Fedha...

nikipewa nyingi na Boflo namuona booonge la mwanaume,akinipa kidogo namwona kachala!
 
Last edited by a moderator:
mpirani/kwenye burudani huitwa kiingilio
 
Marupurupu, mafao, kiinua mgongo, mshahara, noma,
 

Boflo...sometimes you amaze me with the way you think...ukienda kununua dada poa inaitwaje tena?
 

Hapana kiongozi me nitatofautiana na wewe hapo umetafafasiri matumizi ya neno pesa linabadilika kutokana na mazingira ila haujatueleza pesa linamajina gani tofauti na neno lenyewe pesa mfano mzuri ni wa Nyani Ngabu hapo juu ametoa majina ya mtaani ni sahihi kbs na mimi nitakupa yangu km vile mavumba, njuruku na mengine mengi sana.
 
1.malipo kwa kuhudhuria kikao au semina=posho.
2. malipo kutokana na ajira=ujira,mshahara.
3. malipo ya adhabu=faini
4. Malipo ya kupanga nyumba/jengo=pango.
 
1 ikiwa ya tz inaitwa TSH
2 Ikiwa ya kenya KSH
3 Ikiwa ya marekani USD
4 Ikiwa ya Uingereza GBP
5 Ikiwa ya kiongozi wa tanzania lakini iko uswis inaitwaje?




Karamu hufanywa kwa ajili ya kicheko, Na divai huyafurahisha maisha; Na fedha huleta jawabu la mambo yote.
 

Kule uarabuni kumkomboa mtu na hukumu ya kifo inaitwa Dia
Kulipa ili uwachiwe huru Faini.

 
Ukimpa Kikwete ili akuruhusu ujenge hoteli yako Serengeti au kuchimba madini Tanzania na hata ikibidi kuzalisha umeme Tanzania ili ulete GIZA, inaitwa LOBBYING.

Ama kweli HONGO ina majina mengi: Rushwa, Hongo, Takrima, Lobbying.......

Ukilipwa baada ya kutumika kwa miaka kadhaa wanaita KIINUA MGONGO. Kuna ile inaitwa Kifutia machozi, inatokana na nini? Halafu kuna mafao ya uzeeni.... Lohhh!!!!
 
mi najua pesa, hela na fedha!!!


katika ngo inaitwa fund, grants,
benki inaitwa deposits, capital,
kwa simu credit, vocha

wengine wanaita sabuni ya roho!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…