DodomaTZ
Senior Member
- May 20, 2022
- 161
- 200
Wazee huku Tunduma ni changamoto kuvuka aisee siku saba foleni haitembei, huu msongamano wa malori katika mpaka wa Tanzania na Zambia upande wa Tunduma ni kero kubwa sana na hali hii inakwamisha Uchumi wa watu wengi na unawafaidisha wachache.
Kuna kiongozi wa masuala ya Usalama (jina ninalihifadhi kwa sasa) amenunua parking anavusha gari zilizolala kwenye parking yake nyie wanyuma hamna kupita mpaka muingie parking yake.
Kibaya zaidi parking yake gharama ya kulipia ni Sh 10,000 kwa siku wakati sehemu ningine zote parking ni Shilingi 5,000, Wazee mbona inakuwa hivi nchi ya wote mbona mifereji ya pesa ni ya wachache?
Hii Dunia ina mwisho hata wakijilimbikizia pesa kama milima hawataondoka nazo, yote kwa yote wanatupa ugumu wa Maisha tu.
Watumishi wamekosa uhadilifu Viongozi wetu wakuu wa nchi wanafanya kazi kubwa lakini Watumishi wasiokuwa waadilifu wanamuangusha mama.
Pia soma:
~ Wadau wadai msongamano wa malori Tunduma unatengenezwa, RC Chongolo aunda kamati kubaini ukweli
~ Foleni ya Tunduma mpakani haitatuliwi, kuna Watu wana maslahi Binafsi, inatutesa wengi