FIFA yamuidhinisha Okwi kuichezea Young African

FIFA yamuidhinisha Okwi kuichezea Young African

Mimi siahidi lolote kupinga au kuunga mkono utabiri huo, kwani soka ni mchezo wa ajabu, unaweza ukaiweka timu ktk kambi ya sh. mil 500 bado ukaja kufungwa 5-0. Wewe unaahidi nini matokeo yasipokuwa hivyo?

Umesema uko bize bado unafanya nini hapa? Umehoji eti tunafanyaga kazi saa ngapi utafikiri tunakulaga kwako, log out uende zako bana.
 
Hivi wakati Yanga inapigwa 3 na Mnyama mkali Okwi hakuwepo? Kuwafunga Wakojani sijui Wangazija wale ambao kazi yao ni uvuvi tu sio sawa na kuwafunga Wamisri au Simba SC.

Ukiwauliza Wamisri ni timu gani Tanzania bado wanaikumbuka kwa Umafia waliofanyiwa 2003 tena kwenye uwanja wao wa nyumbani watakujibu hawataki hata kusikia jina la Simba SC. Hahahaaaaaaaaaaaaaaa....pana chezea mzee wa kupiga njano 5 veve heeeee....hata Obama na ile rais staafu naitwa Bush najua.

Mbona unatoka nje ya mada?
 
Hapa Rage itabidi akakate rufaa kwenye kamati ya 'oparesheni bunju',haiwezekani OKWI achezee yanga.
 
1. Dida / Barthez
2. Juma Abdul
3. Oscar Joshua
4. Rajab Zahir
5. Reliants Lusajo
6. Athuman Idd Chuji
7. Simon Msuva
8. Hassan Dilunga
9. Jerson Tegete
10. Said Bahanunzi
11. Hamis Kiiza

Hapo bado sijamuweka Nizar na Hamis Thabit
du yanga wana timu mbili!
 
Hiki ndicho kikosi cha kuwatoa waarabu koko wa misri.
1.Juma K Juma
2.Mbuyu Twite
3.Oscar Joshua
4.Nadri Cannavaro
5.Kelvin Yondani
6.Frank Domayo
7.Mrisho Ngassa
8.Haruna Niyonzima
9.Didier Kavumbagu
10.Emanuel Okwi
11.David Luhende

Benchi...........

1. Dida / Barthez
2. Juma Abdul
3. Oscar Joshua
4. Rajab Zahir
5. Reliants Lusajo
6. Athuman Idd Chuji
7. Simon Msuva
8. Hassan Dilunga
9. Jerson Tegete
10. Said Bahanunzi
11. Hamis Kiiza

Hapo bado sijamuweka Nizar na Hamis Thabit

kumbe tuna timu mbili ndani ya 1
 
SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA) limemuidhinisha mshambuliaji Mganda, Emmanuel Arnold Okwi kuchezea klabu ya Yanga ya Dar es Salaam.

Katibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Celestine Mwesigwa amesema muda huu kwamba, FIFA imewaandikia barua ikiwaambia Okwi ni halali kuchezea Yanga SC.

“Suala la Okwi limekwisha, ila siwezi kuzungumza zaidi kwa sasa naingia kwenye kikao, tutatuma taarifa kwa vyombo vya habari baadaye,”alisema Mwesigwa.-

kwa TFF ya sasa hakuna jambo la Yanga litakalokwama
 
kumbe tuna timu mbili ndani ya 1
Mbona sio kitu cha ajabu jamani, mnataka watu watucheke kwamba hatujui hesabu? Kama timu imesajili wachezaji 30, na uwanjani wanaingia wachezaji 11, ukigawanya hapo 30 ÷ 11 = 2 baki 8, kulikuwa kuna haja ya kushangaa kwamba timu ina vikosi viwili?
 
niliwahi kuwa shabiki sana wa soka la bongo,ila nilikuja kuachana kabisa na ushabiki wa kijinga wa yanga na simba baada ya kujitambua,klabu zinaendeshwa kiswahili mno hizi na hakuna kabisa professionalism,siku hzi hata siku simba na yanga zikicheza mechi huwa sina habari kabisa,

Sasa huo ni unafiki mkubwa tena uliopitiliza, sasa humu umefikaje kwan hukuona thread nyingine? Nin kilichokuvutia hadi ukafungua hii post kama huwa hauna habari na soka la bongo? Na je kwan nilazima kushabikia simba na yanga as if bongo kuna timu mbili tu au umeandika uonekane we ni mstaarab na kwamba wengine wote waliobakia humu ni makazuzu..acha u**f**la..shame on you
 
Umesema uko bize bado unafanya nini hapa? Umehoji eti tunafanyaga kazi saa ngapi utafikiri tunakulaga kwako, log out uende zako bana.
Aende wapi tena wakati hapo alipo anatumia "wireless connection" popote alipo jukwaa kama kawa?
 
Jinsi watu wanavyoweka post zao humu, sipati shaka kabisa nikiambiwa kwamba hawa ni miongoni mwa wale wanaodondoka uwanjani mambo yakienda kombo. Hivi mtu mzima unakaa unashupalia jambo as if you don't have something to do at your office/home? Mnafanya kazi saa ngapi? Wengine tunaingiaga humu tukichoka kutype codes, lakini ajabu unakuta mtu ameanzisha thread saa kumi na moja alfajiri (5.00am) na ameendelea kuchangia hadi usiku! Mmmh, kweli soccer ni dini mpya! Tena nikiingia humu naweka post tatu nne za kuwaudhi watu, halafu nalog-out

Mkuu grafani11 umeona madongo ya huyu jamaa? Hatujawahi kwendaga kwake kudai ugali, tunajilisha wenyewe, asitubabaishe bana. Kama mada haipendi akae kimya.
 
Last edited by a moderator:
Rage mtt wa kitaa kaishapiga hela na kamzubaisha Hans na wana simba kwa rufaa feki ya fifa. Ah!! Rage kitu ingine , kimbembe ni kuitisha mkutano wa wanachama hapo tusahau na ukiitishwa kasha nunua mamluki wakutetea hoja zake.
 
Hata Simba walisema wataifunga Mgambo Shooting, kilichotokea tunajua wote. Mlisema kamwe Okwi hatacheza Yanga, sasa karuhusiwa. Hans papa alisema Okwi atacheza Mtani Jembe pekee, sasa atakipiga kwenye ligi hadi CAF. Kwa mara nyingine Rage et al. wameaibika tena; hiki ndicho kiini cha furaha yetu! Yanga oyee na Simba zii.
Hakuna cha kushangaza kwa TFFYANGA hii, na bado mengi ya ajabu tutayaona kwa nguvu ya pesa ya G@bacholi fisadi la EPA.

Ametumia pesa nyingi sana kuhalalisha uongozi wake ndani ya Yanga "at least" akubalike na awasahaulishe vipigo vya aibu Yanga inavyopata kutoka kwa Simba SC katika kipindi cha Uongozi wake. Ametangaza kujiuzulu mwaka huu si kwa kupenda ameona hasara anayoipata kiuchumi ni kubwa kuliko faida. Ngoja aondoke kama mtaendelea kuhonga hadi FIFA tena.
 
Mkuu grafani11 umeona madongo ya huyu jamaa? Hatujawahi kwendaga kwake kudai ugali, tunajilisha wenyewe, asitubabaishe bana. Kama mada haipendi akae kimya.
Utani wa jadi hauwezi huyu, tumsamehe bure. Hawa ndiyo wale wale Wakenya wanaoua shabiki wa timu pinzani timu zao zikifungwa. Shekhe acha sisi tuendelee...
 
Back
Top Bottom