Foleni Mbezi-Kibaha mizani inaashiria nini?

Kabwela

Member
Feb 11, 2008
76
5
Juzi mchani nikiwa natoka kibaha kwenda mjini Dar nilikwama njiani eneo la kibamba CCM kwa muda wa saa 3. Jana jioni nikiwa natoka kibaha kwenda kiluvya madukani imenichukua saa 2 (mita 800) kwa gari kutokana na msongamano wa magari. Inaanza kuzoeleka kuwa kukitokea tatizo lolote maeneo hayo inakuwa na usumbufu kwa kila anayetumia barabara ya morogoro. Nauliza haya maandamano (foleni) ndio mazoezi ya kuadhimisha miaka 50 ya uhuru au ndio maisha bora yenyewe. Ukiuliza hivi kina.... Watasema mmetumwa na.... wengine watasema mnamsakama JK. Nashauri wanaohusika na barabara hii kuu ya nchi watengeneze njia za kuchepuka (service roads) kukitokea matatizo na hii inatuaibisha pia kwa majirani zetu wanaotumia bandari zetu. Nawasilisha
 
Mawazo Mazuri ila ni nani anayesikiliza? Hii sio aibu tu ila ni pamoja na kuchoka Kufikiri? Mimi sioni sababu yoyote ya Kuboresha Barabara Mbali Huku mwanzo Kukiwa Ni kero Tupu!! Fikiria Mtu Unatoka Magomeni Unafika Kibaha Baada ya Masaha matatu Hadi Manne!! Jumani Huwa siku zote najiuliza kuna Lolote la Kujifaraji na kusherehekea miaka Hamsini ya Uhuru Huku Kero zikiwa Zimeongezeka mara Kumi zaidi? Hadi aibu!! Hata hao Watembeza Bakuli hata wajitahidi Kupunguza Haya Matatizo!! Waende Wakapige Magoti Huko!! Nataka tu Wajue Hii Kero imezidi Kiwango Cha Kuvumilika!! Magufuli Ndugu Yetu Tukomboe!!
 
Hiyo barabara jana nliiona ya ajabu kabisa toka saa11 nimefika home sita kasoro!
 
Msijali naskia kuna mtu anaitwa simba mzee ndo suluhisho la kila kitu....kuweni na subra tu
 
Mkuu, mimi jana nilitoka kibaha kwenye mahafali ya waifu, nakimbilia pilau, we acha tu nilifika nyumbani sa 5 uck. Leo niko naelekea moro kuna ajali hapa imetokea karbu na mlandizi ni foleni tu. Utafikiri nina mapepo ya foleni
 
hiyo barabara jana nliiona ya ajabu kabisa toka saa11 nimefika home sita kasoro!

jana ilinikera sana
nlitoka kilimanjaro tlipofika kibaha tuliambiwa eti kuna ajali mbele ikabidi tule boda tutokee barbar ya bagamoyo na huko tunakuta foleni inayotia kinyaa,leo wadogo zangu wamefka mlandizi wakaambiwa tena eti kuna ajali mbele! Wamekaa masaa ya kutosha ,theres something fishy going on!
 
Tatizo ni Miundo mbinu mibovu.

Tatizo si miundombinu mibovu ila ni uzembe wa madereva hawataki kukaa foleni. Fikiria roli au basi kubwa linaovateki unategemea nini ikiwa mbele kunakuja roli au basi kubwa upande wa pili; kwa vyovyote watabaki wanatazamana tu. Kitu muhimu ni nidhamu barabarani kwani akitokea askari wa usalama barabarani vipi magari yanaanza kwenda hata kama ni polepole?
 
ile barabara ni kero kubwa sana kama mtu unafanya kazi Dar na unaishi Kibaha unaweza kulia kwa hasira na kujuta kwa nn umejenga Kibaha ni mwendo wa masaa matatu au zaidi kwa KM 30 au 40 tu
 
Subiri Wamalize Kuvuana Magamba, af Wapate Mgombea Urais Wa 2015, Then Watalishughulikia Tatizo Lenu...
 
Back
Top Bottom