Leo Oktoba 14, 2024 tunakumbuka kifo cha muasisi wa Tanzania Mwl. Julius Kambarage Nyerere aliyefariki siku na mwezi kama leo mwaka 1999 takribani miaka 25 sasa imepita
Baada ya Tanzania kupata uhuru wake mwaka 1961 Mwalimu Nyerere alipata kufanya ziara nchini Marekani (USA) alikutana na Rais wa 35 wa nchi hiyo John F. Kennedy maarufu kama JFK
Mwalimu alivutiwa sana na siasa za Marekani na aina ya uongozi wa Rais Kennedy na aliporejea nchini Tanzania akawa na mawazo ya kufuata siasa hizo za Marekani za ubepari.
Ikumbukwe kuwa Mwl. Nyerere baadaye akaja kuwa rafiki mkubwa na mpenzi wa uongozi na siasa za Kennedy na JFK naye akavutiwa na Nyerere wakawa maswahiba.
Haikuchukua muda mwaka 1963 Rais huyo wa USA akauawa kwa kudunguliwa na risasi na walenga shabaha. Mwalimu alihuzunishwa sana na kifo hicho akamlilia rafiki yake Kennedy.
Baada ya kifo cha Kennedy Mwalimu Nyerere alifanya ziara nchini China huko pia akavutiwa na siasa za nchi hiyo na uongozi wa Mao Zedong.
Mahaba ya mwalimu yakahamia kwenye siasa za "ukomonisti" akaona ndio siasa kistaarabu zenye kuleta umoja wa nchi na kuheshim utu wa mtu
Baadaye Mwalimu Nyerere akawashawishi wenziye na chama chake cha TANU na kuanzisha siasa zinazoendana na ukomonisti akaziita siasa za Tanzania ni siasa za ujamaa na kukitegemea
Hapo ikawa Mwalimu amebadilika kabisa kutoka kufikiria siasa za ubapari za rafiki yake Kennedy na kufuata siasa za Ujamaa
Mnamo mwaka 1967 Mwalimu akiongoza chama chake cha TANU wakakutana Arusha wakapitisha azimio la Arusha hapo ndipo nchi ilipoanza kuzama jahazi lake na kutopea kwenye umaskini wa kutupa mpaka sasa
Siasa za ujamaa na kujitegemea za Mwalimu Nyerere na itikadi ya Azimio la Arusha hazitaki utajiri wala watu kufanyabiashara kubwa na kupata utajiri na kujirimbikidhia utajiri
Ile sera yake ya binadamu wote ni sawa ndio walitaka hata kwenye kipato watu wote wawe sawa kusiwe na matajiri na maskini.
Hatuwezi kuendelea kwa sera hiyo ya Azimio la Arusha na siasa za kijamaa za aina hiyo za Mwalimu Nyerere
Kuthibitisha hilo miaka ya 80 mwalimu alimtuma waziri mkuu wake Edward Moringe Sokoine kuwakamata wafanyabiashara wote wakubwa na kuwaita majina mabaya "wahujumu uchumi"
Matokeo yake wafanyabiashara wakatiwa ndani wengine wakakimbia nchi na hao waliotiwa ndani walipoachiwa huru wakataifishiwa mali zao
Nchi za Magharibi na Mashirika ya fedha ya kimataifa IMF na Banki ya Dunia yakaiwekea vikwazo Tanzania na kunyimwa misaada hali ya kiuchumi ikazidi kuwa ngumu
Laiti kama Kennedy asingeuawa pengine Mwalimu Nyerere angefuata siasa za kiliberali za Magharibi ingekuwa Tanzania inamaendeleo makubwa ya kiviwanda kama jirani zao Kenya ambao tangu wapate uhuru wao siasa zao ni za kibepari
Baadaye Mwalimu Nyerere aliona siasa zake za ujamaa na kujitemea na itikadi yake ya Azimio la Arusha vimeshindwa kukwamua hali ya chumi wa Tanzania akaamuua kung'atuka na kuachia ngazi akampisha Rais Ally Hassan Mwinyi
Rais Mwinyi alipoingia madarakani haraka sana akatengua Pole pole siasa za ujamaa na kuingiza siasa za kibepari kuruhusu uwekezazi, ubinafishaji na ushiriki wa sekta binafsi kwenye kuchechemua uchumi wa nchi
Baadaye rais Mwinyi akapewa jina la mzee Ruksa akaenda mbali zaidi na kuanzisha Azimio la Zanzibar ambalo kimsingi limelifuta azimio la Arusha la Mwalimu Nyerere
Nisiwachoshe, Kesho nitaendelea kuwaletea siasa za Mwalimu zilivyogonga mwamba na kudidimiza uchumi wa nchi hii nitaendelea kuonyesha sehemu ambazo Mwalimu amefeli na sehemuambazo amefanikiwa
Comasa