BekaNurdin
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 2,267
- 2,044
Kuanzia leo sina tatizo tena la kujibu nyie watu, jibu langu litakuwa moja tu na lenyewe ni hiii link ya documentary ya BBC:
https://www.jamiiforums.com/international-forum/736913-finally-bbc-speaks-the-truth.html
BBC wamenirahisishia kazi kwani vitu vyote ambavyo nilikuwa nasema hapa na nyinyi mnapinga kwa kuniitwa interahamwe ndio hivyo hivyo wamesema BBC, this proves kwamba either i wasn't lying, or ME AND BBC are INTERAHAMWE, you take a pick!
Humo kuna idadi ya tutsis waliokufa genocide, ushahidi wa kagame kutungua ndege, mauaji ya kimbari dhidi ya wahutu, political assasinations, Kuzuiwa kwa UN forces by kagame (tena kufukuzwa actually!) na yote ambayo nilishayasema na nyinyi mkabisha. Sasa kila siku you will have to call BBC interahamwe, besides kwa vile kila mtu anaweza kutazama mwenyewe na kuamua, mi nadhani tusipoteze mapovu bure hapa JF.
cc: Talkandtalk murutongore.
Yenyewe hii video ina utata kweli, yaani inawezekana kweli Kagame ndiye kalipua ndege na kusababisha hayo maafa yote. Jamaa namuona siku zote kama shupavu na mwenye upendo na kuwaunganisha Warwanda. Sasa hii sijui kama ni propaganda za Wazungu ama vipi. Haya mambo ya Rwanda siyajadili tena, nageuza na kurudi kwenye masuala ya nchi yangu Kenya. Tuna matatizo yetu mengi ya kuhangaika nayo. Nawaacha Warwanda wajijue, waamue kutengeneza nchi yao ama waichome tena.

GACACA lilikuwa jukwaa la maridhiano zaidi kuliko mahakama. Ebu soma maelezo haya hapa.
However, there was no time to waste as the new Tutsi-led rulers were keen on showing the survivors and the international community that justice was being done in arresting and putting on trial those who were involved.
During these trials(GACACA), defendants are given shorter sentences in exchange for confessing and are encouraged to seek forgiveness from the victims family. The survivors are also able to finally discover how their loved ones were killed and where their remains had been disposed of.
But these trials provoked anger among many genocide survivors who thought the Gacaca courts would let many killers off the hook by allowing them to enter plea bargains.
SOURCE:Rwandaâs Gacaca courts: a mixed legacy -- New Internationalist
Maridhiano gani hayo ambayo msingi wake ni kuwa wahutu ndio wakosaji pekee? na maridhiano ya Rwanda yanatakiwa kufanywa kupitia mazungumzo sio kupeleka watu mahakama za ajabu ajabu.
.....hiyo video haiongelei Africa inaongelea Rwanda. We vipi mbona una-generalize vitu!Toka lini mzungu akaitakia mema afrrika?
wafukunyuku wa mambo ya rwanda si wa rwanda,vita inayopiganwa misitu ya congo nani anafadhili buti,chakula ,silaha,mahema,radio comm,etc ni nani? Na kwa faida ya nani? Ili iweje?.....hiyo video haiongelei africa inaongelea rwanda. We vipi mbona una-generalize vitu!
hii ni sehemu ya afrika,.....hiyo video haiongelei africa inaongelea rwanda. We vipi mbona una-generalize vitu!
Mpaka hapa utakuwa umekubali kuwa kwa kiasi fulani Kagame alikuwa na nia ya dhati ya kuharakisha maridhiano nchini mwake. Kwa maelezo yako ya awali juu ya GACACA yamekosa ushahidi usiotiliwa shaka kuwa GACACA ilikuwa kwa ajili ya kuwamaliza baadhi ya waafrika wa Rwanda na kuwaacha wengine.
Sasa waweza kuendelea na mkakati wako juu ya serikali ya waafrika wa Rwanda....lakini ukijichanganya tena sisi waafrika (sina hakika kama na wewe ni mwaafrika mwenzetu) tutakurudisha kwenye mstari.
Kimsingi Kagame uhalifu aliofanya alikuwa- supported na UK, US, Canada & Israel. Wazungu wanaanza kumgeuka, mwishowe atabaki peke yake na kusimama The Hague kupewa haki yake anayositahili!
1. ....... Mkataba wa kugawana madaraka ulishasainiwa na RPF/kagame na serikali hiyo hiyo ambayo anadai eti ilipanga kuwamaliza watutsi....... Kagame alipoingia madarakani akavunja mkataba..... Sasa hapo kuna maridhiano gani? Wanyarwanda hawajakubali uhalali wa Kagame ku-dictate maridhiano yaweje wakati yeye alikuwa ni upande wa RPF! Nani anawakilisha serikali ya Habyarimana.....?
2. Nimewahi kusingiziwa Uhutu lakini hii ya kuambiwa sio mwafrika kwangu mpya...kama "huna uhakika mimi ni mwafrika" unadhani mimi ni nani? mchina? mzungu? ....
......
Lakini nadhani wadau wenzetu hasa kutoka Rwanda wanaweza kuwa na la kuchangia. Maoni ya jamaa waliokuwa na Kagame nadhani si ya kupuuza hata kidogo, tena yametolewa kupitia BBC. Ingekuwa ni media ya kijinga nadhani ningepuuza, lakini BBC si media blog au sio extremeist media outlet.
......
Yenyewe hii video ina utata kweli, yaani inawezekana kweli Kagame ndiye kalipua ndege na kusababisha hayo maafa yote. Jamaa namuona siku zote kama shupavu na mwenye upendo na kuwaunganisha Warwanda. Sasa hii sijui kama ni propaganda za Wazungu ama vipi. Haya mambo ya Rwanda siyajadili tena, nageuza na kurudi kwenye masuala ya nchi yangu Kenya. Tuna matatizo yetu mengi ya kuhangaika nayo. Nawaacha Warwanda wajijue, waamue kutengeneza nchi yao ama waichome tena.
1. Ni kweli maridhiano yalifikiwa Arusha. Na yalitakiwa kueshimika na pande zote mbili serikali ya wakti huo na RPF....Lakini kabla ya kuanza kutekeleza maridhiano hayo, inatokea kadhia inayoondoa uhai wa mtu/watu muhimu katika makubaliano hayo, Rais wa Rwanda (Mungu amurehemu) na kufuatiwa na mauaji ya kutisha yanayosemekena kufanywa kwa kiasi kikubwa na baadhi ya viongozi na askari wa serikali ya wakati huo, na kikundi cha RPF kilichokuwa kikipigana kuiteka Kigali kwa madai ya kukomesha mauaji. Mpaka RPF wanafika Kigali viongozi wa serikali ambao walitakiwa kutekeleza kwa pamoja na RPF, makubaliano ya Arusha walikuwa ama wamekimbia nchi au kuuwawa wakati wa harakati za RPF kuikamata Kagali. Sasa katika mazingira haya RPF/Kagame angetekelezaje makubaliano hayo bila kuwepo upande wa pili?
Kagame kwa kutambua umuhimu wa upande wa pili katika kuwaunganisha tena waafrika wa Rwanda akaona ni vyema kuwa na mfumo wa kimaridhinao ambao ulikuwa na lengo kama lile la makubalino ya Arusha. Mfumo huo ndiyo GACACA. Na ni katika GACACA ambapo upande wapili ulikuwa umepewa nafasi ya kurudi mezani kutekeleza maridhiano (rejea post na.44 ya uzi huu na soma nukuu ). Upande wa pili haukukubali...wakaenda mafichoni huko misitu ya Kongo(FDLR) wakaanza kuleta chokochoko za kuhatarisha usalama wa waafrika wenzao walioko Rwanda.....kilichoendela unakijua. Narudia tena katika mazingira haya utamlaumu vipi Kagame kushidwa kutekeleza maridhiano ya Arusha?
2. Nashukuru sana kwa kukutambua kuwa na wewe pia ni mwafrika mwezetu. Ni wie radhi kwa kutokutambua mapema kuwa na wewe ni mwafrika mwenzangu. Na sababu ni moja tu ya kutokukutambua nikuwa nilipoangalia JF ID yako nikaona wewe siyo Verified user hivyo imeniwia vigumu kutumia mbinu za kukutambua kuwa wewe ni Mwaafrika.
Uwenda ukawaza kuwa nilifanya makusudi kuwa sijakutambua kuwa wewe ni mwafrika kwani unaweza kuandika lugha ya kiswahili vyema! kwamba hiyo inatosha kukutambua. Siku hizi kiswahili kinazungumzwa na kuandikwa kwa ufasaha na wachina, wazungu, nakadhlika nakadhaliaki.
Kwa leo naishia hapa.
Nashukuru mimi hujanipiga ban kuchangia post hii...
Mimi sikubalini na wewe kuwa BBC ni chombo cha kuaminika asiliamia mia moja kwa kila tahariri, habari ama makala yoyote inayoandaa. Kuonyesha udhaifu wa BBC katika hili rejea uchaguzi wa juzi huko Scotland. BBC waliegemea upande mmoja...wamefanya hivyo Iraq wamefanya hivyo Libya wamefanya hivyo Syria na wanendelea huko Ukraine; ushahidi upo.
mfano suala la scotland
https://www.jamiiforums.com/interna...ill-go-to-the-wire-bbc-biased-to-no-vote.html

.....
By the way sizui mtu, lakini si vizuri kuwaweka wenzetu kwenye mazingira magumu na kutonesha madonda yao kwa kuwafanya wachangie kwenye mabandiko kama haya....
Katika hili BBC wanaaminika 100% hakuna chochote ambacho kinapingika. To make it worse upande unaotuhumiwa wote wamekataa japo kutoa maoni yao. Lakini kagame huyo huyo akiandaliwa mahojiano na BBC hiyo hiyo kupitia PR companies anakwenda kwa moyo mmoja. Kagame huyo huyo akitoa press release anatumia BBC hiyo hiyo. Sasa kwa nini BBC hiyo hiyo ikifanya independent documentary kagame akatae.