadri ninavyofahamu mimi, kama kuna marekebisho basi yafuatie:

=> Credit Qualification kwa hali ya kawaaida ni 'C'-Na ili uende Form 5 unahitaji uwe na C 3, hapa ni either umebalance Combination(Comb) au hujabalance. Sasa kama una C 3 na comb hujabalance, hautachaguliwa serikalini bali shule binafsi utaenda kusoma mchepuo utakaofanana na masomo yako.
[ Mfano: Civ-C, Kisw-C, Geo-C...unaweza fanya HGK ama HGL ama kozi nyingine hata kama english na History una D].

=>Ukiwa na C 2 na D kadhaa(lets say 4 ya 26), hapa utaweza kwenda Form 5 shule za Private lakini utatakiwa utafute C ya 3 kw kureset wakati upo form 5. Same na C 1 You need to re-sit.

=> Hapa sasa ndipo kwenye utata. Ukiwa na D 3, kiukweli sahau Form 5 kama hauhitaji kurisit, sasa qualification hizi zina option zifuatazo:
1. Unahitaji kupiga long pass kwa kwenda Chuo kwa ngazi ya Certificates. Duraation ya hii kozi ni 1 year Certificate. Sasa hapa kuna vyuo kadhaa vinavyotoa certificates. Hapa ni D za masomo yoyote yale Basic(sina uhakika kama B/Knwoledge na Islam zinazingatiwa na ndio maana nasema D za Basic Subjects)
Mfano: Unaweza kufanya Certicates vyuo vya CBE-Mambo ya Biashara, IFM, TIA, Utumishi wa Umma(Public Service) Vyuo vya Kilimo na Ualimunk.
Nakozi nyingi tu wanatoa kwa certificates..mfano Procurement, Accounts, Public Admistration, Recording, Clearing and Forwarding, Social Development, Secretarial Duties, Education nk.

=> Ukiwa na D 4 upo qualified kufanya ngazi ya certificate kama nilivyoanisha hapo juu.

=> Ukiwa na D 5 sasa hapa wewe umeula!! Hapa unaruhusiwa kabisa kufanya Basic Diploma katika vyuo vyote wanavyotoa Duploma. Kwa mfano vyuo hivyo nilivyovitaja hapa JUU, chukua form yako kwa maringo achana na biashara ya kurisit omba kozi ya diploma, Teana kama una D ya hesabu na English ndo inakuwa rahisi zaidi kuchukuliwa.

=> Kwa wale waliosoma mahesabu kuna vyuo vingine kama DIT(Daar Institute), AIT(Arusha Inst) na Mbeya Tech Msishau kufanya maombi, na kwale waliopiga fresh Biology with minimum of D angalieni option za Nursing ni nzuri sana na katika vyuo vya MATC na COTC.

Kama kuna marekebisho yanakaribishwa na kama hoja ama daubt basi uwanja ndio huu. Most welcome!!

UPDATE:

2i9m911.jpg

jidhjp.gif
Wakuu kuna mdogo wangu ana four ya 27 amemaliza mwaka 2021. Je anaweza kwwnda course za afya? Yani certificate ya either nursing, clinical officer au Dental?
 
Mimi binti yangu kapata div one ya 14 combination ya science naomba ushauri Kuna wanaonishauri aombe vyuo ili apige diploma ya clinical alafu baadaye akipata ajira apply degree ya medicine au engineering hivyo hivyo na kunawengine wananiambia nimuache aende five na six ila kunakutoil Sana kwenye science hivyo anaweza anguka akawa amewest time ni bora vyuo hebu nishaurini which is the best option
 
Chuo ni chaguo bora zaidi
 
Mpeleke akasome Radiology au Dental...C.O now majanga Ila Kama ana ndoto za kua MD na wewe mzazi una uwezo mpeleke shule nzuri akapige one kali 3-6 aende moja kwa moja MD kupitia form 6 Ila C.O kwa sasa ni risk kubwa kutokana na uchache wa nafasi kwenda MD na kukamiwa anaweza jikuta anatumia zaidi ya miaka 3 kuipata.
 
Akisoma hizo kozi hata juta na kazi kupata fasta kwa sababu wanahitajika Sana na ni wachache.
 
Ndugu zangu naomba msaada wenu,mimi nilifanya mtihani wa form four(QT) mwaka 2009 na kupata division four ya point 27.Je ni kozi gani nzuri ya biahara naweza kusoma kwa ngazi ya certificate na baadae diploma,nisaidien ndugu zangu.
B/MATH C
GEOGRAPHY C
HISTORY D
KISWAHILI D
ENGLISH D
CIVICS D
BIOLOGY F

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Fafanua mkuu,,ni kwamba una biashara unataka ujindeleze kielimu au hauna biashara Ila unataka kuanza kusoma kozi ya biashara ili uajiriwe au ifanye baishara.

NB samahani kwa maswali yangu nimeuliza hivyo kwa sababu ya umri wako pia maana 2009 sio mchezo
 
Mimi binti yangu kapata div one ya 14 combination ya science naomba ushauri Kuna wanaonishauri aombe vyuo ili apige diploma ya clinical alafu baadaye akipata ajira apply degree ya medicine au engineering hivyo hivyo na kunawengine wananiambia nimuache aende five na six ila kunakutoil Sana kwenye science hivyo anaweza anguka akawa amewest time ni bora vyuo hebu nishaurini which is the best option
Agonge chuo tu.
 
Fafanua mkuu,,ni kwamba una biashara unataka ujindeleze kielimu au hauna biashara Ila unataka kuanza kusoma kozi ya biashara ili uajiriwe au ifanye baishara.

NB samahani kwa maswali yangu nimeuliza hivyo kwa sababu ya umri wako pia maana 2009 sio mchezo
Nina biashara nataka kujiendeleza kielimu

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
COTC- Hii ni Clinical Officers Training College ambapo watu wa form naao wanajiunga na huwa mara nyingi ukimaliza diploma yako(3yrs kama sio 4yrs) unakuwa na direct employment frm government au sehemu nyingine.(Tumbi hospital, Mtwara hospital nk)
Miaka inaenda kasi sana, yaan enzi hizo unamaliza zako COTC Kibaha mtwara, kilosa, Lindi, mvumi, sengerema au lugalo ..unasubiri jina kuona umepangiwa wapi. Ila zilovyoanza tu sijui city college of health, sijui KAM na ujinga mwingine kama huo..ikawa kozi ya kipuuzi sana.
 
Back
Top Bottom