Fedha a.k.a hela

KARIA

JF-Expert Member
Jan 15, 2011
717
472
Majina ya hii kitu yanabadilika kila idara! Mfano ukiitoa sehemu ya ibada inaitwa sadaka! Endelea........!
 
1 . Ukimpa polisi rushwa !
2. Ukitoa shule ada !
3. Ukimpa mkeo matumizi
4. Ukimpa hawara
hongo!
5. Ukipeleka Tanesco/idara ya maji bili .
6. Ukimpa mfanyakazi mshahara!
 
- Ukilipa nyumba kodi !
- Ukilipa TRA ushuru!
- Ukitoa Bonus bahshish
- Ukiwapa wasiojiweza wajikwamue itaitwa zaka.
- Ukiwalipa vibarua itaitwa ujira.
 
Ukirudishiwa dukani chenji
Ukiolea mke mahari
Ukimpa mbunge posho ya kikao
Ukiuza madini mrahaba
 
Back
Top Bottom