IshaLubuva
JF-Expert Member
- Dec 4, 2008
- 250
- 11
Nionavyo mimi wakati fulani ni kama Menejimenti za Benki huwa zinapendelea wateja wao kulundikana kwenye foleni ndefu na kushinda ndani ya benki zao kama vile hawana kazi za kufanya. Utakuta benki ina counter 6 lakini kaunta 2 au 3 tu ndiyo zinafanya kazi. Halafu kwenye nguzo zao wamekuwekeeni matangazo ya kuzima simu eti kwa usalama wa wateja bila kuzingatia kuwa wateja walioko kwenye foleni ndefu wanawajibika kufanya mawasiliano ya kibiashara na wadau wao.
Lakini hata kwenye mashine za kutolea fedha nako hali ya foleni ni hivyo hivyo na wakati mwingine mashine hazifanyi kazi. Lakini cha kushangaza na kusikitisha zaidi ni pale benki, ikijua fika kuwa ina mkataba wa kuuza Luku, inashindwa kuhakikisha uwepo wa karatasi za kuchapishia miamala inayofanywa na wateja wake. Mteja ananunua luku fedha yake inakatwa halafu anaambiwa hakuna karatasi, ukiwauliza wanasema wasiliana na TANESCO.
Nazishauri Menejimenti za Benki zibadilike na pale inapolazimu kuongeza nyenzo za kufanyia kazi wafanye hivyo badala ya kuendelea kuwatesa wateja wao.