Hii ni huzuni kwa Bongo Flava hadi Fid Q na Alikiba nao wameingia mkenge?

NEGAN

JF-Expert Member
May 12, 2023
648
1,446
Hivi kama wakereketwa wa Bongo Flava tumeshindwa kabisa kuiweka bongo flava kwenye ramani ya mziki Africa? Maana hii movement ya Amapiano bongo imekuja kuimalizia kabisa bongo fleva na kuizika kabisa.

Alianza Diamond kuikatia tamaa bongo fleva,wakaja akina Nandy,Marioo, Mtaalam Jux naye kafuata upepo, Harmonize nae katembea na upepo wa Amapiano.

Kinachonisikitisha Alikiba alisema hawezi imba Amapiano ila na yeye kaunga mkono movement. Mkali na icon ya Hip hop Fid q naye kaunga mkono movement kageuka na kuwa Ngosha Wana man.

Ni huzuni kubwa kuiona bongo fleva inaangamia.
IMG_20230714_124358.jpg
 
Hivu kama wakereketwa wa Bongo Flava tumeshindwa kabisa kuiweka bongo flava kwenye ramani ya mziki Africa? Maana hii movement ya Amapiano bongo imekuja kuimalizia kabisa bongo fleva na kuizika kabisa.

Alianza Diamond kuikatia tamaa bongo fleva,wakaja akina Nandy,Marioo, Mtaalam Jux naye kafuata upepo, Harmonize nae katembea na upepo wa Amapiano.

Kinachonisikitisha Alikiba alisema hawezi imba Amapiano ila na yeye kaunga mkono movement. Mkali na icon ya Hip hop Fid q naye kaunga mkono movement kageuka na kuwa Ngosha Wana man.

Ni huzuni kubwa kuiona bongo fleva inaangamia.
View attachment 2687699
Video ipo wapi
 
Wabongo kujikuta mnajua kupenda mziki wenu wakati hao kina fid q wakiimba hardcore hamnunui Album ,, watu wanatafuta pesa.
Identify inapotea mkuu Diamond alikua kwenye right track mwanzoni wa miaka ya 2010 anakimbizana na akina Wizkid na Davido kwenye tuzo kubwa anakua nominated na pesa alikua anapiga vizuri tu ila recently kabadili uelekeo.
 
Mbona Nigeria wamekomaa na mziki wao wanapambana na wasouth
Hayo mataifa kwa idadi na uchumi yako juu so wanajitosheleza, wanaweza kuimba chao na wakapata chao.

Mashabiki wanafuatilia vitu vya mataifa makubwa ili mwanamuziki atoboe lazima aimbe kama wao.

Mwanamuziki wa SA au Nigeria aimbe bongo fleva avune nini? Mbongo fleva ndo anaimba kisouth au kinigeria angalau apewe sikio na dunia
 
Wale mawe wakiimba bongo fleva au mtawapa kande. Hakuna kazi ya kabisa au ya jamii kwenye uwekezaji wa sanaa na matunda yake
 
Tatizo la bongo fleva ni R&B na hiphop, yote ni miziki ya kuiga tu. Labda ungeuliza kuhusu singeli kidogo na mziki wa pwani/taarabu.
Umeongea kitu kikubwa sana. Muziki ni utamaduni. Muziki lazima uwe na vionjo vya kitamaduni. Hip Hop ni ya mtu mweusi popote alipo. Rock ni ya weupe. Hata kama. Sisi tungestic na singeli. Unajua shoo ya Fid Ujerumani na Shoo ya Jagwa ujerumani ipo ilifana kiasili?
 
Wale mawe wakiimba bongo fleva au mtawapa kande. Hakuna kazi ya kabisa au ya jamii kwenye uwekezaji wa sanaa na matunda yake
Huu ukweli mchungu lakini Diamond alikua kwenye right track sijui nini kilimkumba
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom