Mimi kama mwanamke wa kitanzania, na ninayejiita good feminist naona changamoto mbili tu kuhusu dada zangu na kaka zangu wanaozungumzwa hapa
baadhi ya wanawake,tumepata elimu na nafasi na uhuru wa kufanya mambo fulani ambayo mama zetu hawakuyafanya wala wale waliotutangulia....zaidi tukalelewa tukakua tukijua kuwa kuna mfumo dume na kwamba wanaume wamekuwa sehemu ya kutudumaza,kutuonea,kutudharau na kutufanya tuwe nyuma.
(Hili ni complicated kidogo nikitumia mila,misingi ya dini na majukumu ambayo wanawake tumelelewa na kuandaliwa kufanya kwenye familia).
Tumeamua basi sasa basi nasisi tutapigana kama wao,tufanye yale tunayoweza kufanya na wanaume hawakuwa kikwazo....priority hapa ikiwa ni Hela na mafanikio yanayotafsiriwa kwa yale ambayo hela inaweza kutoa.
Kitu nilichojifunza kwangu binafsi kwa wanawake ninaowatazama kwasababu ya mafanikio na heshima waliyojijengea ni kuwa mafanikio,furaha na heshima haviletwi tu na hela....katika vitu vigumu lakini wanawake tunapaswa kujifunza ni ku-balance maisha yetu ya kikazi,kifamilia na kindoa.Binafsi nimejifunza sana kwa Sheryl Sandberg COO wa Facebook na mama yangu ambaye ni mtumishi.
Mafanikio ni nini? kuwa na hela na kulala na wanaume tofauti tofauti,kuwa safarini na kuacha familia yako muda mrefu mikononi mwa watu wengine ukitafuta hela?kumuacha partner wako wa maisha nyumbani amudu majukumu ambayo kimsingi yaliandaliwa kuwa yako),kuwa na kauli za rahisi na nyepesi kama za mafanikio yangu kwanza mengine baadaye wakati ulishaamua kuwa na ndoa?
yabidi kujipanga sana na kuangalia mitazamo gani ya kubeba na ipi siyo ya kubeba.
Kwa wanaume,ukweli ni kuwa maisha yamebadilika. hatutakuwa wanawake ambao mama zetu walikuwa.hata lifestyle tu za sasa hazituruhusu. Ni muhimu kushauriana na mke/mpenzi wako ni kwa namna gani mnaweza kuishi na mapambano ya maisha ambayo sote tunayo na mwisho wa siku kuwe na mafanikio si tu ya kifedha bali pia ya ndoa yenu,watoto wenu,jamii na hata uzee wenu.
Mabadiliko ni magumu sana.kuweni sehemu ya mabadiliko,badala ya vitisho na lawama,tushauriane kwa namna ya kuenenda. ukitishia kumuacha mwanamke ambaye akili yake inaangalia tu kwamba hela ndio kila kitu na pengine alikuoa kwa uwezo wako na sasa anaona uwezekano wa kuwa na zaidi au tayari ana uwezo zaidi ya alivyowahi kuwaza na sio kingine utaumia na wewe na familia pia.
sasa ushauri wangu kwako mi nadhani,usipigishane kelele na mwanamke. Kuwa clear tu,nini unaweza kubaliana nacho na nini huwezi. mpe uhuru wa kuchagua na muda wa kufanya hilo,baada ya hapo waite washauri wenu au hata wazee weka maamuzi yako kama mwanaume na uyasimamie ukiwa umejipanga na majibu hasi na chanya kutegemeana na kile ukitakacho. Forever Living kuna wanawake wanaifanya vizuri na kwa kulinda heshima na ndoa na familia zao,usiichukie.