FILAMU BORA YA MUDA WOTE TANZANIA

FILAMU BORA YA MUDA WOTE TANZANIA

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,741
Reaction score
25,681
GIRLFRIEND ni jina la filamu iliyotoka mwaka 2003 nchini Tanzania. Filamu inahusu muziki na maisha na ndani yake anakuja T.I.D, Yvonne Cherrie (Monalisa), Beatris Morris (Nina), Jay Moe, A.Y na King Crazy GK.
Filamu inaonesha jitihada binafsi katika kile unachokiamini na mwisho wa siku unatusua. Picha linaanza TID maisha magumu, harakati kila siku, huku ana mpenzi wake wa karibu mara kulala na njaa, mara hivi. Basi tu ilimradi maisha ya bahati nasibu. Hatimaye wakatoka katika namna ya kipekee licha ya majaribu kadhaa yaliyoonekana katika kipindi kigumu cha maisha yao. Filamu ina kibwagizo chake kinaitwa Girlfriend ambacho kiliimbwa na T.I.D akishirikiana na Jay Moe kutoka Bongo Records.



MUHTASARI WA FILAMU

Filamu inaanza Eric (T.I.D) akiwa nyumbani anasikiliza Sister Sister ya King Crazy GK kwa zogo kubwa. Ghafla Zuwena anaingia kuzima mazogo yale. Zeuna anamsihi mpenziwe atafute kazi ya kufanya na si hiyo ya muziki. Eric anaamini katika muziki na kamwe hawezi kuacha muziki. Zuwena anaona muziki hauna faida yoyote kwa Eric, kwani hata kodi inamshinda kulipa.

Mazungumzo yao hatimaye wakakubaliana kwenda wote katika kilabu ya muziki. Huko kilabuni, hakuwa kwenye ratiba, anabahatisha kutumbuiza. Kilabuni anaonekana Ndende, Jay Moe. Jahffarie, Sista P., G.K. anayebughudhi wasichana kilabuni hapo akiwa na A.Y. Stella (Nina) anamshawishi Zuwena aachane na Eric kwa vile hana kitu.
Bila mafanikio.

AY anamwona Zuena na kujaribu kumkuwadia GK. Eric bado hali mbaya katika kukubaliwa kutumbuiza. GK na AY wanarudi tena kuja kumbughudhi Zuwena. Zuwena anahofia nongwa na Eric na kuamua kuwatimua wawili wale. Kilabuni kunazuka ugomvi kila sehemu, GK na AY wanaleta fujo, hawataki kulipa pesa za vinywaji walivyokunywa.
Hadi mwisho, Eric kabaniwa kutumbuiza kule kilabuni. Nyumbani kwa GK kinanuka kati ya Stella na mwanamke mwengine (Joan). GK kagonganisha magari.
Nyumbani kwa Sam (kaka yake Eric), malumbano makubwa ndani ya nyumba. Amekuwa kisirani kiasi hata mkewe anaoiona hiyo hali.


Washiriki
Pumzika kwa amani George Tyson


 
bongo movie ni bongo movie tuu, unaweza kuta movie imepangiliwa vizuri lakini bado mlinzi dish limeyumba n.k
 
CCM inawakumbusha wapiga kura wake wote wasiokata tamaa miaka na miaka ya kua msilale bila kuweka neti malaria isiwaguse mfikishe 2020, baada ya hapo utaamua hata kulala kwenye karavati. Usiku mwema
 
Back
Top Bottom