friendsofjeykey
Senior Member
- Aug 12, 2010
- 129
- 13
Dont hate the player, hate the game...considering huyo Hosea naye ana kashfa za kifisadi pia
Mkuu,Ilikuwa ni siku ya Desemba 9, 2010. Tanzania ilikuwa inasherekea miaka 49 ya Uhuru wa taifa. Baada ya kukagua gwaride Uwanja wa Taifa, Rais Jakaya Kikwete alifanya dhifa ya kitaifa Ikulu na kualika viongozi wa serikali, mabalozi, viongozi wa dini na wafanyabiashara wakuu.
Waalikwa wote, walikuwa wanaingia Ikulu kupitia mlango wa nyuma ulio karibu na bahari upande wa ferry. Lango kuu la kuingia Ikulu lilikuwa halitumiki kwa wageni siku hiyo na lilitumiwa na Rais na viongozi wengine wakuu. Magari yote, ikiwemo ya mawaziri na mabalozi yalipaki nje ya Ikulu kwenye uwanja mkubwa ulio karibu na ferry na wageni waalikwa waliingia kwa mguu kwenye viwanja vya Ikulu.
Mmoja wa wageni waalikwa mashuhuri wa Kikwete alikuwa ni Tanil Somaiya, mmiliki wa Shivacom Group of Companies.
Wakati mawaziri na mabalozi waliambiwa na maafisa usalama Ikulu watumie mlango wa nyuma wa kuingia Ikulu na kutembea mpaka kwenye gardens ambako sherehe ilifanyika, Tanil alipewa heshima ya kipekee na kuruhusiwa kutumia main entrance gate.
Tanil aliingia Ikulu na gari la kifahari jekundu (a red FERRARI) na kuipaki gari hiyo kwenye mlango mkuu wa kuingia IKULU ampako huwa gari la Rais ndipo linapaki.
Aliiacha FERRARI hiyo hapo kwenye lango la kuingia Ikulu kwa zaidi ya masaa mawili huku akijimwaga kwenye dhifa.
Mawaziri, mabalozi na vigogo wengine walibaki wamepigwa na butwaa iwaje wageni wote waambiwe waingie Ikulu kupitia mlango wa nyuma kwa mguu na kuacha magari yao nje halafu mfanyabiashara huyu apite main gate na kuweka gari lake kwenye main entrance ya lango kuu la kuingia Ikulu.
Tanil ni rafiki wa karibu na business partner wa Shailesh Vithlani, mfanyabiashara ambaye amekimbia nchi kutokana na kashfa ya rada.
Tanil, ambaye ametajwa kwenye WikiLeaks kuhusu rada, amehusishwa pamoja na Vithlani kwenye kashfa ya rada, military trucks, military choppers, Gulfstream presidential jet na scandal nyingine.
Inaeleweka kuwa Tanil alimchangia pesa nyingi sana Kikwete kwenye uchaguzi wa Rais uliopita na pia alitoa helikopta zake zitumike kwenye kampeni ya CCM, lakini hii ndivyo Ikulu ya Mwalimu Julius Nyerere inavyodharauliwa siku hizi?
Kwa kutumia main entrance na kupaki gari lake mbele ya lango kuu la Ikulu, Tanil alikuwa anataka kuwaonesha wageni wote kuwa yeye yuko karibu sana na Rais wa nchi na Ikulu ni kama nyumbani kwake.
Mbaya zaidi, kufuru hii ilifanywa siku ambayo Tanzania inaadhimisha uhuru wake. Kuna uhuru kamili kweli kama watuhumiwa wakubwa wa ufisadi wanafanya kufuru namna hii mpaka IKULU?
Unatarajia kweli Edward Hoseah wa PCCB anaweza kuondokana na uoga wa kumkamata Tanil kwa ufisadi wa rada wakati Rais wa nchi ni besti wake na Ikulu ni kama playground yake?
1. hakuna aliyehukumiwa kwenye kesi hii hivyo wote bado ni innocent
2. Issue ya kuingiza gari geti la mbele au nyuma ni kazi za walinzi au watu wa protocal hivyo ni non issue
3. Tangu lini ikulu ikawa ya Nyerere? Ikulu ni ya waTanzania wote au ushasahau kama nyerer naye alikuwa na secretary wake ambaye alikuwa CIA kwenye hiyo hiyo ikulu yetu?
4. Wikileaks doc...hosea mwenyewe anasema tatizo sio watu kupewa kamisheni ya 30% bali je ni halali?
5. Dont hate the player, hate the game...considering huyo Hosea naye ana kashfa za kifisadi pia
Ukiona comments kama hizo ujue mtoto wa fisadi yuko kazini.Comment kama hizi huwa zinaninyima raha kabisa......(and I always ask myself ni wangapi tuliobaki wenye uchungu na hii nchi) kwahiyo kama Hosea ana kashfa so its okay kwa wengine kuwa na kashfa????? au kuwa na kashfa kwa hosea inajustify huu upuuzi........ brother "Two wrongs dont make a right"
And what kind of a game is being played???? am sure wananchi are nor part of this game... they are just on the loosing end
Je wewe ulikuwepo??? Au wee ndio ulikuwa zamu ya ulinzi siku hiyo??? Hata hivyo mwandishi nawe wa story hii kiasi fulani unatia wasiwasi, iweje toka siku ya Uhuru tarehe 9/Dec, hadi hii leo ndio unaitoa hii story, kweli ???? Siku zote hizo ulikuwa wapi????? Unatia wasiwasi!!
jamani hivi ikulu inautakatifu gani?? acheni kufuru bwana.Nafuu Baba wa taifa JK Nyerere alijifia, sijui angefanyeje kuona sehemu takatifu kama ile ikichezewa na MAFISADI KAMA SOMAIYA. ........ NADHANI HATA SASA ANGEPEWA NAFASI YA KUFUFUKA NA KUSHUHUDIA MAMBO YANAYO FANYIKA, ANGESEMA BORA AENDELEE KUPUMZIKA KUZIMU.
HALAFU MOD KUFUTA POSTI ZA WENZAKO BILA KUTOA SABABU SI UUNGWANA. UMEZOEA SANA KUFUTA MICHANGO YANGU BILA KUTAJA SABABU ZA MSINGI ZA KUFANYA HIVYO.
nadhani wakati wa kulalamika umekwisha sasa sisi kama wananchi lazima tuchukue hatua kama nikueneza elimu ya uzalendo kwa watu waliokaribu na sisi ,ukitoa mifano ya jinsi mafedhuli walivyo na nguvu nchi hii wanaweza wakaamua nani awekwe madarakani ,nani atoke ,kupitishwa mbele na kinyume cha utaratibu uliowekwa kwa wanadiplomasia hii taabu sana hata kumeza,inauma lakini roho yangu inaniambia tuta vuk siku moja na watalia na kusaga meno
Kibopa aliyehudhuria tafrija ya uhuru wa Tanganyika alikuwa nje ya nchi. Nilikutana naye jana ndio akananipa taarifa hizi kwa uchungu mkubwa. Yeye anamfahamu vizuri Tanil na anaijua Ferrari yake ndio maana ikawa rahisi kwake kushuhudia tukio hili la kihistoria. In fact, Tanil ndiyo tajiri pekee mwenye Ferrari hapa Dar es Salaam. The shiny red car was very conspicuous pale mbele ya Ikulu. Lakini kwa mtu wa kawaida, tena ambaye hana interest na magari inaweza kuwa ni vigumu kwake ku-notice mambo kama haya. Nina hakika kuwa cctv image za Ikulu na huenda hata footage za tv kama TBC, ITV, Chanel Ten, Star TV, na Mlimani TV wanaweza kuwa walipata picha za gari hili jekundu mbele ya lango la Ikulu. Kibopa huyo kaniambia kuwa Tanil huwa anatamba kwa wahindi wenzake kuwa Rais ni rafiki wake wa karibu. "The president once asked me to give one of his girlfriends from South Africa a ride on my yatch," alisikika Tanil akitamba kwa watu. Tanil anasema kuwa yuko in regular contact with the president. Huwa anawasiliana na mkuu wa nchi kwa simu na sms kila mara. Hata walinzi wa Ikulu wanamfahamu sana ndiyo maana alipoingia na red Ferrari yake walibaki kumpungia mkono tu na kumruhusu apaki mbele ya lango kuu la Ikulu. Kwa ufupi, Ikulu ya nchi is his little playground.
nimeanzaje kusoma hapa napata hasira sana mimi! HALAFU EEETI WENGINE WANAPAITA PATAKATIFU ALAAAAAAAAAAAA!Kibopa aliyehudhuria tafrija ya uhuru wa Tanganyika alikuwa nje ya nchi. Nilikutana naye jana ndio akananipa taarifa hizi kwa uchungu mkubwa. Yeye anamfahamu vizuri Tanil na anaijua Ferrari yake ndio maana ikawa rahisi kwake kushuhudia tukio hili la kihistoria. In fact, Tanil ndiyo tajiri pekee mwenye Ferrari hapa Dar es Salaam. The shiny red car was very conspicuous pale mbele ya Ikulu. Lakini kwa mtu wa kawaida, tena ambaye hana interest na magari inaweza kuwa ni vigumu kwake ku-notice mambo kama haya. Nina hakika kuwa cctv image za Ikulu na huenda hata footage za tv kama TBC, ITV, Chanel Ten, Star TV, na Mlimani TV wanaweza kuwa walipata picha za gari hili jekundu mbele ya lango la Ikulu. Kibopa huyo kaniambia kuwa Tanil huwa anatamba kwa wahindi wenzake kuwa Rais ni rafiki wake wa karibu. "The president once asked me to give one of his girlfriends from South Africa a ride on my yatch," alisikika Tanil akitamba kwa watu. Tanil anasema kuwa yuko in regular contact with the president. Huwa anawasiliana na mkuu wa nchi kwa simu na sms kila mara. Hata walinzi wa Ikulu wanamfahamu sana ndiyo maana alipoingia na red Ferrari yake walibaki kumpungia mkono tu na kumruhusu apaki mbele ya lango kuu la Ikulu. Kwa ufupi, Ikulu ya nchi is his little playground.
jakaya kikwete uku kwetu wanamwita kubwa jinga...
kifupi kapoteza heshima yake, hafai hata kuwa mjumbe wa nyumba 10