Fomu kwa wale wambao wanataka ukarani kwenye sensa ikiwemo waliomaliza chuo lakini hawana ajira

NGOGO CHINAVACH

JF-Expert Member
Apr 8, 2011
943
368
1
TANGAZO LA KAZI YA MUDA KATIKA MRADI WA SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA 2012
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inakamilisha maandalizi ya kufanya Sensa ya Watu na Makazi ambayo itafanyika tarehe 26 Agosti, 2012. Ili kufanikisha Sensa hii, Serikali inatangaza nafasi za kazi za muda za MAKARANI NA MAKARANI WAANDAMIZI WA SENSA kwa Watanzania wenye nia na sifa zinazostahili kama ilivyoainishwa katika tangazo hili. Kazi hii itaanza tarehe 06 Agosti, 2012 na kumalizika tarehe 14 Septemba 2012.
1. KARANI WA SENSA
Kazi za Kufanya
Mwombaji wa nafasi hii, endapo atachaguliwa atapangwa katika eneo analofanyia kazi au eneo analoishi na atakuwa na kazi zifuatazo:-
a) Kuhudhuria mafunzo ya kuhesabu watu;
b) Kuhesabu watu kwa kutumia dodoso fupi katika Eneo la Kuhesabia Watu na kuhakikisha kuwa kila mtu anahesabiwa na anahesabiwa mara moja tu;
c) Kutunza vifaa vyote na nyaraka za Sensa katika hali ya usafi na usalama; na
d) Kufanya kazi nyingine zinazohusiana na Sensa atakazopangiwa na Kiongozi wake.
Sifa za Mwombaji
Mwombaji wa nafasi hii anatakiwa awe na sifa zifuatazo:-
a) Awe na umri usiozidi miaka 60 na mwenye afya njema;
b) Awe amehitimu angalau kidato cha nne;
c) Awe ni Mkaguzi au Mratibu wa Elimu, Mwalimu katika Chuo cha Ualimu, Shule ya Sekondari au Shule ya Msingi (Shule za Serikali au Binafsi) katika eneo husika, AU
d) Awe ni mfanyakazi yeyote wa umma anayeishi au kufanya kazi katika eneo husika, AU
e) Kijana aliyehitimu masomo yake na hajapata ajira, na
f) Asiwe na kesi yoyote ya jinai.
2. KARANI MWANDAMIZI WA SENSA
Kazi za Kufanya
Mwombaji wa nafasi hii, endapo atachaguliwa atapangwa katika eneo analofanyia kazi au eneo analoishi na atakuwa na kazi zifuatazo:-
2
a) Kuhudhuria mafunzo ya kuhesabu watu,
b) Kuhesabu watu kwa kutumia dodoso refu katika Eneo la Kuhesabia Watu na kuhakikisha kuwa kila mtu anahesabiwa na anahesabiwa mara moja tu,
c) Kutunza vifaa vyote na nyaraka za Sensa katika hali ya usafi na usalama, na
d) Kufanya kazi nyingine zinazohusiana na Sensa atakazopangiwa na Kiongozi wake.
Sifa za Mwombaji
Mwombaji wa nafasi hii anatakiwa awe na sifa zifuatazo:-
a) Awe na umri usiozidi miaka 60 na mwenye afya njema,
b) Awe amehitimu angalau kidato cha sita,
c) Awe ni Mkaguzi au Mratibu wa Elimu, Mwalimu katika Chuo cha Ualimu, Shule ya Sekondari au Shule ya Msingi (Shule za Serikali au Binafsi) katika eneo husika, AU
d) Awe ni mfanyakazi yeyote wa umma anayeishi au kufanya kazi katika eneo husika, AU
e) Kijana aliyehitimu masomo yake na hajapata ajira, na
f) Asiwe na kesi yoyote ya jinai.
3. Namna ya Kutuma Maombi
Mtanzania mwenye sifa zilizotajwa hapo juu atume maombi yake kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Sensa ya Wilaya/Halmashauri kwa anuani iliyowekwa hapa chini, akiambatisha nakala za vyeti na nyaraka muhimu ili kuonyesha sifa alizonazo.
Maombi hayo yatumwe kwa kujaza Fomu Maalum ya maombi ya kazi ambayo inapatikana katika Ofisi ya Mratibu wa Sensa wa Wilaya/Halmashauri, na endapo fomu haikupatikana, mwombaji atume maombi kwa kuandika barua akionyesha anuani kamili ya mahali anapofanyia kazi na namba ya simu kama anayo.
Maombi yapitishwe kwa wakuu wa kazi kwa walioajiriwa au Watendaji wa Mtaa/Kijiji kwa wale wasiokuwa na ajira, ili maombi hayo yafike wilayani kabla ya tarehe 25 Julai, 2012.
Mwenyekiti wa Kamati ya Sensa ya Wilaya
Wilaya ya ………………………..
S.L.P……………………………….……

N.B
USIPATE SHIDA KUHUSU FOMU UNACHOTAKIWA KUFANYA NI KUDOWNLOAD(KUPAKUA) HIZI NILIZOZIATTACH, DEADLINE NI TAREHE 25/07/2012

KILA LA KHERI
 
Attachments

  • KAZI YA SENSA HIYO.zip
    283.3 KB · Views: 2,103
asante mkuu,toka Feb form six tuko nyumbani,ngoja tujaribu bahati yetu.
 
dah,asavali wengne tumemaliza vyuo,ajira hakuna hata pakushkiza,
 
mkuu,unaenda kwenye ofisi za kitongoji chako unapoish hapo dar!sasa sisi hatujui wewe uko dar pande gani ili tuweze kukupa ramani.

jaman nimeenda hawana taarifa, nakaa mbezi beach, makonde area, sasa mtoa mada amezungumzia wilaya, kesho naelekea mjin kama ni pale magomen au kule ilala nipitie.
 
jaman nimeenda hawana taarifa, nakaa mbezi beach, makonde area, sasa mtoa mada amezungumzia wilaya, kesho naelekea mjin kama ni pale magomen au kule ilala nipitie.
nenda wilayani au halmashauri, wenyekiti weng wa serikali za mtaa hawajui
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom