Fidia. . . | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fidia. . .

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Lizzy, Jan 24, 2012.

 1. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #1
  Jan 24, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Siku hizi wengi wanaingia kwenye mapenzi kwa sababu ya pesa, maumbo ama sura nzuri. Waoamini mapenzi bila pesa nao wanaongezeka kila siku kutokana na hali halisi hivyo siwezi kuwalaumu japo sikubaliani nao. Nnachojua mimi ni kwamba mapenzi hayanunuliki, kinachonunulika ni mahusiano.

  Nwy nilikua nafikiria jinsi gani hivi vitu vitatu (pesa, sura na umbo) vinavyosababisha watu wasizingatie vitu ambavyo ndio misingi ya kuendesha mahusiano yenye faida kwa pande zote.

  Kwasababu wanaume (sio wote) wanaamini kwamba mapenzi yananunulika, kishawishi wanachotumia kuwakamata wanawake ni pesa. Na wanawake wanatumia sura na maumbo yao.Pesa inatumika kufidia mambo ambayo ni ya msingi. Vile vitu vyote ambavyo havinunuliwi kwa pesa, na vinachukua muda mrefu sana kuwa navyo hawana.

  Mtu
  Anakosa uaminifu, heshima, uelewa, utayari wa kumsikiliza mwenzake, muda wa kuwa na mwenzake, mapenzi, kumjali kihisia na kimwili, kuona umuhimu wa mwenzi wake, anamnyanyasa mwenzake kimwili/kihisia na kifikra, hajishughulishi jikoni, sebleni wala chumbani (kwa wamama zaidi. . kila kitu dada wa kazi), anakua na dharau, anamtumia mume kifedha/kimwili, anamdharau mwenzake na kufidia hayo yote kwa kuwa na PESA, UMBO ama SURA NZURI.

  Yani kwenye jamii yetu kumpata mwenye pesa ni rahisi kuliko kumpata mtu ambae ana"strong values" "good morals" na ni "well mannered". Na ukisema unatafuta mwenzi wa aina hiyo watu watakushangaa kuliko ukisema unatafuta mtu wa kumchuna a.k.a ATM , tena zinazotembea. . lolz.

  Swali : WEWE ukiambiwa uchague kati ya 'sura nzuri, pesa, umbo la kupindisha shingo za wake kwa waume' na ' stong values, good manners, good morals' utachagua kipi?
   
 2. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #2
  Jan 24, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Good values, good morals.
  Nina wasi wasi wengi watasema hivi sababu sio rahisi kusema kua utachagua pesa, umbo na sura.
  Ukweli ni kwamba mtu huwezi kuvutiwa ghafla na mwanaume maskini, mwenye umbo na sura baya. Labda mlikutana internet na umesha ziona values zake?
  Ila ukifikiria sustainability, relation haiwezi kujengeka kwa kufata hayo tu. lazima na values zichunguzwe.
   
 3. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #3
  Jan 24, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Mi ntachagua SGGs..the latter..strong values,good manners,good morals Lizzy.. Ila upatikanaji sasa ndo kimbembe..
   
 4. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #4
  Jan 24, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Sio lazima uvutiwe na mtu siku ya kwanza mnaonana. Labda uniambie hata kuwa rafiki na mtu ambae hakuvutii kisura na asiye na pesa kwako ni mwiko. Kama sio mwiko basi ndani ya urafiki wenu ndio utajua ni mtu wa aina gani, sio lazima mkutane kama vivuli.
   
 5. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #5
  Jan 24, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Upatikanaji ni kimbembe kwasababu watu hawaoni umuhimu wa kuwa nayo wakati wengi wanakamatika kwa yale yanayopatikana kirahisi na SGGs ni ghali.
   
 6. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #6
  Jan 24, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  sura nzuri, pesa, na ' stong values, good manners, good morals'.....a little bit of both to be honest....!

  ila morals na good manners come first especially kama namuwazia kuwa mume na baba watoto wangu!
   
 7. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #7
  Jan 24, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Mi nimesha sema kwanza kabisa ni values, morals na maners. maana hata mtu wa pesa, umbo na uso akikosa hivyo vitu sioni atakuaje rafiki au mpenzi wangu. Hata sipati picha. Ila pia kama mtu ni mbaya wa uso itachukua muda kidogo kabla ya kuanza kufikiria kua tunaweza kua wapenzi. nitampenda kama rafiki. with bidii yake and time spent together - longer time and more effort kuliko yule mzuri wa sura na umbo- naweza kuja kumpenda. hayo ya pesa yanakuja mwisho.
   
 8. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #8
  Jan 24, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,807
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  mie pesa kwanza sura last lol,tena pesa sio ulizonazo sasa hivi bali kama una mipango endelevu ya kuwa nazo lol...wanangu wasije wakateseka na uhandsome wako!!!lol
   
 9. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #9
  Jan 24, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mpaka hapo inawezekana ukamjua/fahamu mtu kiundani bila kujali muonekano wake na mfuko una kiasi gani uraiani, na sio lazima kila mmoja awe amejificha nyuma ya PC. Tuko pamoja.
   
 10. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #10
  Jan 24, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  In the end that's what we really need. . ila sasa vipaumbele ndio tatizo.
   
 11. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #11
  Jan 24, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Akiwa na pesa + mipango ya maana, mkaoana alafu baadae mambo yakaenda mrama utafanyaje?
   
 12. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #12
  Jan 24, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  Same here...lol....usiku mwema Mwali, see you....niagie Lizzy,mwambie naenda enforce good morals....!
   
 13. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #13
  Jan 24, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  So far, pamoja kabisa. nadhani nimekusoma sasa.
   
 14. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #14
  Jan 24, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Huyo hapo anakusoma. Good night Sissy, and be good. lol
   
 15. Ziltan

  Ziltan JF-Expert Member

  #15
  Jan 24, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 1,350
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Haya mambo tumeyakuta na ingawa hatulazimishwi kuyashiriki,ila zaidi hayakwepeki,
  mie kwa upande wangu nnachukua sura nzuri,umbo na pesa,kwani hata ktk maandiko wanavikubali hiv vitu na ni kama baraka,
  watu hawaaminiki awe ni mtu ambaye mzuri au mbaya, zaid ni kujipanga tu bila kumtegemea mtu,ikitokea sawa,
   
 16. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #16
  Jan 24, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Sura, umbo na pesa ndivyo vinavyoaminika? Vikiyeyuka unafanyaje?
   
 17. m

  mzabzab JF-Expert Member

  #17
  Jan 24, 2012
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 6,981
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  mie nataka special one ambaye ana vyote hapo juu coz my mum told me wanake wenye vyote wapo
   
 18. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #18
  Jan 24, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mimi ntachagua yote.
   
 19. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #19
  Jan 24, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Naona hapo kwenye red inatofautiana kutoka eneo moja hadi jingine
  Hapa kuna western morals and values na african morals and values.

  Nitachagua mwanamme mwenye african morals and values kuliko hivyo vingine.

   
 20. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #20
  Jan 24, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Mi bora niseme shared morals and values kati yake na mimi
  sababu sometimes kuna uonevu fulani wanajiwekea tu chini ya umbrela ya African values.
  vile vile sometimes kuna ujinga fulani wanaweka chini ya umbrella ya modernity and open mindness.
  sasa mwenyewe nimejichagulia zile zinazo nifaa kwa kua na msimamo wa maisha ambao nina kubaliana nao mimi binafsi,
  pia unakubaliwa na wengi kua mzuri na unao nipa heshima kwa watu ninao wajali.
   
Loading...