For Teamo and Co: Baadhi ya imani potofu kuhusu uzazi na watoto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

For Teamo and Co: Baadhi ya imani potofu kuhusu uzazi na watoto

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Dark City, Oct 3, 2010.

 1. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #1
  Oct 3, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kuna mambo mengi yanayoaminika sana katika jamii zetu na huwapa watu mashaka. Nimejaribu kuweka hii list. Naamini wengine wataongezea.

  Kuhusu mambo ya uzazi:
  1. Wazazi wakifanya tendo la ndoa mtoto anapata madhara (maziwa yanachacha)
  2. Mapacha wakirukwa wanakufa (endapo mzazi mmoja atafanya ngono nje ya ndoa kabla au baada ya kuzaliwa)
  3. Wazazi wakifanya ngono nje ya ndoa wanambemenda mtoto
  4. Baba akimpiga mtoto kichwani na uume wake mtoto anakufa
  5. Mama akimlaani mtoto wake kwa kumwonyesha sehemu nyeti anakuwa kichaa
  6. Ukitembea na ndugu yako wa damu watoto wanaozaliwa wanakuwa mazezeta
  7. Ukifanya tendo la ndoa na mama mja mzito (karibia na kujifungua) mtoto anazaliwa na uchafu kichwani.
  8. Bundi akilia karibu na nyumba basi lazimi kuna mtu atakufa kwenye familia hiyo
  9. Mwanamume akitembea na mtu na mwanaye anakuwa na uwezo wa ajabu. Mfano, akitemea mate siafu wanatawanyika na kupoteza dira
  10. Ukipanda nevu ya mwanamke (kwa wale wenye ndevu) utafanikiwa kwenye biashara na kuwa tajiri mkubwa sana.
  11. Kuna mbegu za mimea fulani na mkia wa ndege fulani ukigusisha kwenye mkojo wa mwanamke basi atakutafuta kwa udi na uvumba (ni dawa ya mapezi)
  12. Ndoa, siku ya harusi lazima mwanamume ahakikishe anamkanyaga kidole cha mguu mwanamke, akimuacha mwanamke akamkanyaga yeye, mwanamke atamuendesha kwenye ndoa yao
  13. marufuku kutwanga usiku kwa sababu wachawi watakuja na pia aliamini kwamba
  14. mtu haruhusiwi kufagia usiku kwa kuwa ataita wachawi na haruhusiwi kununua au kuomba chumvi usiku. akihitaji aseme anaomba 'dawa
  15. Ukimwimbia mtu chupi au nywele za sehemu za siri (kwa wanawake) basi unaweza kumfunga uzazi.
  16. Ukinyoa nywele lazima uzizike ardhini vinegenvyo wachawi wakiziokota watakuua.
  17. Ukimchungulia baba au mama yako akiwa uchi unapofuka
  18. Kama unaenda safari, mtu wa kwanza kukutana naye akiwa mwanamke (na hasa hasa vile vibibi) bas safari yote imeinga mikosi.
  19. Kwa wale wenye wake wengi, walikuwa na mmoja ambaye analeta bahati nzuri (hana mkosi. Kwa hiyo endapo mtu anasafiri au anaenda kuwinda, basi siku ya kuamkia safari lazima akalale na yule mke mwenye bahati ili mambo yaende mswano. Wakina Shekh Yahaya wanaendeleza haya mambo kupitia nyota. Kwamba kuna wanaume wanasafiria nyota za wapenzi au waume zao. n.k.....
  20. kuna ile nyingine inasema ukipiga mluzi usiku nyoka wanakuja...hii sijui ilikuwa ina maana gani
  21. Mwanamke akiwa kwenye siku zake asitengeneze mkate wa mayai .....................hauta 'umuka'. yaani utakuwa bumunda! Pia hakuruhusiwa kutengeza baadhi ya pombe za kienyeji.
  22. 22. mwana mwari haruhusiwi kujitia manukato akanukia au atakumbwa na jini (atavutia wengi na mwisho anaweza kukosa mume). Hapa nadhani walimaanisha jini mahaba.
  23. N.k


  Kuhusu mambo ya watoto
  1. Kuna baadhi ya watu hawatakiwi kumwona mtoto mchanga kabla ya kitovu kudondoka kwa hofu kuwa anaweza kufa au kudhurika. Kwa hiyo inabidi mtoto afichwe
  2. Kitovu kikidondokea dudu ya mtoto (uume kwa mtoto wa kiume) anakuwa ******* (hawezi kuzaa)
  3. Kitovu kikidondoka lazima kitunzwe vinginevyo mtoto anaweza kufanyiwa mambo ya uchawi endapo walozi watakiokota
  4. Kitovu anafungwa mtoto kiunoni ili asipate mchango (basically ni utapiamlo)
  5. Kuna dawa lazima mototo afungwe kiunonni au kwenye mkono ili asipate mchango.
  6. Mtoto asipopelekwa kwa babu zake atakuwa anapata ndoto za ajabu na kustuka stuka usiku. Lazima wazee wamwone, wamwekee mikono na baadhi ya makabila wampatie na jina.
  7. mtoto akizaliwa lakini akiwa analia sana labda nyumba haijamkaribisha........mzee wake apige hodi kila kona ya nyumba!
  8. Mtoto lazima apewe jina la utoto (la ukoo) na la ukubwani (may be la dini)
  9. N.K


  Nitaendelea kuongeza na nyingine nikizikumbuka. Pia wengine wanaweza kuongezea kutoka kwenye makabila yao.

  Kweli kuna umuhimu wa kuweka hivi vitu kwenye kumbukumbu. Vijana kama mdogo wangu Teamo watayahitaji haya mambo muda si mrefu.
   
 2. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #2
  Oct 3, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  this is mind boggling!

  sijui hata nianze wapi! karibia ya zote ndo kwanza nazisikia leo!
   
 3. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #3
  Oct 3, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Haaa,

  kwani wewe umetokea wapi nchi hii,

  Tena kuna nyingine zinazidi kunijia. Nitazidi kuziweka hapo.
   
 4. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #4
  Oct 3, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  mtoto akizaliwa lakini akiwa analia sana labda nyumba haijamkaribisha........mzee wake apige hodi kila kona ya nyumba!
   
 5. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #5
  Oct 3, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  ndoa

  siku ya harusi lazima mwanamme ahakikishe anamkanyaga kidole cha mguu mwanamke akimuacha mwanamke akamkanyaga yeye, mwanamke atamuendesha kwenye ndoa yao
   
 6. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #6
  Oct 3, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  katika zote umenimaliza na namba 4! watanzania tuna visa vya ajabu!
   
 7. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #7
  Oct 3, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hiyo ipo sana. Wanadai inatumika kuua watoto ili mama aweze kuzaa endapo mtu kaoa mwanamke mwenye mtoto anayenyonya. Ni kama inavyotokea kwa simba.
   
 8. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #8
  Oct 3, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  mtoto akipigwa kitu utosini lazima afe ati .....na hiyo ni murder case wasisingizie mila! aggggrrr
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  Oct 3, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  nne ipi? ya kwanza au ya pili?

  Ukweli ni kwamba tuna mila nyingi za ajabu na sijui historia yake ni wapi... kuna jirani yetu yeye alikua kapiga marufuku kutwanga usiku kwsababu wachawi watakuja na pia aliamini kwamba mtoto lazima apewejina la utoto na la ukubwani
   
 10. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #10
  Oct 3, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Sure, kutwanga usiku, kunoa kisu, kukata kucha na hata kufua chuma ilikuwa hairuhisiwa. Ilikuwa ni mbinu za kuepusha ajali
   
 11. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #11
  Oct 3, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  ya nne ya kwanza mkuu Acid.

  balaa .......

  Home economics

  mtu haruhusiwi kufagia usiku kwa kuwa ataita wachawi na haruhusiwi kununua au kuomba chumvi usiku. akihitaji aseme anaomba 'dawa' ........LOLOL
   
 12. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #12
  Oct 3, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  Sio wewe tu! Hata mm.....sasa mpaka umpige mwanao na uume unatafuta nn? Hahahaa..bsh*t
   
 13. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #13
  Oct 3, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  mkuu kwenye red nimefurahi sana, wisdom ilitumika
   
 14. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #14
  Oct 3, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Hebu tafuta logic ya hiyo hapo.

  Ngoja niendelee kuvuta hizi mlizoongeza.
   
 15. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #15
  Oct 3, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  most probably ni kuwa ukifagia usiku na vile hakuna mwangaza enzi hizo unaweza kusomba na vitu vyako muhimu ukavitupa!

  lakini lazima watudanganye kwa wachawi na majini? cant they just say it as it is?
   
 16. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #16
  Oct 3, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  nimeipata, kwakweli mpaka mtu umpige mwanao ya nanihii kweli inakuaje, si kichaa hicho??

  hayo ya home economics nimeyakubali, na DC kanipa kitu kizuri hapo kwenye shughuli za jioni kuepusha accidents
   
 17. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #17
  Oct 3, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0

  this is not even Bull's Sh*t .......it's chicken's! ha ha ha
   
 18. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #18
  Oct 3, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  mtu haruhusiwi kuomba chumvi jioni

  my take:

  ni aibu kwa mwanamke mpaka jioni chakula kinatakiwa hujamaliza kupika kwa kuwa huna chumvi. Kuficha aibu unamwambia jirani unaomba dawa!
   
 19. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #19
  Oct 3, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hapana Teacher,

  Lazima uongee na watu kwa lugha watakayoielewa. Ndo maana enzi hizo kumtajia mtu jambo lolote linahusu uchawi ilikuwa inatosha kumjenga hofu. Hata akina Shekhe Yahaya wanatumia hiyo philosophy bila kujua kuwa mambo yamebadilika.

  Katika maisha ya kawaida lazima itumike lugha inayoleta maana halisi (the language which makes senses). Kama ni viboko, vitisho etc.
   
 20. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #20
  Oct 3, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Nitaongeza ni hazi hapa,

  Ukimwimbia mtu chupi au nywele za sehemu za siri (kwa wanawake) basi unaweza kumfunga uzazi.

  Ukinyoa nywele lazima uzizike ardhini vinegenvyo wachawi wakiziokota watakuua. Kwa hiyo hawa jamaa wa saluni za kunyoa nywele wangeshatumaliza.
   
Loading...