Flash Back Memories: Matukio ya Boarding School

Duuuuuh mlikuwa mna raha kweli kweli
 
I see!!!Class of 2008??!!Kumbe humu tupo na watoto wetu bila kujijua.
Kibosho Girls 2008....A school of my "Step-girl"....Humu tunajadiliana na watoto zetu kabisaaaa...
Hujambo mwanangu lakini?

Hahaha sijambo shkamoo baba
 
Hahaha sijambo shkamoo baba
Marahabaa Mwanangu....loooh!!Kumbe mwanangu huwa unasoma "upupu" wa mimi mzee wako kule MMU??Loooh...,Hii mitandao hatari sana hii
 
na mm kifai modern sec. school class of 2012 nakumbuka nlkuwa naenda kuiba machungwa nyumbani kwa director wa shule! mwenzangu akaenda aiku hyo me sikwenda yeye akang'atwa na nyuki mdomoni!! mdomo ukavimba hatari
 
Hahahaha..hii inanikumbusha ezi za 90s GESECO kuna ticha alikua anaitwa Mahushi noma sana jamaa alikua akiona kisogo tu ameshakumaki kama mlikutana mjin ukamkimbia kesho parade yeye anapita nyuma nyuma kila mstari utasikia anakugusa begani afu anakunong'oneza nimekukamata..hahahaha, Jamaa alikua mnonko hatari,

Kulikua na system ya kutesa manyoya(form one) kunasehemu madogo walikua wanapelekwa humo ndani unakutana na Askari,Mwanasheria na Hakimu hahaha Askari anakukamata,Mwanasheria anakupa taratibu za shule afu Hakimu anakupa hukumu ulete uji kisado kizima kimeungwa na sukari, Crew yenyenguvu yakutisha ilikua inaitwa Nzige yani mtu hata akienda kushtaki Officine amafanyiwa nini ticha akijua huyo jamaa ni wa nzige kesi imeisha, au anakwambia kamuite aje mwenyewe maana yeye mwenyewe anaogopa.
Kuna siku Yule ticha Mnoko Mahushi watu walimvizia yupo officine kwake walika wamekamata nyuki wameweka kwenye mfuko mweusi wakamtupia dirishani afu milango ikafungwa hahaha.

Wanafunzi walikua wamepinda hiyo ilijulikana wilaya nzima kuna siku mkuu wa wilaya alitembelea shuleni akafanya mistake aliacha gari mbele ya shule na Askari akawaambia wabaki kwenye gari kengere ilipopigwa watu wakaenda parade uwanja upo nyuma ya shule wakati anahutubia akachafua hali ya hewa kwa kusema yeye anajiamin yupo vizur ndomaana hata hapo amekuja bila askari ile anamalizia kauli tu jiwe lakwanza likarushwa mara yakaanza kushuka kama mvua maaskari kushtukia mabomu ya machozi yakaanza.

Siku ya Mgomo au Vurugu pakiwa na mpira shule nyingine imekuja wakaanzisha vagi form 1-2 na kazi yao ni kukusanya mawe na kusogeza kwa form 3-4 ndo wanashambulia form 5 walikua wakianzisha wao wanatembeza mkono tu na kuchapa mikanda maana wengi wao walikua wanabeba Nondo
 
shule niliyosoma ilianza 2003 ni ya private mwaka 2004 form two walienda kufanyia necta shule ya jirani kwa kuwa ilikuwa haijasajiliwa mwaka 2005 serikali ikapiga marufuku kufanyia shule ya jirani

Ikatakiwa kusajiliwa shule iko mbali na kijiji siku wanakuja wakaguzi mmiliki akawachelewesha makusudi ili wafike usiku maana shule haikuwa na sifa ya kuwa boarding school
mhasibu wa shule anafika kijijini akawakuta wakaguzi akarudi mbio na baiskeli njiani baiskeli ikaharibika akatupa baiskeli pembeni ya njia akaanza kukimbia kwa miguu akatukuta tupo prepo ilikuwa saa mbili akasema nendeni porini mkajifiche wakaguzi wanakuja kusajili shule inatakiwa isajiliwe kama day school
Tukatoka mbio porini tukaacha daftari darasani mwalimu wa zamu akakusanya daftari zote akaweka ofisini tulikaa porini mpaka saa nane usiku, mhasibu wetu alikuwa na zaidi ya miaka hamsini
 
Daaah hii ya huyu mzee imenigusa, inaelekea alifanya kazi kwa moyo aisee
 




nimecheka hadi machozi yamenitoka!
 
 
Tulikuwa na HP mmoja mnoko mno, sasa siku moja tukavizia chumbani kwake mida ya class jamaa akanya kitandani kwake sisi wawili tukabaki nje kumuangalizia kama kuna noma. HP alilia vibaya sana siku ile (HP ni wakili mkubwa mjini sasa). Am sure nikimkumbusha hata leo atanikata mbata tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…