Filamu ya Escape from Pretoria ni nzuri?

Hziyech22

JF-Expert Member
Jun 8, 2019
13,577
18,901
Kwa wale walioiona hii movie vipi ni nzuri? Na inahusu nini?

CE906DEE-62B5-476B-A397-BD44DB3EDF1B.jpeg
 
Ni bonge la. Movie
Kiufipi inaelezea namna wazungu wawilo waliokatwa kutokana na harakati zoa huko mtaani na kupelekwa gereza la Pretoria. Sasa huko ndio kutamu majamaa wanahangaika kutoroka mpaka wanakuja kufanikiwa.

Nilipopenda ni idea ya kuchomga funguo ya Mbao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni movie ilichezwa katika nchi ya S.AFRIKA inayohusu wazungu wawili wapigania uhuru katika nchi hiyo jinsi walivojitahid kupambana na mwisho wa siku kuishia gerezani PRETORIA gereza kubwa huko S.AFRIKA..Ni movie nzuri sana na uzuri wake unaonekana pale majamaa wanavyopambana hadi kutoroka gerezani humo.

Inatofauti gani na ya a scape from sobibor??
 
Labda nijaribu kutoa maoni

Tofauti ipo kubwa sana.
1. Sobibor inahusu kutoloka kwa idadi kubwa ya watu yaani ilikuwa plan ya watu wengi lakini hiyo ingine ni watu wachache sana mi Wanne tu ambapo Wawili ndio vinara.

2. Huko Sibibor ilikuwa ni Working Camp lakini Kule ilikuwa ni Gerezani ambapo kulikuwa na mengi zaidi ya Kazi.

3. Kwenye Sobibor inahusu Jews kutoroka katika mikono ya Germany lakini huko ni Wanaharakati wakigeni wakitoroka katika Gereza walilofungwa na Wazungu wenzao yaani Makaburu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa wale walioiona hii movie vipi ni nzuri? Na inahusu nini?

View attachment 1445539
...Hawakupenda udhalimu uliofanywa na watu weupe kwa watu weusi..rangi zao nyeupe zikapishana lugha na weupe wenzao..wakaamua kuingia mtaani kumwaga karatasi za haki..ni karatasi hizo ndizo zilizowapeleka jela.

Yess..makao ya utetezi wao ikawa ni ndani ya jumba lenye kila aina ya unyama...askari wenye miili yenye roho za wadudu...na maisha asiyostahili mwanadamu...wakakukubali ukweli,wakaamua kuuishi..

Lakini sio kwa Kim Jenkin.

Mhuni mweupe kati ya wale wawili walioingia Pretoria prison...mwili mdogo,macho yanayohitaji miwani na upole uliopitiliza..vyote hivo vilibebwa na kichwa adhimu chenye uwezo wa kufikiria maili milioni moja kwa dakika..ndio jenkin ni genius wa kizazi cha south africa.

Wakati bwana jela anaisifu jela yake kuwa na milango ya chuma 39...jenkin alikuwa anakiamini kichwa chake kuwa ni funguo ya kila geti lililosifiwa na kiongozi yule...jenkini ndo pritoria prison gates keys.

Miaka 12 aliyoambiwa alitumikie gereza. Alihitaji siku zisizozidi 360 kuuonesha ulimwengu kile kilichobebwa na kichwa chake.. ni akili za kiufundi zinazohitaji umakini uliopitliza...jenkin ni michael scofield wa mwaka 2020.

Kila alichoangalia jenkin ndani ya gereza kiliji save kwenye kichwa chake...alihitaji dakika 5 tu kuziangalia funguo za bwana jela kwenye kiuno...na asubuhi ya siku iliyofuata alikuwa na funguo yake ya mbao iliyotokana na fagio...ni jenkin genius.

Moja kati ya vitu vinavoifanya hii movie kuwa nzuri kwetu...ni kushuhudia plan za jenkin zikipangwa kupitia msumbiji kuja Tanzania...ndio

Jenkin na wafanya

Fujo wenzie wamechora ramani ya kuitamka tanzania kwa jina...wakiamini usalama wao ndani ya nchi yetu..mpaka kufika watapoenda.

Ni presha...ni fujo...ni akili na taharuki zitazokufanya ukae roho juu muda wote ukiamini kuna kitu kitafeli...kuna muda utatamani kumsaidia jenkin...na kuna muda utaamini jenkin haitaji msaada wako.. bali wewe ndo unahitaji kuwa jenkin kwenye maisha yako.

Je watafanikiwa?

ESCAPE FROM PRETORIA...2020...

C & P
 
Nitaitafuta hii move just because of your brilliant narration

Back
Top Bottom