Fisadi ni mtu gani?

Habari wanaJf,

Mimi najiuliza maswali kuhusu haya mazngumzo yaliopamba moto siku za karibuni, tangu Mh. J. Kikwete ( respect) aingie madarakani mazungumzo kuhusu UIFISADI (TU-taushinda) ambayo siku zote watu wkiongea lazima wata-involve serikali. Sijui kwanini?

Either fisadi huyo atakuwa serikalini au serikali iko involved!....

Mimi naomba 2wafichue mafisadi popote walipo! Ndani na nje ya serikali, kabla ya kuingia madarakani tuwe tushawafichua and prosecute them!.. Hasa hasa kwenye vyama vya siasa ambapo ndipo viongozi wanapotokea. Vyama vyote, chama tawala na vyama pinzani!...

Tuwe kama msumeno, tukate kote kote, hapo ndipo tutaushinda UFISADI!!
 
Ufisadi na ula rushwa ni matokeo ya kutumia mianya iliyopo kwa wakati fulani ndani ya madaraka yao kufuja pesa za uma. Inawezekana inasababishwa na hofu ya kwamba bila hivyo sitafanikiwa kiuchumi. Ufisadi mwingi tanzania umeongozwa na wasomi wenye kiwango cha phds na zaidi mfano ununuzi wa nyumba ya ubalozi italy. Inatia masaka sasa hawa wasomi wetu ndio wanatuletea hili janga. Hivi hii hofu ya wao kutofanikiwa kimaisha mpaka waibe inatoka wapi? Nisingependa kuona hawa watu wanapata shida mpaka wanatamani ardhi ipasuke wajizike. Tumeshudia hivi karibuni rais mstaafu wa korea kusini ajimaliza. Watu wasiogope kuwa mafisadi eti sababu watafungwa sababu kuu iwe ufisadi ni kinyume cha maadili. Hali iliyompata marehemu balali na hao wengine ni kwamba wamejifisadi wenyewe. Kuna watu hawaujui mshara lakini wanaishi miaka 100 kwa raha mustarehe.
 
Last edited:
Mkuu;


Kuna kitu inaishwa UTASHI.

Uliza Shetani alikosa nin i mbinguni hata akaamua kumwasi Muumba wake?
 
Rushwa Hongo:

ufisadi: Anything to do Kujinufaisha binafsi kwa kutokufuata taratibu zilizowekwa.
 
Wadau;
I have been reading here for a while, sio mchangiaji sana kwa sababu ya kutokujua kwa undani siasa za nyumbani and also plainly lack of interest, but I love my country so much. Ila leo ningependelea mnielimishe kidogo. "Fisadi" as used to identify certain politicians maana yake ni nini? if somebody can name all of them and the reasons why they are mafisadi pia itakuwa poa sana. What makes one a fisadi? or what are the features of a fisadi? Do we have a fisadi index so as we can rank them from top to bottom?


The goal is for all of us to reach a consensus of who are these mafisadi, and once we know them then a strategy can be set to oust them. You can not wage a war without knowing your enemy, or without knowing why one is your enemy.

One more thing, I will advise this forum to stop using the word fisadi. It has a negative connotation to it and I think once you demonize your enemy there goes the civility from the whole process. Lets address these fisadis with other lesser "devilish" word, respecting your enemy and politely pointing out their deficiencies as leaders will bring about changes most of you guys seek in a more Tanzanian way (peaceful way)..

My two cents!
 
Wadau;
I have been reading here for a while, sio mchangiaji sana kwa sababu ya kutokujua kwa undani siasa za nyumbani and also plainly lack of interest, but I love my country so much. Ila leo ningependelea mnielimishe kidogo. "Fisadi" as used to identify certain politicians maana yake ni nini? if somebody can name all of them and the reasons why they are mafisadi pia itakuwa poa sana. What makes one a fisadi? or what are the features of a fisadi? Do we have a fisadi index so as we can rank them from top to bottom?


The goal is for all of us to reach a consensus of who are these mafisadi, and once we know them then a strategy can be set to oust them. You can not wage a war without knowing your enemy, or without knowing why one is your enemy.

One more thing, I will advise this forum to stop using the word fisadi. It has a negative connotation to it and I think once you demonize your enemy there goes the civility from the whole process. Lets address these fisadis with other lesser "devilish" word, respecting your enemy and politely pointing out their deficiencies as leaders will bring about changes most of you guys seek in a more Tanzanian way (peaceful way)..My two cents!

Unasema hatuwaheshimu MAFISADI. Nenda China ukaone MAFISADI wanafanywa nini; wanahukumiwa kifo hadharani ili iwe fundisho kwa watu wengine.
 
Last edited:
Jamaa huyu anaboa -- hajui kabisa akina nani wanaididimiza nchi hii kuwa masikini. Ni serikali yote ya kifisadi -- hata ile sheria ya PCCB ya 2007 ni ya kijanjajanja - ina lengo la kulindana.

Kwanza haina hata definition ya 'fisadi" au "ufisadi" katika utangulizi wake. Pili adhabu ya makosa ya ufisadi ni kifungo au fine -- kama vile mtu aliyemtwanga mwenzie ngumi kwenye bar. Lengo ni kutopelekana jela, kwani watalipa faini kwa hela walizopata kifisadi. kama alivyosema mchangiaji hapo juu, kule China mafisadi wakipatikana hatia ni shaba tu.

Serikali haina nia kabisa nia ya kukomesha ufisadi hata ukiuitaje. After all what's in a name? Ukimwita 'fisadi' "swahiba' itaonda ile element ya wizi?

Mods waifunge thread hii -- kwani huyu seleman anaonekana kama vile anataka kujaribu kuwatetea.
 
This sounds funny! Huyu Selemani mwanzoni kabisa anaomba aelezwe maana ya fisadi, lakini pia anashauri watu wasiitwe mafisadi. Iweje atushauri tusiwaite mafisadi kama hajui maana ya fisadi. Katumwa na mafisadi huyu.
 
Neno fisadi ni neno la kiswahili fasaha likiwa na maana ni mtu ambaye anajilimbikizia vitu/mali bila kujali wengine. Mfano kuna mafisadi wa ngono, mafisadi wa mali nk. Hawa jamaa kuitwa mafisadi msingi wake mkuu ni mali walizoweza kulimbikizia ambazo hazikuangalia jamii inayowazunguka wana nini?? Ukiangalia maisha yao wanayoishi hawa viongozi wetu huwezi kuamini km ni mshahara tu na marupurupu halali ndo wanayotumia. Kuna hata na pesa chafu maana mishahara yao na marupurupu inajulikana na maisha halisi ya mtanzania yanajulikana. Leo hii iweje mtu km Chenge awe anamiliki zaidi ya Bilioni moja nje ya nchi. Utasema ni nini km si ufisadi?? Hapo unahitaji kuwa kipanga kujua hayo? Ila kaka km umetumwa hapa si mahala pake.
 
Fisadi kwa maana pana ya Kiuchumi ni mhujumu, mharifu anaye tumia njia za wazi au Ukuhadi kuharibu kile kilichopandwa kwa manufaa kinyume ya makusudio..patamu hapo!
Sasa tunapopanga mikakati ya Uchumi wetu, tukapanda mbegu za maendeleo yetu kisha wakatokea watu kati yetu kuhujumu kile kilichopandwa kwa kuiba mbegu zetu, kuuza kimagendo mali zetu, kupora matunda ya mbegu kabla hayajavunwa, na wengine kuiba mazao kabla hajayawafikia wananchi..na mengine mengi tu yanayohusiana na mal;engo ya uchumi huo hawa ndio Mafisadi..
Hivyo mtililiko wa Ufisadi unaanza toka tupande mbegu hadi mavuno yake.. Watu wote wanao hujumu hatua yoyote ya Ukulima huu wa maendeleo ya nchi ni MAFISADI.. hata iwe kumwagilia maji mengi mbegu zisipate kuota, au kukuhadia maliasili na rasilimali zetu ziwe mikononi mwa hawala wa kiuchumi.
 
Last edited:
Fisadi...hili ni neno ambalo limetokea kuwa maarufu midomoni mwa watu baada ya mkutano wa Mwembeyanga ambapo Slaa alilitumia. Neno Fisadi limekuwepo kabla likiwa na maana tofauti na maana inayotumika hivi sasa. Fisadi zamani ilikuwa mtu mchonganishi...

Wakenya na kiswahili chao cha kuunga wakalitumia neno fisadi kuanisha "corrupt government officials". Sisi kama kawaida tukaiga kutoka kwa wanafunzi wetu na kwa kuwa lina uwezo wa kuvuta hisia za wananchi wengi, likatumika.

Sisi tulikuwa na hawa:
Wala rushwa, Wahujumu uchumi (enzi za Sokoine hili lilipata umaarufu), nk

Tukirudi kwenye English - Swahili translation tunapata

Mla rushwa = Corrupt person
Mhujumu uchumi = Economic saboteur
Fisadi = ?

[ame]http://www.youtube.com/watch?v=IZFuQ99fy7A[/ame]
 
asili ya hili neno hasa ni lugha gani? labda hapa Umm Maggid au Barubaru wanaweza kutusaidia..
 
Fisadi = Mchonganishi

Tukubali tumeiga kwa wale wanafunzi wetu na kuvuruga lugha yetu. Au MMkijiji hili hulijui? Mmh...bongo kwa kuiga...teh he he
 
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu wangu jina Fisadi linatokana na neno la kiarabu - Fasad (i) ambao lina maana ya Corruption. Na kama ujuavyo kiswahili neno moja linaweza kuwa na maana millioni...mengine mtajaza wenyewe..
 
ningefurahii wote kwa pamoja tungetambuaa ufisadi wetu na kukirii ili tusongee mbelee..

kuendeleaa kunyoosheana vidole yaturudisha nyuma zaidi.
 
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu wangu jina Fisadi linatokana na neno la kiarabu - Fasad (i) ambao lina maana ya Corruption. Na kama ujuavyo kiswahili neno moja linaweza kuwa na maana millioni...mengine mtajaza wenyewe..


Ndugu zangu wana Jamii Forums Amani Iwe kwenu.

Nachukua wasaa huu kuweka sawa maana halisi ya neno Fisadi.

Asili ya neno hili ni lugha ya kiarabu kama alivyosema Mkandara, ila maana yake siyo (Rushwa) Corruption. Kiarabu kina neno Rash ambalo ndilo rushwa. Na mafundisho ya kiislam (Hadithi) imesema "AL Raash wal Murtash Mar uuni" yaani mtoa rushwa na mpokea rushwa wote wamelaaniwa. Haisemi Al Fasada....

Tafsiri sahihi ya Fisadi inapatikana katika Kurani, sura ya pili (Bakara) aya ya 11 , 12 na 27; Maana yake ni Mharibifu;


11. Na wanapo ambiwa: Msifanye uharibifu ulimwenguni. Husema: Bali sisi ni watengenezaji.

12. Hakika wao ndio waharibifu, lakini hawatambui.

27. Wanao vunja ahadi ya Mwenyezi Mungu baada ya kwisha ifunga, na wakayakata aliyo amrisha Mwenyezi Mungu kuungwa, na wakafanya uharibifu katika nchi; hao ndio wenye khasara.

Hapo ntaona kuwa Fisadi lina maana pana saana, kitendo / matendo yote yaletayo uharibifu katika nchi / ulimwengu ni ufisadi. Na mungu kawaahidi adhabu kali, hizo aya sikuziweka hapa. Hii ina maana kuwa hata

  1. uharibifu wa mazingira ni ufisadi
  2. uharibifu wa maadili mema kuhimiza watu wafanye mambo machafu katika jamii kama, ngono, watembee uchi n.k ni ufusadi.
  3. utoaji na ulaji rushwa ni ufisadi.
  4. Uhujumu uchumi, wizi, ubadhirifu wa mali ni ufisadi.
  5. Hata ubaguzi, fitina , chuki, uchonganishi, uzushi, uzindaki n.k vyote ni ufisadi
Na sifa kubwa anayotwambia mwenyezi mungu ni kwamba Fisadi akiambiwa wewe ni fisadi basi haraka hukanusha na kudai kuwa yeye ni mtengenezaji.

Kwa hiyo mafisadi kwa hali halisi ilivyo hapa Tanzania, wapo katika kila nyanja. Wanasiasa, wafanyabiashara, wafanyakazi, wanahabari, wataalam, Viongozi wa dini hata Raia wa kawaida.

Naomba tutambue kuwa vita ya ufisadi ni kubwa sana tofauti na wengi wanavyotaka tuamini kuwa mafisadi ni kundi dogo selikarini na kataika chama tawala tu kama wengi katika mtandao huu wanavyotaka tuamini.

Nadhani huenda hata vinara wa vita dhidi ya ufisadi wakawa ni mafisadi kwa tafsiri sahihi ya ufisadi.

Ili tufanikiwe turejee kwa mola muumba anasemaje; Kura ani 2 , 42;44
42. Wala msichanganye kweli na uwongo na mkaificha kweli nanyi mnajua.
44. Je! Mnawaamrisha watu mema na mnajisahau nafsi zenu, na hali nyinyi mnasoma Kitabu? Basi je, hamzingatii?


Hivyo basi lazi tuwafichue mafisadi wote bila kujali rangi zao, vyama vyao, kazi zao, uhusiono wetu na hukumu yao iwe ya haki. Hapo tutafaulu.
 
Aliye mbadhirifu, kwenye ofisi za umma?
Ajiona mtukufu, ni mvivu kujituma,
Apenda umaarufu, asiyejali dhuluma
 
Ulamaa,
Mkuu, kidogo umechanganya... Rushwa tafsiri yake ni Raash kwa kiarabu na Corruption inaangukia ktk neno Fasad..vitu viwili tofauti, rushwa ni moja ya vifungu ndani ya neno kubwa - Corruption. Hata kiingereza Fisadi (Corrupt person) ni Mharibifu ila mara nyingi tunaongeza ni kitu gani uharibifu huo unafanyika.
 
Last edited:
Back
Top Bottom