First Lady umesahau ulikotoka?

Nakumbuka kabla jk hajawa JK, Mama Chalma alikuwa mwalimu pale sinza. Kila mwisha wa mwezi,tulipigana vikumbo wilayani kugombea mishahara. Najua kabisa, hali ile hakuipenda, maana ni hatari kwa walimu na ulikuwa ni usumbufu mno. Wakati mwingine walikuwa wanasota kwa masaa kibao, ikibidi kurudi siku ya pili hadi ya tatu kabla hawajapata mishahara yao.

Sasa Mama umekuwa First Lady kwa miaka 7, umefanya nini kuwasaidia walimu wenzako? Je unafahamu vijijini wapo walimu hawajalipwa kwa miezi kadhaa? Chondechonde mama yetu, tufikishie ujumbe kwa baba, ikiwezekana siku yake ya kuzaliwa mpelekee sinia tupu bila ya keki.

Baba akiuliza nini hii tena, mwambie "IMEPITA ZAIDI YA MIEZI MIWILI, SIJALIPWA MSHAHARA WANGU?
Baba akiuliza mshahara gani?

Mama tafadhali mjibu, Mimi ni mwalimu, umesahau? Baba Riz anaweza kuelewa somo, na kutoa msaada kwa walimu wetu

hivi kwa nini mama yako sio first lady? mwambie baba yako amfanye mama yako kuwa first lady matatizo yote yatakwisha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom