Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,395
- 39,531
FISADI NI MTU GANI?
Barazani naingia, wakijiji nasalimu,
Swali nalipangilia, mkanijuze walimu,
Hili ninaulizia, kwenu ninyi watalaamu,
Fisadi ni mtu gani, mimi ninaulizia.
Neno hili la fisadi, sasa lazidi tangaa,
Limekuja bila hodi, kila kona lasambaa,
Kama tungetoza kodi, "vijisenti" vingejaa,
Fisadi ni mtu gani, nauliza Tanzania.
Fisadi sifaze zipi, naombe mzichambue,
Zimekaa vyepivyepi, wananchi tutambue,
Tukwepe kama makapi, fisadi tuwagundue,
Fisadi ni mtu gani, kujua ni yangu nia!
Kila aliye muizi, huyo naye ni fisadi?
Kila mtu mdokozi, naye aibebe kadi,
Hata yule mchokozi, naye mtu mkaidi,
Fisadi ni mtu gani, nani ataniambia!
Aliye mbadhirifu, kwenye ofisi za umma?
Ajiona mtukufu, ni mvivu kujituma,
Apenda umaarufu, asiyejali dhuluma,
Fisadi ni mtu gani, mchango naulizia!
Asiyependa shauri, mgumu kushaurika,
Kutwa ni mtu wa shari, hapendi kukosoleka,
Anofura kwa jeuri, na ndita imekunjika,
Fisadi ni mtu gani, mashaka yameingia!
Lazima wa serikali, au hata mitaani,
Hili ndilo langu swali, kazini au sokoni,
Karamagi na Balali, sifa zao ndio nini,
Fisadi ni mtu gani, jasho linanishukia!
Mwenye kutumia ngono, kupata akitakacho,
Kutwa atazama porno, tumpe na cheo hicho,
Huyu fisadi wa ngono, au mpaka awe nacho?
Fisadi ni mtu gani, wakijiji ninalia.
Tumewaita Lowassa, na Chenge ni mafisadi,
Bangusilo hasahasa, naye tukampa kadi,
Kila mtu mwenye kosa, jina hili tunanadi,
Fisadi ni mtu gani, nani atanijulia!
Vidole vinaniuma, kuchapa sasa nakoma,
Mkono washika tama, kichwa changu chaniuma,
Swali langu nalituma, kaditamati na tama,
Fisadi ni mtu gani, mimi nawaulizia!!!
Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Shamba)
Barazani naingia, wakijiji nasalimu,
Swali nalipangilia, mkanijuze walimu,
Hili ninaulizia, kwenu ninyi watalaamu,
Fisadi ni mtu gani, mimi ninaulizia.
Neno hili la fisadi, sasa lazidi tangaa,
Limekuja bila hodi, kila kona lasambaa,
Kama tungetoza kodi, "vijisenti" vingejaa,
Fisadi ni mtu gani, nauliza Tanzania.
Fisadi sifaze zipi, naombe mzichambue,
Zimekaa vyepivyepi, wananchi tutambue,
Tukwepe kama makapi, fisadi tuwagundue,
Fisadi ni mtu gani, kujua ni yangu nia!
Kila aliye muizi, huyo naye ni fisadi?
Kila mtu mdokozi, naye aibebe kadi,
Hata yule mchokozi, naye mtu mkaidi,
Fisadi ni mtu gani, nani ataniambia!
Aliye mbadhirifu, kwenye ofisi za umma?
Ajiona mtukufu, ni mvivu kujituma,
Apenda umaarufu, asiyejali dhuluma,
Fisadi ni mtu gani, mchango naulizia!
Asiyependa shauri, mgumu kushaurika,
Kutwa ni mtu wa shari, hapendi kukosoleka,
Anofura kwa jeuri, na ndita imekunjika,
Fisadi ni mtu gani, mashaka yameingia!
Lazima wa serikali, au hata mitaani,
Hili ndilo langu swali, kazini au sokoni,
Karamagi na Balali, sifa zao ndio nini,
Fisadi ni mtu gani, jasho linanishukia!
Mwenye kutumia ngono, kupata akitakacho,
Kutwa atazama porno, tumpe na cheo hicho,
Huyu fisadi wa ngono, au mpaka awe nacho?
Fisadi ni mtu gani, wakijiji ninalia.
Tumewaita Lowassa, na Chenge ni mafisadi,
Bangusilo hasahasa, naye tukampa kadi,
Kila mtu mwenye kosa, jina hili tunanadi,
Fisadi ni mtu gani, nani atanijulia!
Vidole vinaniuma, kuchapa sasa nakoma,
Mkono washika tama, kichwa changu chaniuma,
Swali langu nalituma, kaditamati na tama,
Fisadi ni mtu gani, mimi nawaulizia!!!
Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Shamba)