Flight that took off in 2017 landed in 2016

Non-stop flight kutoka Shanghai kwenda San Francisco ni muda wa saa 11 na dakika 05,wakati Shanghai ipo mbele kwa saa 08 GMT sawa na saa 16 tofauti yake na San Francisco CA.
Hivi ilipitia upande wa pili au iliruka kupitia nchi za waarab??
 
Daaah, hiyo geography yapi mkuu yani ndege izidi speed ya dunia


hakuna ndege ya abiria inayozidi speed ya dunia inajizungusha kwenye mhimili wake

Na vile vile sidhani kama kuna chombo kimetengenezwa na binadamu ambacho kinazidi speed ya dunia kulizunguka jua ambayo ni zaidi ya kilometa 100,000 kwa saa
Sasa iliwezekana vp wao kuondoka 2017 na kufika 2016? Au ni uzushi?
 
Mungu ni mkubwa na muweza mjuzh wa kila kitu....(Allama l-iinsaana Maalam ya'alam) Amemfundisha/amemjuza mwanaadam yale aliyo kuwa hayafahamu.....Mungu ni mkubwa...
 
kiufupi nchi zilizo magharib huwa nyuma kimasaa kuliko zilizo mashariki,mambo ya latitude hayo, marekani (San Francisco ) ipo magharibi zaidi kadhalika China (Shanghai) ipo mashariki sana, hivyo basi ndege ikitoka China kuelekea Marekani itegemee kukuta muda mkubwa ambao ulishatumika pindi ipo china, kama ni tarehe 08 ulishaitumia China tegemea kuikuta America. jamaa alikuwa sahihi kabisa
Ni longitude...
 
Hata mimi nilitoka Manyovu Kigoma kwa kwa gari saa 6.01 usiku mwaka 2017 Nikafika Burundi mwaka 2016.

Ha ha ha, ungejitangaza mapema na wewe ungepata sifa mkuu, tena pale Munanila ni fasta tu uko Burundi, ngoja nisubiri mwaka kesho na mimi nifanye hiyo adventure.
 
Itakuwa ni pangaboi iyo
Suala sio pangaboi ila ni tofauti ya masaa kijiografia. Mfano Tanzani na Burundi tunapishana saa 1 wakati Tz ni saa 6 usiku Burundi inakuwa saa 5. Hivyo mtu anaweza kuukaribisha mwaka mpya akiwa Tz saa 6.01 usiku halafu akatoka kwenda Burundi na kufika kule saa 5.50 akakuta baado hawajaingia mwaka mpya akaupokea pamoja nao tena saa 6.00.01 wakati huo Tz itakuwa saa 7 usiku
 
Mi nilichoelewa ni kwamba, mzunguko wa dunia, una spidi ndogo kuliko ndege, ndiyo maaana ndege iliipita tarehe husika na kufika mahala ambapo siku haijabadilika, bado pana tarwhe ya jana, kwa kule ndege ilikotoka
Speed ya dunia ni 1670 km/ hr.. hata ndege ingelikuwa inakwenda 1000km/hr.... kitu kama hicho kingeweza kuwa achieved....

Kwa kifupi hata kama ungekuwa unatembea kwa miguu... the idea is simple ukipita mstari wa tarehe wa kimataifa basi utakuwa unaongeza siku au unapunguza siku.

Katika point ambayo wewe unasema ni morning basi upande mwengine wanasema evening. Vile vile kwenye duara sehemu ambayo unasema ni nyuzi 0 ukilizunguka nyuzi 360 zinakuwa ni sehemu hiyo uliyoanzia.

Mfano mshale wa dakika wa saa ukiwa kwenye 60.. ina maana ukiupeleka mbele (clockwise) ukitaka kufika kwenye 59... utausogeza kwa hatua 59 ila ukiupeleka kinyume (anticlockwise) utausogeza hatua moja kuifikia 59... kama 60 ndio sehemu inayotofautisha siku... basi kutola 1 hadi 59 ni rahisi kwa anticlockwise (hatua mbili) kuliko clockwise (hatua 58). Na ndicho kilichifanyika hapa. (Clock hapa ndio kama dunia yetu inavyozunguka)
 
Daaah, hiyo geography yapi mkuu yani ndege izidi speed ya dunia


hakuna ndege ya abiria inayozidi speed ya dunia inajizungusha kwenye mhimili wake

Na vile vile sidhani kama kuna chombo kimetengenezwa na binadamu ambacho kinazidi speed ya dunia kulizunguka jua ambayo ni zaidi ya kilometa 100,000 kwa saa
Mkuu soma thread #55... hope unaweza ukapa concept.
 
Sasa iliwezekana vp wao kuondoka 2017 na kufika 2016? Au ni uzushi?
Unafahamu kwa sasa hivi Tanzania ni saa kumi na dakika tano jioni (04:05PM) Na New York Marekani ni saa mbili na dakika tano asubuhi 08:05AM ......Think outside the box jombaa
 
Back
Top Bottom