mungu wangu!!!! tangu nizaliwe sijawahi kusikia unyanyapaa wa namna hii dunianina pia kuna kamtindo nilishawahi kuona kondakta wa basi moja kabla ya kuondoka anarusha vimawe ndani ya basi nikauliza sababu ni nini nikaambiwa eti kuna wanawake wako kwenye siku zao wataleta mkosi barabarani.....kwa kweli huu ni uonevu
mkuu umejibu vema sana, ingawa umechakachua kidogo tafsiri lakini nakupongeza maana umehahalisha mila zote potofu tena kwa uzuri sanadah! mengine wengine wanaweza kujazia. hizo ndo busara za wazee wetu
Shikamooni wakubwa
Marahaba wadogo zangu
Kule kwetu Mkuu Rombo tulikuwa tuaamini hifi:
Ukiwashwa kiganja cha mkono wa kushoto basi kuna pesa natafuta wewe...ole wako uwashwe kiganja cha kulia...pesa sote uliyo naso napotesa
Kope ya Jicho la kushoto ikitingishika kuna wageni wanakuja, likitingishika la kulia jiandae na msiba...OMG!
Kiamka usubuhi baioloji megoma kusimama jua siku hiyo kuna kabinti mtadumisha nako mila chini ya mkahawa, ila ukiamka imesimama, labda umbake dadako hiyo siku!!
Niendelee au nisiendelee? Damn hangover!
Ha ha ha ha ha pazuri hapo
Naona uko kichama zaidi....ushalipia joho?
Naona uko kichama zaidi....ushalipia joho?
6. Ukitembea na ndugu yako wa damu watoto wanaozaliwa wanakuwa mazezeta
Duh......Asprin kumbe unazijua mila japo kuwa nyengine kaa za kutunga hivi!
Hapo katibu naona uko kikazi zaidi! Hiyo iko kwenye katiba yetu?Kwamba kama mwanamke amepata ujauzito kwa infii wake....basi akimrudi mme wake (wakati akiwa mjamzito bado) basi mtoto atakae zaliwa atakua fotokopi ya mzee...
Kwamba kama mwanamke amepata ujauzito kwa infii wake....basi akimrudi mme wake (wakati akiwa mjamzito bado) basi mtoto atakae zaliwa atakua fotokopi ya mzee...
zingine
- mama mjamzito au anayenyonyesha akimuangalia na kumshangaa mwenye ulemavu au kasoro (km kengeza, kiwete), mwanae anachukua hiyo hali (makwata)
- Ni marufuku kuosha vyombo vya chakula usiku baada ya watu kula, kwani wataumwa tumbo
- asubuhi mtu wa kwanza unayekutana naye kama ameweke mikono mfukoni ni mkosi (unamwambia 'fungua mkosi', anatoa mikono mfukoni)
- Mama aliye kwenye siku zake akiwepo wakati ng'ombe wanapandishwa, zoezi halifanikiwi (nilishashuhudia wamama wanafukuzwa katika eneo la tukio, then dume akaweza kulenga)
- kuna mmea unaitwa 'isale', ukitoa maua ni kiashiria cha njaa mwaka huo. dawa yake ni kukata hayo maua na kuyatupa barabarani
- mzazi akifariki (bila kuacha wosia wa mali zake) atakwenda nazo kwa maana kuwa watakaozirithi watafilisika. dawa ni kukata migomba (uchagani) na kuiotesha kichwa chini miguu juu
- mama yako akikupiga na mwiko hautaoa
mama yako akikubinulia ****** unaweza kufa
- jogoo akiwika mlangoni asubuhi mtatembelewa na mgeni/wageni siku hiyo
- hairuhusiwi kukaa ukiwa umeshikilia pombe. unampa mtu anakushikia, ukishakaa ndo unaichukua
- ni marufuku kumpa mtu pombe bila kuonja hapo
- mbweha akipita anabweka usiku, kuna mtu atakufa mtaa huo
- mtoto akizaliwa saa sita kamili usiku (au dakika chache kabla/baada ya hapo) anakuwa na akili sana
- Je, mnaijua ile ya watu kuwa na kijicho? Kuwa baadhi ya watu wakimtazama mtoto mchanga atalia sana (anaweza hata kufa ) pale wanapoondoka. Au akiangalia kitu kizuri sana (km ngombe mkubwa), huyo ngombe anakufa. Kuna mama alikuwa akienda kwa watu anasema kwa sauti tangu akiwa nje kuwa kama kuna mtoto karibu afichwe (alikuwa anajijua kuwa ana kijicho!)