Mkuu naona umetoa mpya hapa, unawezaje kusema FM ni digital version ya AM! Nijuavyo mimi tofauti ya AM na FM ziko kwenye mbinu zinazotumika kusafirisha/kusambaza mawimbi ya audio kwa kusaidiwa na Radio frequencies kama CARRIER. Sasa kinacho tokea ni nini: Sauti inachanganywa na hizo carrier frequency ambazo huwa ziko fixed, kwa hiyo inategemea mwenye transmitter anataka mawibi ya radio transmitter yasambazwe kwa mtindo gani AM au FM, kama ni AM basi mawimbi ya sauti yana bebwa na radio frequency kupitia amplitude modulation, sauti ikiwa kubwa amplitude za carrrier inaongezeka ikiwa ndogo inapungua, tatizo la mtindo huu ni kuwa na kelele sana na interference kutokana na magari, pikipiki, storm, umeme wa grid and what have you. Tukija kwenye mfumo wa FM hapo unakuta mawimbi ya sauti yanabebwa na carrier kwa mtindo wa ku-contract na expand carrier frequency (Frequency Modulation-FM), sauti ikiwa kubwa wawimbi ya RF yanakuwa compressed zaidi, sauti ikiwa ndogo yana-expand lakini amplitude zinabaki vile vile, uzuri wa mfumo huu ni kwamba sauti inasikika vizuri sana na hakuna interefence za aina yoyote kwa kuwa interference by nature zinatokana amplitude variation generated by equipment or galactic.
Mwenzangu humu alisema FM is a digital version ya AM! Mimi hilo sihafikiani naye na sijuhi kwa nini anasema hivyo labda kwa kuwa FM inakuwa na fixed amplitude basi mtu unaweza kughafilika ukafikili kwa kuwa analouge to digital conveters zinatoaga a fixed amplitude za bits basi na FM itakuwa hivyo, hiyo si kweli. FM na AM zote zinabaki analogue unless base band ya sauti ikibadilishwa i.e ikawa digitised kabla ya kuchanganywa na carrrier hili sauti hiwe transmitted in digital form by carrier frequencies, labda nirudie hapa kwamba carrier frequencies will always remain analogue you can't transmitt digital signal RAW you need analogue carrier frequency to realize that.