Ingawa mambo mengi yamechanganywa humu kuanzia uarabini,uingereza na pia bado exel auliza kuhusu utofauti wa maisha baina ya UK na US, hebu niongelee kuhusu falme za kiarabu ambazo ni sita tu Saudia, UAE, Kuwait, Bahrain, Qatar na Oman.
Wafanyakazi wengi wa ndani na madereva wa familia wanatoka India, Sri Lanka ,Philippines, na far east kwa ujumla lakini wengi wa kutoka Philippines ni wataalamu huwa wanachukuliwa kama nurse,
Unapokwenda huko unakuwa na sponser wako ambapo utakaa kwa miaka miwili au zaidi inategemea na permit, na mshahara ni mdogo kwani unakula na kulala kwake kazi zote utafanya kama ni safari utaenda nao,
Hayo ni Arab world ,
Sasa hao wamepitia maisha hayo magumu na kuamuwa kuwaachia nyie na nyie mkaja shtuka baada ya miaka 50 tough!
Kwa $125 kwa mwezi sina uhakika maana nakumbuka miaka ya nyuma sana walikuwa wanapata $100 that's almost 30 yrs ago,
Uongo unakuja kwa madalali kuwahadaa watu,kama ukiambiwa maisha mazuri chakula bure pa kulala bure na mshahara laki 2 nafikiri wengi wenu mtakurupuka na kwenda
Lakini mkae mkijua mlo pekee ni elfu 8
Ok haya ya UK ni mengine huko nako kwa mshahara wa kiwango cha chini huwezi kula burger kila siku kwani ni £4 sasa
una familia unaenda kula MacDonald umebaki na nini? Maisha ni ghali sana kwani unalipa kachumba £100 (260,000) kwa wiki bado bills,chakula,petrol,insurance,na mengine mengi sasa niambie hata £10 SAA bado unapumulia mrija yaani ni maskini tu
Nafikiri utafiti wako nimeutosheleza ingawa ni mengi ya kueleza, lakini mada ni Arab world,