Kwa kweli hapa Mhe. Sugu amechemka, na walio karibu nae basi wajaribu kumshauri asifanye maamuzi ambayo yataonekana kama ni ya kidikteta, issue kama hii itamfanya aonekane yuko out of touch na vijana, ambao akumbuke ndio margin kubwa ya wapiga kura ifikapo 2015.
Tufahamu walengwa wa Fiesta ni vijana na wengi ni wa rika la miaka 15-22 na kwa mtazamo wangu nadhani dhumuni la tamasha kama hili ni kuwaburudisha (entertain) vijana, ni nafasi yao pekee kuwaona ma-Idols wao jukwaa moja kwa kiingilio rahisi.
Vijana wa Mbeya nao wana haki kama vijana wenzao nchini kwetu ya kuwaona wanamuziki wao wanaowapenda na sio sahihi kuwanyima haki yao hii.
Hivi mfano yeye Sugu ndio mmoja wa wasanii kwenye hii Fiesta mfano Mwana FA ama FidQ angejisikia vipi kama wapenzi wake wa Mbeya waliojiandaa kumuona wameshindwa, kisa Mbunge kaleta kauzu?
Naelewa wazazi walio wengi watampa sapoti kwa sababu kwa jicho la mzazi vijana wao bado wako vulnerable katika mikusanyiko kama hii, lakini hii isiwe ndio sababu ya vijana kukosa haki zao kufurahi, la msingi ni kila mzazi kumpa darasa kijana wake, na hawa waandaaji wa matamasha na wasanii wajitahidi kutoa elimu na ujumbe katika hii mikusanyiko.
Zama hizi za utandawazi, vijana wengi wa leo wanawasikiliza zaidi ma-Idols wao kushinda wazee wao. Huo ndio ukweli wa kusikitisha.
Mr. Sugu ajue asilimia kubwa ya wapiga kura 2015 ndio hao anaowakataza wasione Fiesta, anatakiwa ajenge ukaribu nao zaidi na sio kuwapeperusha. Akiendelea na mwendo huu asahau kipindi cha pili.