Forever Living!

Mi nilijiunga nao tatizpouuhabawa product ukanipotezea wateja, nilikaa karibu mwezi mzima kiongozi wangu anadai no product makao makuu.Hela yangu iliniuma sana maana nilikusa najipiga ganji ili nilipie/ nijiunge. Ila product zao ni nzuri.
 
Maelezo marefu, sayansi yake fupi, tupe data wanaofanya biashara hiyo ni wangapi, na waliofanikiwa kiasi hicho ni wangapi na wangapi wamefeli???? Tupe graph  hapa

hebu jiulize na wewe ulioanza nao darasa la kwanza wangapi walifika chuo na wangapi waliishia njiani? c ajabu ukakuta ni 10 kati ya 60 kwa hyo ni kawaida kwnye system yoyote ya ushindani
 
Tanzania inanufaika na
30% income tax from profit earned. na
10% repatriated income
thank you.
 
DECI ililiza wengi.na mpaka leo watawala wamepora mbegu za watu.
 
huu ni utapeli mpya wa kalamu. usipoteze mda, wala kujisumbua. niulize mimi kilichonitokea baada na kukomaa nao miaka miwili, najuta, yani bora hata ela yako ukaweka kwenye kilimo cha greenhouse. Hii biashara tayari inatawaliwa na watu 5, walioko top kama unafikiri kujiunga unapoteza mda wako, mimi nisingependa yawakute yaliyonikuta mimi. na unyama niliofanyiwa na hao viongozi ma top sponsor, wana roho mbaya. na hawawezi kuruusu mtu yoyote aingie kwenye chain yao. Kama unabisha katupe laki 8, hii biashara kwa watanzania wa kawaida haiwafai. mimi nimeachana na huu ujinga na sasa nafanya kilimobiashara au agribussiness. na sasa tuko hatua ya kuanzisha kikundi cha wanakilimo. kusajili kisheria, na kuwa na miradi ya kilimo ambayo inagurantee. tuwe na wataalamu. Kama mtu yuko interested ni pm. kuna kikundi kimoja kimeafanikiwa sana tuu na sasa wamepata wahisani mpaka nje ya nchi wao wanalima ufuta. fanya biashara yoyote na Mungu atakubariki sio huu upatu huu.
 
Mimi nilihudhuria semina yao na sikuweza kuwaelewa hata kidogo. Mapicha picha tuu
 
Kama umeamua kufunga basi funguka full... Wataje kwa majina hao "ma top sponsor" wenye roho mbaya na uelezee kiundani walikufanya nini exactly ili kila mmoja aelewe unyama unaouzungumzia hasa.
Utakuwa umeokoa watu wengi sana kuliko kutoa maelezo ya kiujumla jumla hivi.
Ni ushauri tuu Mjasiriamali1 Big Sam
 
Last edited by a moderator:

Yaani we ni hovyo kabisa!! Mburulaaaaaaaa

Hivi unajua maana ya pyramid wewe? Eti network marketing....nyambaf.....haya wenzako wanapiga hela we umeingiza sh ngap?
 
Nilipofikia level ya kufikia manager, top sponsor kizazi changu cha sita tokea juu, akamfuata downline wangu akamshauri akope ela yule dada akakopa hela mil 20 akanunua product ikasababisha mimi kuwa unrecognised manager, na yule dada sababu ya lile deni biashara kaacha,system inataka uqualify kwa kuwa na back ya watu chini yako, watu ambao nilikuwa nawaingiza mimi alikuwa anatafuta namba zao anakaa nao chini anaanza walazimisha wafanye 4cc wakawa wanakopa ela wananunua product na hawajui pa kupeleka, matokeo yake mtu anaishi na madeni sababu ya kulazimishwa kufanya 4cc ambayo ni karibia mil 1.2 , haishii hapo tuu anakufanyia majungu na na kukudharaulisha kwa hao downline na hii biashara haisogei bila downline hakuishia hapo akaendelea mbele kwa kututenga kwenye iyo ofisi yao, au anawakatisha tamaa downline wako akiona wewe huendani na mipangilio yake. Na alikuwa anafanya hivyo makusudi kusudi a qualify chairman bonus, wakiingia watu wapya anachukua namba zao anawaforce wafanye 4cc sababu ya ugeni wa mtu kwenye biashara mtu anakopa kwa iyo wewe ukiiingiza team yeye anauwa timu yako, mbaya zaidi anawapa maneno ya kinafiki na ya kuwakatisha moyo tofauti na sheria za hii biashara, watu wengi wameshalizwa na uyo top sponsor na wameacha biashara, wanatengeneza fake testmonies kwa kuwanunulia watu umanager kwa ajili ya kudanganya watu. Hii biashara naijua zaidi ya kuijua watu wameshapoteza nyumba zao,magari, sababu ya kudanganywa, kwa mimi niliuliwa timu yangu sababu mtu alitaka chairman bonus kwa kuwadanganya downline wangu wafanye kitu ambacho kiliwaacha na madeni. Watu wanamjua na ofisi zake mitaa ya bamaga-sinza. Nikaenda kumuambia sponsor wake kuona nafichua uovu wao, sasa wakaamua kudeal na mimi kwa kuniulia timu yoyote nayoianzisha kwa kuwafundisha uongo na majungu. Vita vilipozidi nikaamua kuacha iyo biashara ya utapeli iliyoshikiliwa na mtandao wa watu 5 tuu. Fanya kampuni yoyote sio forever!
 
nimeshatumia nguvu nyingi Sana kwenye huu Uzi. Hii biashara ni DECI. Ni utapeli. Haina uzalishaji na hivyo haina tija kwa uchumi Wa taifa
 
Dah! Pole sana
 
 
Mbona mimi nilinunua dawa ya meno kwa 15,000/= na kwingine wakawa wanauza 18,000/= huu sio utapeli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…