DIZZO MTAWALA

JF-Expert Member
Aug 22, 2015
240
767
Awamu ya sita na mwendelezo wa awamu ya tano ya mwendazake imefika “shingoni” mwa mwenyekiti FREEMAN AIKAELI MBOWE.

Mashtaka ya kigaidi aliyopewa jana ni mwendelezo wa vitendo vya kikandamizaji dhidi ya viongozi na wanachama wa upinzani hususani CHADEMA leo Tanzania mahabusu wengi wamesambaa wanaotokana na upinzani; karibu kila gereza Tanzania na kichaka wanachotumia ni sheria hii ya uhujumu uchumi

Serikali ya CCM inaamini ikimnyo’ngonyesha Mbowe CHADEMA itafubaa au kupotea kabisa. Hizi ni fikiria ya karne ya 18 Mwendazake alitumia kila mbinu za kufilisi biashara ya mbowe bado cdm haikutetereka sanasana ilibidi wapore uchaguzi wa 2019 serikali za mitaa na uchaguzi mkuu 2020

Rais samia baada ya pumzi kukata sasa karudi kwenye mafaili ya mwendazake kumdhibiti Mbowe na CHADEMA kwa ujumla sasa ugaidi ndio silaha yao ya mwisho na kwa cdm sio geni JK alitumia mbinu kupitia mwigulu kwa kumkamata mkurugenzi mkuu usalama ndani ya cdm mh lwakatare lakini walifeli.

Walimrushia Mbowe mabomu kwenye mkutano wake arusha napo walifeli leo Rais samia anatumia mbinu zilezile zilizofeli.

Japo ni maumivu kwa mbowe na cdm lakini faida kwa Taifa naaamini huu ndio mwelekeo wa kupata katiba mpya na ccm watakuja mezani wakiwa hoi bin taabani

CHADEMA ina watu CCM ina vyombo

Alamsk
 
Back
Top Bottom