Feedback hasa katika mazungumzo yanayolenga kutatua migogoro

Feedback hasa katika mazungumzo yanayolenga kutatua migogoro

bulajunior

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2024
Posts
624
Reaction score
895
Habari wadau tupo siku zinakwenda na tunazidi kutatua matatizo mengi ya kiuchumi kijamii kielemu na zaidi.

Kuna kitu ningependa tujadili na huenda kikatuongezea silaha zaidi za kupambana na challenge mbali mbali kwenye maisha yetu.

Kitu hiki ni feedback yaani mrejesho hasa wa mazungumzo tu kama nilivoandika kwenye title hapo, hii imekuwa ikutumaliza wengi tunajikuta tunapoteza watu muhimu kwenye maisha yetu hasa inapotokea tumekwazana yeah tunashindwa kuwasiliana vizuri na kutengeneza uaminifu tena.

Kumrudishia mrejesho mwenzio hasa Yule anaelalamika kuwa ulimkwaza ni jambo muhimu Sana kuliko kukaa kimya hiyo haifai Rudisha feedback na kubali kosa lako na haiwezekani eti mtu atakuonea tu mwanzo mwisho kwenye malalamiko yake lazima kuna vitu itakuwa kweli umekosea na katika vile muunge mkono na kumuahidi kutokurudia lkn pia inawezekana ametafsiri vibaya kitu akaanza kukulaumu basi kwa heshima tu mweleweshe na usimbishie ili usimkwaze zaidi hapo tutakuwa na mwendelezo mzuri wa uhusiono wetu wa aina yoyote.

Kama ni ndoa tutazidi kuwa pamoja tutalea watoto wetu kwa pamoja na kwa furaha wala hatutakuwa na watoto wa kulelewa na mzazi mmoja kwa kigezo cha kutengana kisa migogoro. Asanteni sana 🙏🙏🙏🙏
 
Back
Top Bottom