FBI ndani ya Tanzania, kazi ipo

FBI ndani ya Tanzania, kazi ipo

Usalama wa Taifa tunaulipa mishahara ya kazi gani? Tunashindwaje kukamata wa halifu wenyewe mpaka tuagize watu kutoka nje? Hawa watu kiusalama tunawaamini vipi?o Watanzania tunahitaji kufanya maamuzi ya haraka sana na siyo lazima 2015 hata sasa ikibidi tufanye hivyo, kwa hali hii nchi ulinzi ni zero... Aliyesema JK ni chaguo la mungu na alaaniwe milele... Tunawalipa kiasi gani cha fedha na zinatoka wapi? Wanakaa kwa siku ngapi? Taifa liwekwe wazi!

Wanafuatilia Zaidi watumishi wa umma, walevi , wapenda ngono, wanaonunua magari wakiwa kazini kwa mwaka mmoja na kutembea na vibastola huku mawilayani mkuu
 
Mkuu nikiwa kama raia wa tanzania sikubali hata mara moja kuhusiana na hili.hii siyo ishara nzuri ni bora vyombo vyetu vikafanya kazi ndo wakihitaji msaada ndo wawaite wenzetu.sikubali hata mara moja na nitakuwa wa mwisho kuamini kuwa vyombo vyetu vimeshindwa nina imani navyo sana.

Ila nadhani tuwe watu makini katika kuhakikisha maamuzi mengine ya kisiasa hayatuadhiri mustakabathi wa nchi yetu. Hii natolea mfano kwa wenzetu wa kenya wao walikataa mara nyingi hata kama ulibahatika kumsikiliza wagombee wa urais kwenye mdahalo walitaka kwanza wale watu waliopelekwa hague watendewe haki kenya na sio the hague. Lazima tuvipe kipaumbele vyombo vyetu kwanza ndo tukishindwa tuombee msaad. Tanzania nakupenda sana

Vyombo gani hivyo ambavyo bado unaimani navyo?
 
sasa wewe tuna vyombo gani vya dola hapa Tanzania vya kuchunguza jambo kama hili na wakati ukatili dhidi ya raia unafanywa na vyombo hivi hivi vya dola, Ameuawa Mwangosi ,padri kunusurika kifo hivi karibuni huko Zanzibar, kunusurika kifo Dr Ulimboka hata hivyo lengo lao ilikuwa si kumtesa bali kuua kabisa lakini mungu akawa upande wa Ulimboka zaidi, Mauaji ya raia 3 wasiokuwa na hatia Arusha, Raia 1 asiyekuwa na hatia Morogoro aliuawa na polisi zaidi ya hayo uchunguzi wa polisi ukaripoti aliangukiwa na kitu chenye ncha kali, sasa leo tuwape kazi ya kuchunguza mauji wanayoyafanya wao?

Hata kama unapinga FBI wasifike hapa ni sawa lakini Bora tujilinde sisi wenyewe kuliko kuendelea na SINEMA ZINAZOCHEZWA NA POLISI-SISIEMU YA TANZANIA, Kilichobaki Tanzania ni kuanza kujilinda kitemi kama akina Mirambo, Isike, Mkwawa,Rumanyika na wengine kwani hata wakati huo ulinzi wa nchi na raia wake ulikuwa fresh tu kuliko sasa tunavyotembezewa kichapo na haya MARUHANI haya yanavyotufanyia, kwani raia hawana kabisa raha na nchi yao
ndg yangu ukweli ndio huo kama wewe bado unaendelea kuliamini hili jeshi la hapa Tanzania basi utakuwa una maslahi nalo wewe binafsi kwani sisi ndg zako, jamaa zako, watoto wako tumechoka
 
Mkuu,hawa wa kwelu hawakawii kukwambia tumemkamati alipoenda kutubu au kuungama dhami zake kwa mchungaji.Je hapo utaridhika?
 
Usalama wa taifa wa tanzania wanafanya nini?hii nchi dhaifu kweli.
 
mkuu kama niko sawa and i stand to be corrected kuna issue inaitwa state soveregnity. na pili ingekuwa bora hizi statement za kuomba msaada zitoke kwa watawala wenyewe na sio kwa political figures

Nielimishe nani ni mtawala na nani ni political figure? JK ndo kasema hayo, unajua siku hizi kufa kufaana na usikute haya mambo yote ni dili za JK. Maana Jk na Americans wanampenda kwa sababu ni loop hole kwao, usikute kila kitu kilipangwa na wanakuja kuchunguza mambo mengi sana ila sisi tumefunikwa na hilo moja.
 
Tunalisubiri hili gazeti la mwanchi liombe radhi baada ya huu utumbo
 
Jamani watanzania hatuna jema,wangesema watafanya UWT na polisi tungekuja juu na kusema hatuna imani nao.Wamewaleta tunaofikiri wanauwezao,nguvu na technologia ya kisasa tunailaumu serikali kwa nini wamewaita,hebu tujiulize tunaopenda kulalamika tunataka serikali ifanyeje?
 
Yaaani tunashindwa kumkamata hata muuaji hadi tuite FBI?? Kwani ule "mkono mrefu wa serikali" ulikatika? au sikuhizi umepooza au umepata kiharusi? au ni mrefu tu kwa wanachadema??? Hahahahahaaaaa kazi ipo
CC: zumbemkuu MANI saudari
Hapana acha FBI waje mana wapelelezi wetu police na majeshi yote yanafanya kwa maelekezo ya ccm na kuweka weledi kando hawa watachimbua swala lote na kuwakamata uamsho na mizizi yao yote including Ilunga hawa jamaa wanafanya kwa weledi sio kisiasa!!
 
Mkuu wa Usalama wa Taifa la JF steveachi anaunga mkono Hoja
 
Last edited by a moderator:
Yap hawa jamaa hawanaga masikhara jwenye kazi zao...naona mambo yashaanza kuwa mambo sasa...
 
Kuna mambo ambayo unaweza kusema kuwa tufanye sisi wenyewe kwanza, tukishindwa tutaomba msaada toka nje.

watanzania ni muhimu tukajitambua. Hivi sisi ni nini ambacho huwa tunafanya wenyewe kikawa na ufanisi hata tufikirie kuwa tuna uwezo wa kufanya upelelezi kwa umakini? Makanisa mangapi yamechomwa moto mpaka sasa? Yameanza kuchomwa tangu lini? Padre Mkenda alipigwa risasi lini? Wangapi mmewakamata mpaka sasa? Shekhe alimwagiwa tindikali lini, na ni watu wangapi mmewakamata? Tusijidanganye, hatuna uwezo, na wakati mwingine hata tukiwa na uwezo, hatuna dhamira, na wala hatuna uzalendo. Mnasema tufanye wenyewe wakati watu wanaendelea kuuwawa, makanisa yanaendelea kuchomwa na wahalifu wanazidi kujizatiti? Hivi tutakapokuwa tunasema kwanza tufanye wenyewe, kabla ya kupata jibu, padre/mchungaji mwingine akauawa, bado tutaonekana tulifanya uamuzi wa busara.

Kung'ang'ania kuwa upelelezi tufanye wenyewe wakati mambo mengine hatufanyi wenyewe ni kuionea sekta ya ulinzi na usalama.

Barabara nzuri zinajengwa na makampuni ya nje. Viwanja vya ndege vinajengwa na makampuni ya nje. Njia kuu za umeme zinajengwa na makampuni ya nje. Vituo vya kuzalishia umeme vinajengwa na makampuni ya nje. Mitambo yote tunayotumia nchini ikiwa pamoja na vyombo vya usafiri vinatengenezwa na makampuni ya nje. Kama haya yote hatuwezi kufanya, kwa nini tufikirie kuwa tuna uwezo kwenye ulinzi, usalama na kazi za kijasusi? Tunapenda kuwa na uwezo lakini uwezo hatuna kwa sababu hatuna mipango ya kuweza kufanya chochote. Sasa tuwaache hao watu wa nje watusaidie ili angalao tu tuishi kwa matumaini makubwa zaidi.

Mkuu nikiwa kama raia wa tanzania sikubali hata mara moja kuhusiana na hili.hii siyo ishara nzuri ni bora vyombo vyetu vikafanya kazi ndo wakihitaji msaada ndo wawaite wenzetu.sikubali hata mara moja na nitakuwa wa mwisho kuamini kuwa vyombo vyetu vimeshindwa nina imani navyo sana.

Ila nadhani tuwe watu makini katika kuhakikisha maamuzi mengine ya kisiasa hayatuadhiri mustakabathi wa nchi yetu. Hii natolea mfano kwa wenzetu wa kenya wao walikataa mara nyingi hata kama ulibahatika kumsikiliza wagombee wa urais kwenye mdahalo walitaka kwanza wale watu waliopelekwa hague watendewe haki kenya na sio the hague. Lazima tuvipe kipaumbele vyombo vyetu kwanza ndo tukishindwa tuombee msaad. Tanzania nakupenda sana
 
  • Thanks
Reactions: mob
Usalama wa Taifa tunaulipa mishahara ya kazi gani? Tunashindwaje kukamata wa halifu wenyewe mpaka tuagize watu kutoka nje? Hawa watu kiusalama tunawaamini vipi? Watanzania tunahitaji kufanya maamuzi ya haraka sana na siyo lazima 2015 hata sasa ikibidi tufanye hivyo, kwa hali hii nchi ulinzi ni zero... Aliyesema JK ni chaguo la mungu na alaaniwe milele... Tunawalipa kiasi gani cha fedha na zinatoka wapi? Wanakaa kwa siku ngapi? Taifa liwekwe wazi!

kwa sasa watu wa TISS wako likizo,tumeamua kuajiri wageni,TZ no ina tatizo
 
Usalama wataifa wameshindwa hata kumkamata Ilunga!!!?? Nchi hii IMEOZA kila idara...

TISS wamebaki kututishia amani huku mtaani; utawasikia unajua mie nan? Na ukzubaa katoa bastola
 
Back
Top Bottom