FISADI kuzindua Albamu ya Flora Mbasha.

Indume Yene

Platinum Member
Mar 17, 2008
2,958
718
Lowassa kubariki ‘Furaha Yangu’ ya Mbasha
na Fortunatus Malamsha


ALIYEKUWA Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Edward Ngoyai Lowassa, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa albamu ya tatu ya mwimbaji nyota wa nyimbo za injili nchini, Flora Mbasha, inayokwenda kwa jina la ‘Furaha yangu’, utakaofanyika Agosti 24 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Akizungumza kwa njia ya simu jana, Flora alisema kuwa, wapenzi wa nyimbo za injili pamoja na mashabiki wake, wakae mkao wa kula, kwani yeye pamoja na kundi lake wamejiandaa vya kutosha kuwapa burudani wakazi wote wa Kanda ya Ziwa wakianza na Mwanza, ambako Lowassa atajumuika nao.

Flora alisema, huo utakuwa uzinduzi wa pili wa albamu hiyo yenye nyimbo 12, baada ya ule uliofanyika mkoani Dodoma Juni 29 mwaka huu.

Alisema, kwaya mbalimbali zitawasindikiza katika uzinduzi huo ambao atakuwa sambamba na mumewe, Emmanuel Mbasha na kundi lao, ni pamoja na AIC Shinyanga, JC Stars ya Dar es Salaam, Kekundu AIC na Makongoro AIC, huku jitihada za kuzungumza na waimbaji binafsi pamoja na kwaya nyingine zikiendelea, ili kufanya uzinduzi huo ufane zaidi.

Albamu hiyo imerekodiwa katika studio mbalimbali, ili kupata vionjo tofauti, zikiwemo Metro studio, Fabrees, Studio ya Marlon Linje na ile ya Said Comorien, zote za jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya nyimbo zilizomo katika albamu hiyo ni pamoja na ‘Mwanamke’ ambao umeanza kutamba katika vituo mbalimbali vya redio nchini, hasa kutokana na ujumbe wake kuwagusa wengi.

Katika wimbo huo, Mbasha anamwelezea mwanamke kuwa anaweza kufanya kila kitu, ikiwemo hata kushika madaraka ya urais.

Nyimbo nyingine ni pamoja na ‘Adui yako’, ‘Furaha yangu’ (uliobeba jina la albamu), ‘Anaweza’, ‘Jerusalemu’, ‘Rudi nyuma shetani’, ‘Tutamuona’ na ‘Tufurahie’.

Source: Tanzania Daima.



Ama kweli huu ni mkakati mzuri wa kusafisha FISADI lakini siamini kama hii itasaidia. Flora anatakiwa kuwa mwangalifu especially upande wa Marketing maana wananchi wengi wanaumia kwa ugumu wa maisha kutokana na uchafu ambao FISADIZ wamekuwa waki-practise. Na hao hao wananchi ndiyo wanategemewa kumchangia kwa kununua Albamu yake.

Image aliyonayo Lowassa kwa sasa siamini itamsadia Flora kuuza albamu yake. Naelewa Lowassa hatahusika directly kuuza Albamu ya Flora ila uhusika wa FISADI kuzindua albamu unaweza kuangaliwa kwa Mtazamo tofauti. Wanachi wana machungu na hawa FISADI, sasa kumhusisha kuzindua Albamu kunaweza kupokewa kwa different impression.
 
Hivi kwanini waimbaji wa muziki wa injili wasiwatumie viongozi wao let say Maaskofu/Wachungaji/wakuu wa vyuo au taasisi zao mbalimbali katika uzinduzi wa miziki yao? Vijisenti wanavyovitafuta kwa wanasiasa vitawaharibia.
 
Ngome ya mafisadi tz ni makanisaa na misikitii. Huko ndiko wanakoenda kujificha na kutambikia ili shetani wao awazidishie mbinu za kuwafisadi watz, baada ya kutoa sadaka na zaka zao zitokanazo na ufisadi! Na wakuu wa hayo makaniesaa na misikitio huwabariki hawa mafisadi wazidi kuwanyonya watz!
 
Aliyesema mbinguni mbali alikuwa na akili sana. mbele ya pesa hakuna kisichowezekana
 
Muziki wa gospel ni dili siku hizi,wamevamia wengi na wanatafuta pesa wala si kumsifu mwenyezi tena.
Lengo limekuwa pesa wala si kumtukuza Mungu,na mafisadi nao wamegundua hilo na kuingia makanisani moja kwa moja.

Huyu Flora mBASHA naamini ni yule aliyezunguka kwenye kampeni za Kikwete mwaka 2005 akiimba.Huyu ni mmoja wao wala hatushangai sana.
 
Back
Top Bottom