FL Studio 20.7 Vibey n Cool Beat Making

Rosenchold

Member
Jul 6, 2021
38
38
Nawapa hi! members wote wa Jf hasa wana "Entertainment", matumaini yangu muwazima wa afya kabisa kwa wale waliokumbwa na matatizo hapa karibuni hasa hasa moto wa eneo la Kariakoo na matatizo mengine nawaombea kwa m/Mungu awasimamishe tena.

Naomba niende kwenye hoja moja kwa moja, kwa hivi karibuni nimeanza kutumia software ya kutengeneza beats ya FL Studio, kabla ya kuanza nilianza kupitia pitia Tutorial YouTube ili kupata moja mbili na baadhi ya basics.

Nili dedicate muda kiasi chake lakini naona kama mambo hayaendi (my beats aren 't that good ), nilijitahidi kuanza na music theory baada ya kuona mambo ni mengi mno. Nilikuwa napenda sana kutengeneza beats za trap na RnB lakini kwa sasa ninazoweza kuzitengeneza ni za trap na trap soul peke yake.

Channel niliyokuwa natumia kujifunzia ni BusyWorksBeats kwakuwa ni mtu wa kwanza aliyekuwa anafundisha niliyekuwa namuelewa ingawa nilikuwa dummy/beginner 😂😂😂😂.

Nna Plugins zaidi ya 20 za FL Studio lakini najiona nashindwa kuendelea. Kama wewe ni mdau wa muziki nilikuwa naomba mchango wako ni jinsi gani naweza kuendelea nakuwa pro one day😋😋
 
Mi nlianza kutengeneza mabit bila music theory mpaka ikafika levo yakawa somehow good...ila now naona kama ningejifunza music theory mapema ningesave Muda mwingi.

Music theory haikupi creativity lakini inakusaidia ukiwa creative.
Inakusaida kuexpress idea yako Kuwa reality
 
Sina specific...ila Kwa trap/hiphop ipo ya Aiden kenway anafanya. Remakes
Hata busyworks wako vizuri.
Kuna group la WhatsApp la producers
 
kitu cha kwanza unacho takiwa ujue mziki sio plugin..unaweza kuwa na plugin hata buku na ukatoa madesa...Kama mimi kwenye upande wa mixing huwa natumia stock plugin na waves tu lakin madude nnayo yatoa ni balaa. cha msingi kula sana msuli kwenye mziki hakuna shortcut lazima ujue vitu vinafanyaje kazi...alafu kama unatumia sabufa kutengeneza mziki acha kabisa hahahahahah
 
kitu cha kwanza unacho takiwa ujue mziki sio plugin..unaweza kuwa na plugin hata buku na ukatoa madesa...Kama mimi kwenye upande wa mixing huwa natumia stock plugin na waves tu lakin madude nnayo yatoa ni balaa. cha msingi kula sana msuli kwenye mziki hakuna shortcut lazima ujue vitu vinafanyaje kazi...alafu kama unatumia sabufa kutengeneza mziki acha kabisa hahahahahaha
Atumie Nini Sasa headfone au?
 
Kitu cha kwanza unachotakiwa uhangaike sana kujifunza ni jinsi ya kutengeneza melody..Melody unaipata kwa kujua kutumia vizuri plugins ulizonazo na ujifunze kuzipanga kwenye piano roll hakikisha melody yako kwenye piano roll inakuwa na mzunguko angalau wa bars nne(ukifungua piano Roll utaona)...pia mziki unaotaka kuutengeneza unatokana na Key kwa mfano unapendelea kutengeneza beat inayofanana na Wiz khalifa something new na beats kama hizo iwe ndio identity yako basi beat ile imetengenezwa kwa D major..Hakikisha pia unazingatia Tempo(Bpm) unapotengeneza beat Trap nying huwa na tempo ya kuanzia 80 mpaka 90...pia kwenye plugins unaweza ukawa nazo mia lakini nyingine zikawa suck zinatengeneza ringtone tu nakushauri plugins za muhimu kuwa nazo ni Rf Nexus,Flex,Morphine na nyingine za nyongeza..Hiyo ni hatua ya kwanza kabisa kumbuka ukiweza hivi unatakiwa ujue kufanya mastering na mixing pia hili beat yako isound good
 
Citizen B unaweza uka recommend channel yako pendwa ya Tutorial kama hautojali?
[]internet money__ humu utakutana na Wana fl studio wengi tu...hayo madrill matrap hawa jamaa ni mbwa yan ukiwa unawafatilia hawa jamaa alafu huna omnisphere roho itakuuma sana...huku ndo utakutana na wakina nickmira

[]Ocean__huyu Ni mwana logic pro X Ni noma sana hasa akugongee zile flute beats utapenda

[]Chuk beats__huyu pia ni mwana fl ni mtamu sana

[]kichenza beats (hahahah siko siriaz)
 
Daah....huu ndo muda na mie nianze sasa kutengeneza beat za trap,rnb n.k niache hizi za kwaya kwanza, ila za kwaya kuzipiga ni very simpo kwenye kinanda lakini 😂
 
Mi nlianza kutengeneza mabit bila music theory mpaka ikafika levo yakawa somehow good...ila now naona kama ningejifunza music theory mapema ningesave Muda mwingi.

Music theory haikupi creativity lakini inakusaidia ukiwa creative.
Inakusaida kuexpress idea yako Kuwa reality
Elimu ya Music Theory inapatikana wapi?

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
kitu cha kwanza unacho takiwa ujue mziki sio plugin..unaweza kuwa na plugin hata buku na ukatoa madesa...Kama mimi kwenye upande wa mixing huwa natumia stock plugin na waves tu lakin madude nnayo yatoa ni balaa. cha msingi kula sana msuli kwenye mziki hakuna shortcut lazima ujue vitu vinafanyaje kazi...alafu kama unatumia sabufa kutengeneza mziki acha kabisa hahahahahaha
mzee speaker gani unazikubali kwa kuchuja mziki vizuri studio??? Msaada kwenye tuta plug ins ni nini?

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Kitu cha kwanza unachotakiwa uhangaike sana kujifunza ni jinsi ya kutengeneza melody..Melody unaipata kwa kujua kutumia vizuri plugins ulizonazo na ujifunze kuzipanga kwenye piano roll hakikisha melody yako kwenye piano roll inakuwa na mzunguko angalau wa bars nne(ukifungua piano Roll utaona)...pia mziki unaotaka kuutengeneza unatokana na Key kwa mfano unapendelea kutengeneza beat inayofanana na Wiz khalifa something new na beats kama hizo iwe ndio identity yako basi beat ile imetengenezwa kwa D major..Hakikisha pia unazingatia Tempo(Bpm) unapotengeneza beat Trap nying huwa na tempo ya kuanzia 80 mpaka 90...pia kwenye plugins unaweza ukawa nazo mia lakini nyingine zikawa suck zinatengeneza ringtone tu nakushauri plugins za muhimu kuwa nazo ni Rf Nexus,Flex,Morphine na nyingine za nyongeza..Hiyo ni hatua ya kwanza kabisa kumbuka ukiweza hivi unatakiwa ujue kufanya mastering na mixing pia hili beat yako isound good
mimi nataka kujifunza sampling beat kali kama za Duke zile

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
mzee speaker gani unazikubali kwa kuchuja mziki vizuri studio??? Msaada kwenye tuta plug ins ni nini?

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
kwangu Mimi Yamaha mwisho wa matatizo ..plugins ni software zinazo tumika katika kutengeneza mziki...Kuna aina mbili za plugin, plugin zinazotoa saut na zisizo toa saut, plugin zisizotoa saut huwa tuna tumia kwenye mixing mf..Equalizer, compressor na plugin zinazotoa sauti ni kama vinanda,gitaa nk... mfano mzuri labda unataka kupiga gitaa na hauna ilo gitaa live sasa unaingia internet unadownload software ya gita unaiingiza kwenye kompyuta unaanza kupiga sasa hiyo software ndo plugin..
 
Daah....huu ndo muda na mie nianze sasa kutengeneza beat za trap,rnb n.k niache hizi za kwaya kwanza, ila za kwaya kuzipiga ni very simpo kwenye kinanda lakini
usiache kufanya kwaya...kwenye kwaya Kuna ela sana, kanisa ndo huwa linalipa linaweka bajet kabisa..producer unapiga mdundo huku ela yako iko mfukoni na upako juuu
 
kwangu Mimi Yamaha mwisho wa matatizo ..plugins ni software zinazo tumika katika kutengeneza mziki...Kuna aina mbili za plugin, plugin zinazotoa saut na zisizo toa saut, plugin zisizotoa saut huwa tuna tumia kwenye mixing mf..Equalizer, compressor na plugin zinazotoa sauti ni kama vinanda,gitaa nk... mfano mzuri labda unataka kupiga gitaa na hauna ilo gitaa live sasa unaingia internet unadownload software ya gita unaiingiza kwenye kompyuta unaanza kupiga sasa hiyo software ndo plugin..
nimekuelewa sana.mimi napenda kusanple Kama DJ Premier au Duke Yamaha speaker bei gani?

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom