Feedback kutoka arabuni...

Feedback kutoka arabuni...

ahsante sana mkuu Averoes kwa maelezo mazuri... stay blessed please..
 
Last edited by a moderator:
ahsante Averoes kwa ufafanuzi mzuri. vipi gharama za maisha lakini. kwa mfanyakazi anaepokea tsh 200000 huko uarabuni anaweza kumudu maisha kama anajitegemea mwenyewe?

mkuu mbona unadadisi sana? wataka kwenda kula tende?
 
Huko ni ubaguzi na udhalilishaji kamwe msijejidanganya

mkuu nadhani hayo yamepungua sana siku hizi.. kama yangekuwapo basi sidhani kama yangelikuwa kimya mpaka sasa..

ahsante kwa mchango mkuu..
 
mkuu mbona unaongea kwa kashfa namna hiyo? laki mbili kwa mwaka si ni sawa na tshs 17000 tu kwa mwezi?

sasa nani yuko tayari kufanya hio kazi?

tafadhali sana usipindishe kauli..

Usinielewe vibaya tu mkuu, kule hawaitwi wafanyakazi wanaitwa "watumwa" na mila za kiarabu zinaruhusu kutenda chochote mtumwa wako! wale watu wanafanyishwa kazi masaa ya kuzidi, hakuna kupumua na manyanyaso juu, sasa mshahara wa 200K hailipi, ni heri kulima matuta ya viazi hapahapa bongo!
 
Kweli tumefikia pabaya, kumbe wale mabinti wa TMK, mbunge wao anajidai anawatafutua kazi uarabuni na kwenye magazeti anatangazwa kwa mbwembwe kumbe wanaenda kufanya kazi za ndani, loh dada zangu chungeni sana, someni mjikwamue na mkwamue wenzenu. Unasifia uhausgeli wa uarabuni kisa laki 2!!? Shame on you

umepewa feedback mkuu, mbona unalalamika?

hivi ulishawahi hata kuulizia nini kinaendelea huko baada ya wao kwenda?

mbona sasa walia baada ya kupewa ukweli?
 
Usinielewe vibaya tu mkuu, kule hawaitwi wafanyakazi wanaitwa "watumwa" na mila za kiarabu zinaruhusu kutenda chochote mtumwa wako! wale watu wanafanyishwa kazi masaa ya kuzidi, hakuna kupumua na manyanyaso juu, sasa mshahara wa 200K hailipi, ni heri kulima matuta ya viazi hapahapa bongo!

mkuu ntafuatilia kiundani hilo suala.. ila kama ukweli ndio huo, kwanini serikali ya kijani imekalia kimya suala nyeti kama hii?

kama kweli utumwa upo, kwanini hao waendao huko hawalalamiki?
 
Hapana, labda uwe na bahati ya mtende kupata tajiri mzuri. Hawa watu ni wabaguzi na wanawa-treat wafanyakazi wao kama watumwa vile. Nilipata maelezo kutoka kwa dada mmoja wa Kenya aliyelazimika kutoroka kutoka kwa bosi kutokana na matatizo kibao kufanyishwa kazi muda mrefu bila kupumzika, no likizo, chakula cha watoto wa boss na uchafu mwingine kibao. Kibaya zaidi ukifika huko unanyangwa pass ya kusafiria na hivyo hata wakunyanyase vipi huwezi kuondoka kwao.

Kwa kweli nisingewashauri wadogo zangu kwenda arabuni kufanya kazi za ndani, waarabu hawafai (Sitaki kuja kushambuliwa hapa, nimezungumzia waarabu, sijazungumzia dini yao).

Tiba

ahsante mkuu kwa maelezo mazuri.. sikujua kabisa kama haya mambo bado yapo..

pia sidhani kama kuna mtu atakayechanganya na dini... serikali inazungumzia nini kuhusu hili mkuu? kwanini kimya lakini?
 
mafanikio ya watu yana mambo mengi nyuma yake, usione watu wanaenda ng'ambo na kurudi ukakurupukia. hebu muhoji vizuri, mwenyewe nataka kwenda huko.

mkuu unataka kwenda kibiashara?
 
Matumizi ya UK ni bilaha vitu bei ghali ata misosi kwenye mgahawa. Hiyo laki 2 kwa siku wala uwezi kuishi vizuri London
Hapo bado kulipa bills na nyumba etc. Watu wako bize balaha

mkuu, samahani kwa usumbufu lakini, tukifananisha maisha ya UK na USA, wapi kuna ugumu?
 
ahsante mkuu kwa maelezo mazuri.. sikujua kabisa kama haya mambo bado yapo..

pia sidhani kama kuna mtu atakayechanganya na dini... serikali inazungumzia nini kuhusu hili mkuu? kwanini kimya lakini?

Mkuu serikali iseme nini wakati watu wanajipeleka utumwani wenyewe? Zamani waarabu walikuwa wanafunga safari kutufuata huku kwetu lakini sasa upepo umebadirika, sisi wenywe tunaangaika kutafuta nauli na visa na kujipeleka wenyewe utumwani.

ila Tiba sidhani kama serikali kukaa kimya ama kuwapa watu wake uhuru kiasi hiki ni sahihi..

mbona mataifa mengine yanawapigania watu wake? kwanini TANZANIA IKO HIVI?
 
Last edited by a moderator:
umepewa feedback mkuu, mbona unalalamika?

hivi ulishawahi hata kuulizia nini kinaendelea huko baada ya wao kwenda?

mbona sasa walia baada ya kupewa ukweli?

Aliekwambia nalia nani ndugu, fursa zote hizi tulizo nazo hapa nyumbani kuna haja gani ya likiongozi zima kuwataftia sistaz kazi ya ubeki tatu uarabini??? Kama anawajali si angewawezesha kiuchumi mfano wajikusanye vikundi awataftie ardhi mkuranga wakalima mboga mboga kwa ustadi tuna shopping malls na masoko pia, taratibu wangeeleshwa juu ya vikoba na saccos wakiwa wanazalisha shambani, after time na wao wangeajiri. Lakini uhouse girl, wamusomea VETA au? Ndugu? Tujipange
 
MKUU, aina ya uchumi iliyopo sasa ni free market.. nadhani unaelewa hilo!
ni mara ngapi watu wanaambiwa kilimo lakini wanagoma kufanya kazi?

hivi unadhani kilimo ni rahisi tu kama inavyotamkika? kwa wadada wa dar es salaam wanavyopenda simple life, nani atakaeenda kulima?
 
ila Tiba sidhani kama serikali kukaa kimya ama kuwapa watu wake uhuru kiasi hiki ni sahihi..

mbona mataifa mengine yanawapigania watu wake? kwanini TANZANIA IKO HIVI?

I beg to reserve my comments on this!!!! Bado nazipenda kucha zangu ati.

Tiba
 
MKUU, aina ya uchumi iliyopo sasa ni free market.. nadhani unaelewa hilo!
ni mara ngapi watu wanaambiwa kilimo lakini wanagoma kufanya kazi?

hivi unadhani kilimo ni rahisi tu kama inavyotamkika? kwa wadada wa dar es salaam wanavyopenda simple life, nani atakaeenda kulima?

Du! Mkuu Excel unadhani kule wanafanya kazi kwa masaa matano au nane kwa siku? Free market ndo nzuri fursa kwa wote kuzalisha kwa ubora na kupeleka mzigo sokoni, sio free market ya mahouse girl uarabuni. Wadada wa dar ndo nini, unadhani kusista duu ataenda huko au hata aliye na elimu yake?! nawasisi sana na,kiwango cha msomi aneenda kuwa mfanyakazi wa ndani huko??!!? Kila atakae wezeshwa ataweza tuu, karoti, matikiti maji, nyanya, mabiringanya na makabichi ya ajabu yale ya rangi ya zambarau unadhani zinachukua hata miezi mitano kukomaa na kuvunwa?!?! Ndugu kilimo hicho rahisi sana hatuwezeshwi, weka pambeni spinach, chiniz na mchicha, vipi ndugu!
 
Back
Top Bottom