mkuu aleyn hapa kidogo na mimi nataka niingie unaposema pep ni kocha wa kawaida tu unamaanisha kwamba pep ndo hana kitu na hana mpya na hayo mataji aliyoshinda ni kwa ajili ya masupastaa alokua nao kama messi, xavi and iniesta . is ok hapa umesema eti ancelot unamkubali zaidi kuliko pep wakati anceloti huyo huyo ametimuliwa pale madrid na kama pep alikua anashinda mataji kwa ajili ya xavi . messi na iniesta mbona kocha kama tata martino alipokuja barca alimaliza season yote ya mwaka 2013/2014 bila hata kikombe cha mbuzi wakati palikua na xavi. messi . neymar na iniesta hapa utasema kua xavi alishapungua kasi mbona kaja lius enrique kaendeleza style ile ya barca ya tikitaka na xavi ndani na iniesta na uengezeko wa suarez na neymar kawatumia vizuri tumeona matunda yake big up kwa enrique na hapo utasema enrique sio kocha ila kapata wachezaji wazuri tu .
mourihno ma fan wa chelsea walimsifu sana na hata media za uk zikampamba sana kua ni bonge la kocha yoote kwa sababu kawaletea kombe la epl juzi tumeona walivyo muadhirisha ni kwa sababu tu ya matokeo mabaya . nataka nikuambiye tu mkuu hii ndo soka unapofanya vizuri ndipo utaambiwa wee ni bora ukiboronga huna kitu sasa wee jiulize huyu pep kila timu inamtaka kuanzia psg . cheslea . man u n.k. jiulize kama sio kocha mzuri kwanini wanamtaka mourinho mpaka leo hajapata kibarua pep anaachiya tawi anakamata tawi
-Tunaposema wa kawaida haina maana kwamba tunamuweka level moja na makocha akina Maximo. Ninasema wa kawaida kwa kile ambacho alichofanikiwa, huwezi kumuweka Pep level moja na akina Mourinho ama Anceloti unless kwamba mpira umeanza kushabikia 2008.
-Suala la Pep Guardiola kutakiwa na timu kubwa haimaanishi kwamba yeye ni bora, mpira ni biashara kubwa sana ambayo inalipa kuliko maelezo. Unaposikia mtu kama Messi mkataba mpya ambao ataingia atalipwa 1.2 Bilion za kitanzania kwa wiki basi ujue kwenye mpira kuna pesa nyingi sana. Unapoambiwa Cristiano Ronaldo anamiliki magali zaidi ya 20 ya kifahali basi tambua mpira ulipa. Unapoambiwa John Terry anamzidi kwa pesa Wazir wao Mkuu wa Uingereza basi tambua mpira ni biashara kubwa mno.
Kwa waliosoma Biashara kuna kitu kinaitwa Brand, Brand inasehemu kubwa sana ya kuincrease sales ktk biashara. Kwanini Pep ni Brand kubwa!?
1. Mashabiki wengi wanatambua Pep ni mtu wa mafanikio, kuja kwa Pep kunavuta attention kwa mashabiki kuifatilia Man City.
2. Pep ataleta soka la tofauti EPL, tangu EPL ianzishwe, sidhani kama kuna timu itacheza soka la kuvutia kama ambalo Pep atalipeleka EPL na ndo maana hata Abramovic alikiri kuwa anamtaka Pep ili aje alete soka la tofauti Chelsea, HAKUSEMA ILI ALETE MAKOMBE ILA ALISEMA ILI ALETE SOKA LENYE BURUDANI.
3. Man City wanatumaini kumpata Neymar au Messi kwa miaka ya hivi karibuni, kumchukua Pep wanaamini kutaleta matumaini ya kuwapata hao nyota. Ukitaka kuamini hili angalia Club zote ambazo zinawawinda Messi na Neymar zimetangaza dau juu ya Pep ila Man City ndo imeshinda hapa majuzi.
4. Wachezaji wataweka imani kwa Pep, wachezaji wa Man City lazima watamheshimu sana Pep. Unapokuwa na kocha mwenye jina kubwa huwa inapelekea kuwa na heshima kubwa ndani ya club pamoja na wachezaji kumheshimu kocha. Ukiwa na kocha ambaye anaonekana ana mafanikio wachezaji watacheza kwa umakini mkubwa uwanjani, timu ikiyumba itaonekana ni wao wachezaji na si kocha ila kocha akiwa akiishiwa mbinu au akiwa mbovu huwa tunaona hali ya uchezaji itakavyobadilika.
-Mafanikio aliyoyapata Pep pale Barca kwa asilimia kubwa yalichangiwa na mfumo pamoja na wachezaji hao watatu. Ule mfumo miaka ya 2009-2010 hususani Mourinho alivyoenda Madrid mfumo wa Barca ulipata shida sana. Na kama unakumbuka kipindi kile Barca alikuwa anasemwa sana kwamba anabebwa. Binafsi suala la Barca kubebwa nalipinga kiasi na nalikubali kiasi kwa miaka ile. Barca ilikuwa ikikutana na Madrid ilikuwa ikishinda kwa tabu sana tangu alipokuja Mourinho, Mourinho amechangia kiasi kikubwa sana kudhibiti mfumo wa Barca. Rejea 3-1 tulizopigwa Milan, style ya magoli yalivyopatikana na ndo tukawa tunafungwa hivyo hivyo na Madrid na timu zingine na mpaka leo Bayern anafungwa hivyo hivyo, walau Barca amejirekebisha.
-Sitaweza kusema hasa kwanini Tata kashindwa kubeba Makombe Barca ila nachodhani ni kwamba Geraldo Tata ni msimu wake wa kwanza pale Barca na sidhani kama alishawahi kufundisha Ulaya. Ila nikukumbushe tu kuwa Tata alikosa kombe la ligi ktk mechi ya mwishi kabisa ya Ligi pia alikosa kombe la Mfalme ktk fainali, so unaweza ukasema jamaa hakuwa na bahati tuu pia ilichangiwa na Barca kukosa namba 9. Kumbuka kipindi kile Messi alikuwa anacheza winga wa kulia huku namba 9 akicheza Cesc Fabregas na ndo maana msimu ulivyoisha akasajiliwa Suarez.
-Carlo Ancelot katimuliwa Madrid sababu tu ya utahira na sifa za kijinga za Perez, Carlo ni kocha mzuri na ni kocha mwenye CV kubwa sana kwa sasa sawasawa na Jose Mourinho na Sir Alex.