isije kuwa huyo dada chakula ya bosi. vipi lakini gharama za maisha maana hiyo hela ilivyoletwa kwenye tsh imeonekana ndefu sana kwa hg lakini si ajabu kwa maisha ya huko utaishia kununua chakula tu cha mwezi.
@Husniyo,
Arabuni hasa Oman, kwa vile wanaoagiza hao dada wa nyumbani wengi wao ni wenyeji wa Tanzania, Kenya, Uganda, Congo na Ruwanda na Burundi. Hivyo basi mazingira ya uhusiano wao baina ya Dada na Bosi (Mama wa nyumba) hasa wa Tanzania hayana tofauti na huku nyumbani.
Mara nyingi wanaishi kama ndugu, wanatakiwa wawe weledi wa kazi zao, na wawe wasafi kimwili na katika kitunza mazingira ya ndani ya nyumba. Kuwa Muislam na kujuwa Kiingereza au Kiarabu or any of the three is an added value.
Kazi ni kusafisha nyumba ndani na nje, kufua nguo kwa automatic machines, kusaidia kupika au kupika na kazi za jikoni.
Wengine hutakiwa ulezi wa mtoto tu au kusaidia kizee cha nyumbani kama vile kufuatana nae katika mazoezi ya kutembea, kumtandikia kitanda, kumtayarishia.chakula chake maalum hata kumsimamia.msalani kwa wale vizee wagonjwa.
Wengine hata kumwagia maji bustani.
Wengine dereva wa kupeleka watoto shule na mama sokoni.
Mambo anayopata free:
Malazi mazuri sana chumba chake mwenyewe, self contained with A/C.
Chakula ndio hicho hicho kitakachopikwa na ikiwa mfano anataka kupika cha kwake mwenyewe mfano Ugali.
Matibabu na gaharama zake ni juu ya mwajiri wake. Mara nyingi hufunguliwa Life Insurance account ikawa analipiwa na Insurance firm.
Mara akifika tu hupewa induction na pia kusaidiwa nguo na hata kupewa simu kama hana.
Kwa hivyo mshahara wake ni.safi tax free.
Asiyotakiwa kufanya:
1. Umbea, ikiwamo kuwa asishiriki maongezi ya wanafamilia wala kuchonganisha.
2. Kuvaa nguo sisizo staha kama vimini na vitop. Anatakiwa asionekane, makwapa yake na kifua wazi au kitovu wala sehem za mwili wake sehemu zengine zinazoleta uchokozi.
3. Uzinzi wa ndani na nje, ulevi, na kudandia baba au watoto wake. Hili litamwondoa na kumrudisha nyumbani Bongo siku ifuatayo.
Hata hivyo mambo yote hayo yamo kwenye mkataba ambao unasimamiwa na Ubalozi wa Tanzania. Kama huna huo mkataba huoni ndani ya ndege katika.viwanjavyetu JKNIA, AAKIA znz.
Muwe na hadhari kuhusu maeneo ya kazi. Maagenti wengine hawasemi ukweli. Msikubali kupelekwa kufanya kazi nje Mji Mkuu wa Muscat. Ombeni mhakikishiwe kama mwajiri wenu yuko mji mkuu au at least awe ana asili ya huku kwetu.
Msikubali kufanya kazi kwenye nyumba za wasio ongea Kiswahili na wenye watoto wengi wadogo.
Mishahara nayo inategemea mabosi wenyewe huwa inatofautiana na kazi zenyewe lakini si chini ya 200,000.