Flora Mbasha kufunga ndoa wiki ijayo

Biblia inasisitiza sana kusameheana na inasema asiye samehe wengine bila kujali aina ya kosa, basi hata yeye Mungu hatamsamehe mtu huyo.

Kuhusu kisa cha hawa wawili, Flora ndiye aliye mwacha Emma, wakati ule Emma alimbembeleza sana Flora wasahau tofauti zao warudi waishi kwenye ndoa yao lakini Flora alikataaa kata kata hata kumtia aibu mumewe. Wakati huo Flora alikuwa anahatia mbele za Mungu kwa kuvunja ndoa na kukataa msamaha wa mumewe.
maana biblia inasema mtu akikosa hata saba
mara sabini kwa siku akija na kuomba msamaha, msamehe.

Baada ya kesi kwisha, Flora alimtaka mume wake amsamehe warudiane, kakini Emma alikataa katakata. Hivyo hatia ikageuka kwa Emma.

Kwa sababu hiyo Flora amehesabiwa haki kwa sababu aliomba msamaha kabla Emma hajaoa lakini Emma alikataa, kibiblia hata Mungu hajamsamehe Emma dhambi zake kwa kukataa kumsamehe Flora. hivyo Emma anahesabiwa kama mdhambi tu aliye amua kumwacha mkewe.

Hivyo Flora aliye tubu anapata uhalali wa kuolewa kwa neno linalosema:- yeye asiye amini akitaka kuondoka na aondoke, ndipo huyo ndugu mume au mke yu huru.

Kwa sasa Flora yuko huru
kuolewa kwa sababu Emma kamwacha kwa kukataa kumsamehe pale Flora alipoomba Emma amsamehe warudiane.

Emma atabaki na hatia.

Biblia inasema heri kuoa au kuolewa kuliko kuwaka tamaa. Flora bado kijana sana. Hana hatia kabisa mwacheni aolewe amtumikie Mungu vizuri.

HAPPY WEDDING FLORA.

Aisee.. Watu na profession zenu bwana!
 
Hebu someni maandiko vizuri najua alichokiunganisha Mungu mwanadamu asikitenganishe isipokua kifo au uzinzi so ukithibitisha mwezako anachepuka talaka tu ingawa Mungu haipendi kwakua hapendi kuachana.
Hilo la uzinzi nimelisikia kwao.
Ngoja niende kwa biblia kwanza ntarudi
 
Kwenye Biblia ya Kiingereza imendikwa hivi; " And I say to you, whoever divorces his wife, except for sexual immorality, and marries another, commits adultery; and whoever marries her who is divorced commits adultery "
 
Mwimbaji wa muziki wa Injili nchini, Madame Flora (Flora Mbasha zamani), Jumapili ya wiki ijayo anatarajia kufunga ndoa na mume wake mtarajiwa Daudi Kusekwa katika bustani za hoteli ya Rock Beach jijini Mwanza.

Madame Flora ameliambia Swaggaz kuwa ndoa hiyo itaambatana na uzinduzi wa albamu yake mpya inayoitwa Wakati Wake pamoja na kitabu alichokipachika jina la Siri za Flora Mbasha.

“Ndoa itafungwa asubuhi na jioni kutakuwa na sherehe ya harusi, utambulisho wa albamu yangu mpya pamoja na kitabu, watu wote wanakaribishwa kadi zimebaki chache tu kutokana na idadi ya ambayo imepangwa na kamati,” alisema Flora.

Chanzo. Mtanzania
Kama wewe Ni Mwanaume Jitahidi kutomuamini Mwanamke maana mwanamke Hachelewi kukusaliti ni Matumaini Yangu Flora alimwambiaga Mume wake Kwamba Kifo Ndio Kingewatenganisha lakini sasa Hicho hakikuwatenganisha...nA Leo anaolewa tena....Wanaume Jifunzeni kitu Hapo i know wanaume tuna tamaa hata ikitokea tukasaliti wapenz au wake zetu ni kwa tamaa za wakati huo tyu bali yale mapenzi ya dhati yanakuwa Bado yapo kwa wenzi wetu tofautu na mwanamke akichepuka ndo keshapenda mrengo wa kushoto na wewe huna chako tena hapo Na huwa nachekaga sana Pale nikikumbuka yule binti Nilimpendaga akaniambiaga Kwamba mimi na wewe hatutoachana Milele lakini leo hata salamu Hakuna......Anyway Nmamtakia Flora Bahati Njema!
 
e6fc6121bf4eba75eeaf87f954ce922c.jpg
 
Kweli machangudoa wapo kila sehemu, Kumbe hata waimba nyimbo za enjili nao ni wahuni kiasi hili? Hivi hao wanaokwenda kumsikiliza Frola wanaupako sawa sawa? Tangu lini NDOA iliyofungwa kanisani ikavunjwa na mahakama na bado ukenda olewa tena?
Mkuu hebu tupe sheria za ndoa zinasemaje
 
Kwenye Biblia ya Kiingereza imendikwa hivi; " And I say to you, whoever divorces his wife, except for sexual immorality, and marries another, commits adultery; and whoever marries her who is divorced commits adultery "
Tafsiri ya haraka, ikiwa mume atamtaliki mke kwa sababu nyingine yoyote, asioe tena kwa kuwa atakuwa anadhini. Mke aliye achika naye akiolewa, basi huyo aliyemuoa anadhini. Hapa haijamzungumzia mwanamke. Lakini, ikiwa amemtariki kwa sababu za uzinifu, mume anaweza kuoa tena.
 
Maswali ya kujiuliza kwa jambo hili: Je kila ndoa imefungwa na Mungu? Na Je! Ikiwa mwanadamu hawezi kutenganisha kilichofungwa na Mungu, yeye Mungu aweza kukitenganisha? Ikiwa Mungu anataka kutenganisha ni lazima amuue mmoja wa wanandoa?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom