Wakuu wote JF, wasalaaam waleiykum!
- Katika siku za karibuni wananchi wa Tanzania tumejionea jinsi watawala wetu either wasivyo na maadili na uongozi tuliowapatia kama dhamana tu, wasivyo na adabu na sisi tuliowachagua, wasivyo na heshima kwa katiba na sheria za jamhuri yetu, wasivyo na utu, wengine walevi, waropokaji hovyo hovyo, incompetent, wasiowawajibikaji na ubaradhuli mwingi sana unaoonyesha kutotujali kabisa wananchi wa taifa hili.
- Ningependa sana kuwasikia wapinzani au kwa wale mlio karibu nao, kwamba wanafanya nini kuka-capitalize on yote haya ya uozo wa CCM? Na je tukiwapa uongozi hivi ni kweli watafanya tofauti na hawa waliopo kwenye uongozi wa sasa yaani CCM?
- I was just, thinking aloud!
Respect.
Field Marshall Es!
Mkuu it is very frustrating. Hopes zote kwa sasa ziko CHADEMA, hawa ndio wanaonekana at least wanaweza kuleta genuine opposition lakini so far bado hawaonekani kuwa na msukomo wa kutaka kuwa really opposition, na bado hawajaonekana kuwa wanataka kutuletea real alternative. Miezi hii michache iliyopita nao wameanza kuwa kama CCM, inaonekana hawana msemaji maalum, kila mmoja anakuwa kama msemaji wa Chama na anasema bila kupima athari ya anayosema, japokuwa hali hiyo wanaonekana kuifanyia kazi.
It is very obvious kuwa CCM wame mess big time, as a party hawastahili kurudi. Despite the efforts zinazofanywa na wapiganaji kusafisha chama, still the party is stinking and kimaadili hawatakiwa kurudi.
At this point nilitegemea kuwa CHADEMA watakuwa on offensive, lakini hali haioneshi hivyo ninachokiona ni kuwa wako in defence and they are defending themselves against something they do not have to. They have fallen right into mafisadis trap. Naona kuna watu ndani ya CHADEMA wamenunuliwa tena kwa bei rahisi (kwa ahadi za pipi kama ilivyokuwa kwa Chief Magungo) na wengine tunasikiatayari wamejivua wengine wanakaribia kujivua uanachama, a nonsense which was not supposed to be there at this vital moment for any serious particular party.
Monopoly ya CCM kwenye siasa za Tanzania, ni laana ambayo tumejitakia, tunafahamu kuwa Monopoly ni kitu kibaya lakini hakuna lolote tulilofanya kuhakikisha kuwa hakuna monopoly ya CCM for the good of Tanzania. Ndio maana unaona hata baadhi ya viongozi wanaonesha wazi kabisa kutokuwa na maadili ya uongozi, wanaropokaropoka kama watoto, au wamejiingiza kwenye siasa za mipasho, wengine hata bila aibu wanampitisha JK kuwa mgombea wa CCM 2010 as if hawajui kama kuna utaratibu maalum wa kufanya hivyo, na sio through media. It will be a blessing for Tanzania, kama CCM itapasuka kuwe na kundi la pumba na mchele na kama haitapasuka basi CHADEMA inatakiwa kujiput together na kupull up socks na ku absorb real wapiganaji na kuhakikisha kuwa come 2010 wanarudi Dodoma kuendeleza mapambano in a better way.
CUF Visiwani, big up. CUF Bara bado hakuna kitu. Lakini CHDEMA mnatakiwa kujua kuwa mnatakiwa kumkomboa mtanzania, kazi yenu kwa mwaka mmoja uliopita imeonekana nzuri, inatakiwa iendelee kwa nyie kuwa madarakani au kuwa stronger opposition, inawezekana.