Preta
JF-Expert Member
- Nov 28, 2009
- 24,323
- 18,793
Halafu kuna hii nyingine (natanguliza samahani kwa wakereketwa wa mambo ya gender),
Kama unaenda safari, mtu wa kwanza kukutana naye akiwa mwanamke (na hasa hasa vile vibibi) bas safari yote imeinga mikosi.
Kwa wale wenye wake wengi, walikuwa na mmoja ambaye analeta bahati nzuri (hana mkosi. Kwa hiyo endapo mtu anasafiri au anaenda kuwinda, basi siku ya kuamkia safari lazima akalale na yule mke mwenye bahati ili mambo yaende mswano. Wakina Shekh Yahaya wanaendeleza haya mambo kupitia nyota. Kwamba kuna wanaume wanasafiria nyota za wapenzi au waume zao. n.k.....
na pia kuna kamtindo nilishawahi kuona kondakta wa basi moja kabla ya kuondoka anarusha vimawe ndani ya basi nikauliza sababu ni nini nikaambiwa eti kuna wanawake wako kwenye siku zao wataleta mkosi barabarani.....kwa kweli huu ni uonevu