Mkuu,
Ngoja nikusaidie kitu muhimu sana katika maisha yako. Kama unataka kuwa Traffic Engineer basi tafadhali kasomee vyuo vikuu na pia uwe na kipaji. Nilisomea hili somo na hasa kwenye kudesign barabara za mwendo kasi.
Hizo barabara zote unazoziona hapo kwenye michoro, hazipo kwa bahati mbaya. Ni kutokana na idadi ya magari yaliyopo siku wana design na kuongeza factor kuwa baada ya miaka kwa mfano 10, idadi itaongezeka na kuwa magari XXX.
Ukishapata idadi ya magari yote yanayopita moja kwa moja, kukata kulia na kukata kushoto hapo ndipo maamuzi ya magari haya yapite wapi yanaanza.
Hili somo kuna watu wa kipaji na hata usome vipi, kama huna kipaji bado unaweza usiwe mzuri. Pamoja na kuwa na kipaji ila badi usomee ili kutumia utaalamu uliousomea na kuuweka kwenye michoro. Wakati mie nasoma, Mkali wa somo hili alikuwa jamaa asiye na Phd ila wenye PhD na hata Maprofesa walikuwa wanakuja kwake kuuliza kama walichokifanya kiko sawa au siyo. Kwa mfano sehemu za taa, aliweza kabisa kuona kwa haraka sana magari yatakavyokutana na hatari ya kuruhusu magari FFF kabla ya magari DDD. Kwa ufupi ni kuwa jamaa alikuwa na kipaji cha kuzaliwa kwenye Traffic Engineering.
Sasa basi tukirudi kwenye Interchange, kwanza huwa kuna Junction za kawaida. Magari yakizidi, kwa mjini unaweza Traffic light na nje ya mji unaweka hiyo round about. Kazi kubwa ya round about (hilo duara) ni kutuliza munkari wa madereva wanaoingia sehemu ya makutano ya barabara. Ni njia rahisi sana kutumia (gharama) ila inakula eneo kubwa. Ndiyo maana inafaa sehemuza pembeni au nje ya mji.
Ubungo ni kama katikati ya mji. Hilo duara litasababisha majengo mengi sana kubomolewa. Ni afadhali kutumia solution nyingine ambazo pia unaweza kuchanganya na taa za barabarani. Faida ya taa za barabarani ni kuwa magari yakishapata green, yanakwenda kasi na kuondoka wakati round about inawataka wapunguze mwendo.
Mfano mzuri wa hizi Interchange ni kama hii hapa. Kama unaona kwenye picha, inachukua eneo dogo sana pembeni ila kuna sehemu imewekwa taa za barabarani. Ogopa sana round about mjini na sehemu za heavy traffic. Ndiyo maana hata pale shule ya uhuru ile round about imeondolewa.
KWA MAONI YANGU NADHANI MCHORO HUU UNAFAA UKIJENGWA PALE UBUNGO MATAA , KUMEKUWA NA MICHORO MINGI ISIO ENDANA NA UFINYU WA NAFASI YA PALE UBUNGO NA NI YA GARAMA KUBWA LAKINI HUU KIDOGO UNABANA NAFASI NA NI RAHISI MTU UPANDE WOWOTE KUINGIA NA KUTOKA . NAFIKIRI WENGI WETU MNA JUA ADHA YA KUINGIA UBUNGO TERMINAL UKIWA UMETOKEA MJINI LAKINI KUNGEKUWA NA FLYOVER YA NAMNA HII TUSINGEPATA ADHA YA KUINGIA STAND KUU NA KUELEKEA MJINI,MWENGE NA BUGURUNI NA KIMARA.
ASANTENI.
ANGALIZO .
MSIINGIZE SIASA HILI NI WAZO BINAFSI.