First Lady umesahau ulikotoka?

First Lady umesahau ulikotoka?

Siasaniupendo

Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
20
Reaction score
7
Nakumbuka kabla jk hajawa JK, Mama Chalma alikuwa mwalimu pale sinza. Kila mwisha wa mwezi,tulipigana vikumbo wilayani kugombea mishahara. Najua kabisa, hali ile hakuipenda, maana ni hatari kwa walimu na ulikuwa ni usumbufu mno. Wakati mwingine walikuwa wanasota kwa masaa kibao, ikibidi kurudi siku ya pili hadi ya tatu kabla hawajapata mishahara yao.

Sasa Mama umekuwa First Lady kwa miaka 7, umefanya nini kuwasaidia walimu wenzako? Je unafahamu vijijini wapo walimu hawajalipwa kwa miezi kadhaa? Chondechonde mama yetu, tufikishie ujumbe kwa baba, ikiwezekana siku yake ya kuzaliwa mpelekee sinia tupu bila ya keki.

Baba akiuliza nini hii tena, mwambie "IMEPITA ZAIDI YA MIEZI MIWILI, SIJALIPWA MSHAHARA WANGU?
Baba akiuliza mshahara gani?

Mama tafadhali mjibu, Mimi ni mwalimu, umesahau? Baba Riz anaweza kuelewa somo, na kutoa msaada kwa walimu wetu
 
Kimsingi hana uwezo huo, ila kwa woga wa ki-TZ ana uwezo wa kufanya hivyo
 
Anakula kuku sasa hivi hawezi kukumbuka alikotoka hata siku moja lakini atahukumiwa kwa kushindwa kutumia nafasi yake kama first lady kumshauri baba Riz
 
Angel Msoffe umeua kabisa!
Umemkoma nyani- source le mutuz
 
Kama unategemea heri chini ya utawala wa CCM umepotea ndugu, chukua hatua, siku ya ukombozi yaja, iunge mkono.
 
Angel Msoffe umeua kabisa! Umemkoma nyani- source le mutuz
hawa walimu inabidi tuwape za uso mana wamezidi! Kila siku kulalamika lalamika hawachukui hatua yoyote, wanategemea huruma ya mama Salma! Kila mtu aipiganie nafsi yake waige mfano kwa Madaktari.
 
Mbona anapokujaga huko mashuleni kumuuzia mumewe sera hamumpagi vidonge vyake!? Kazi yenu ni kufunga watoto"wanafunzi"vibwebwe na kuwaambia wamwimbie nyimbo za kumpongeza! Nyie walimu nyie kinachowatesa ni uoga na unafiki.
You have said it all Angel!
 
Mbona anapokujaga huko mashuleni kumuuzia mumewe sera hamumpagi vidonge vyake!? Kazi yenu ni kufunga watoto"wanafunzi"vibwebwe na kuwaambia wamwimbie nyimbo za kumpongeza! Nyie walimu nyie kinachowatesa ni uoga na unafiki.

Woga na unafiki una sababu. Wanauma na kupuliza kwa sababu wengi hawana sifa za kuwa walimu in the first place. Wakikazania kuuliza mshahara watadaiwa kupeleka vyeti! Wengi wao ni aibu tupu. "Usile na kipofu ukamkamata mkono" Serikali ni kipofu, hawataki kuishika mkono.
 
Ubinafsi wetu cku zote una2fanya 2sahau 2likotoka. Mama Salma hajui wala kukumbuka kama kuna foleni popote. Hatoki jasho kwa lolote na hatathubutu kutoka jasho kwa kukumbuka yaliyopita. Sisi tunaweza kufanya mabadiliko ktk nafasi ndgo 2lizonazo na hii itatujengea uwezo wa kuthubutu 2takapokuwa na nafasi kubwa.
 
alivyo na mzaha hata kwenye mambo ya msingi mbona atakenua kama miss tanzania tuu
upuuzi mtupu....sasa yeye ni nani ? Ni just mke tu..hiyo first lady ni title tu hana uwezo huo...usimchukie mtu mpaka basi tu...ogopa mungu...
 
Woga na unafiki una sababu. Wanauma na kupuliza kwa sababu wengi hawana sifa za kuwa walimu in the first place. Wakikazania kuuliza mshahara watadaiwa kupeleka vyeti! Wengi wao ni aibu tupu. "Usile na kipofu ukamkamata mkono" Serikali ni kipofu, hawataki kuishika mkono.

Mween. nakuhakikishia katika sekta yenye watu wanaoqualify tena wasomi ni elimu, hii ni sehemu utakayopata watu wenye vyeti hadi PHD. sisi waalim tuko hivi tulifundishwa kuwa na nidham sana na pia tulifundishwa kujiheshimu ingawa sasa ile heshima imetumika kama kamba ya kutunyonga. ipo siku tutaamka na sisi manake ni binadami na uvumilivu huwa unamipaka yake.
 
walimu mpaka mtakapo badilika ndiyo mtafaidi haki yenu kwa kuendelea kumchekea nyani (CCM) mtaendelea kuvuna mabua! Uchaguzi ukifika mnasema zimwi likujualo sasa cha moto mnakiona!
 
Wasiosoma ni chakula cha wasomi and viceversa is true
 
mshaurini afuate ushauri wa Bi Sofia simba na Bibi mkwasa, amnyime nanii mpaka atekeleze madai ya walimu
 
Mween. nakuhakikishia katika sekta yenye watu wanaoqualify tena wasomi ni elimu, hii ni sehemu utakayopata watu wenye vyeti hadi PHD. sisi waalim tuko hivi tulifundishwa kuwa na nidham sana na pia tulifundishwa kujiheshimu ingawa sasa ile heshima imetumika kama kamba ya kutunyonga. ipo siku tutaamka na sisi manake ni binadami na uvumilivu huwa unamipaka yake.

Ni kweli elimu kuna watu wamesoma sana lakini kumbuka waalimu wa shule za msingi ndio wengi na wengi wao hawana sifa za kuwa waalimu.Mimi ni mwalimu kwa kitaaluma(UDSM) sikumbuki kama nilifundishwa kuogopa kudai haki zangu!!Waalimu wengi ni wanafiki na waoga ndo maana hadi leo siutaki huo ualimu!
 
Uliyosema ni kweli. Namshauri mama Kikwete arudi kule alikotoka asaidie kutatua kero za huko kwa nguvu zake zote. Kumbuka Salma kuwa Mumeo karibu kuachia ngazi nawe utakuwa tena mitaani japo katika hali tofauti na watu wengine lakini bado utatazamwa kwa kile ulichofanya. Pia ukifanya vema una nafasi ya kuja kuwa hata mwanasiasa kwa kupitia kazi zako ukiwa first lady.

Wala watu uliokuwa ukishirikiana nao kulalamikia kero mbalimbali. baadhi okipata nao chai ya saa nne na maandazi au mihogo wapo wanakutazama hawajakata tamaa.
 
Siamini mwalimu wa UDSM anasema maneno ya dharau kwa walimu wa shule za msingi. Bila wao usingefika ulipo, hata hapo UDSM pia hamna hadhi, mnajikomba kwa watawala mteuliwe. Kama ungekuwa sio mwoga mbona haujatoka hata siku moja kuwatetea wanafunzi wako wanaopewa posho 2000 kwa week? Go back to school, to learn theraputic language.

Ni kweli elimu kuna watu wamesoma sana lakini kumbuka waalimu wa shule za msingi ndio wengi na wengi wao hawana sifa za kuwa waalimu.Mimi ni mwalimu kwa kitaaluma(UDSM) sikumbuki kama nilifundishwa kuogopa kudai haki zangu!!Waalimu wengi ni wanafiki na waoga ndo maana hadi leo siutaki huo ualimu!
 
Huna maana kabisa wee, unamdhalau mwanamke kiasi hicho, where are from? Unadhalau mchango wa mke katika jamii? Leo ni Jpili, nenda kanisani kaungamena Uombe Ufunuo.
upuuzi mtupu....sasa yeye ni nani ? Ni just mke tu..hiyo first lady ni title tu hana uwezo huo...usimchukie mtu mpaka basi tu...ogopa mungu...
 
Back
Top Bottom